Uchaguzi 2020 Dar es Salaam: Watu watatu zaidi wakamatwa kuzuia maandamano

Uchaguzi 2020 Dar es Salaam: Watu watatu zaidi wakamatwa kuzuia maandamano

Maandamano & Sheria Husika

Sheria ya Jeshi la Polisi ya mwaka 1961 na marekebisho yake ya mwaka 1995, ambayo ndiyo huelekeza na kuongoza kuhusu njia na namna ya kuendesha maandamano nchini, inasema:

(1) Mtu yeyote ambaye ana mpango wa kufanya, kukusanya, kuunda au kupanga mkusanyiko au maandamano ya hadhara, kwa muda usiopungua saa 48 kabla ya mkusanyiko au maandamano kwa muda uliopangwa kuanza, atawasilisha kwa maandishi notisi kuhusu kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano hayo kwa afisa polisi msimamizi wa eneo hilo akianisha:

(a) Sehemu na muda ambao mkutano utafanyika;
(b) Dhumuni kwa ujumla kuhusu mkutano huo; na
(c) Maelezo mengine kama Waziri atakavyotangaza kwa notisi, mara kwa mara kwenye Gazeti la Serikali.

(2) Pale ambapo mtu amewasilisha taarifa kulingana na kifungu kidogo cha (1), anaweza kuendelea kuitisha, kukusanya, kuunda, au kuandaa mkusanyiko au maandamano hayo kama yalivyopangwa isipokuwa pale atakapopokea amri kutoka kwa afisa polisi msimamizi wa eneo husika ikielekeza kwamba mkusanyiko au maandamano hayo hayatafanyika kama ilivyotaarifiwa.

(3) Afisa polisi ambaye taarifa imewasilishwa kwake kulingana na kifungu kidogo cha (1), hatatoa amri ya kusitisha chini ya kifungu kidogo cha (2) kulingana na taarifa husika, isipokuwa ameridhika kwamba kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano hayo kuna uwezekano wa kusababisha kuvunjika kwa amani au kuathiri usalama wa taifa au kudumisha amri kwa umma au kutumika kwa dhumuni lolote lisilokuwa halali.

Hii ndiyo sheria inayoongoza Jeshi la Polisi kwa maana rahisi maandamano ni mpaka pale jeshi la polisi limekubali na kutoa kibali baada ya waandamanaji kuomba kibali hicho.

Vyovyote vile, kuhusu maandamano hayo, jeshi la polisi linapaswa lijiridhishe pasipo shaka kuwa hayahatarishi maisha au kuleta madhara yoyote na hayataingilia haki za watu wengine ambao hawataki kuandamana.

NINI KINACHOWEZA KUTOKEA?

Kinachoweza kutokea baada ya katazo la jeshi la polisi, ni kujitokeza kwa watu wenye nia ya kutaka kuandamana kwa nguvu. Ukifanya hivyo moja kwa moja utakuwa unatenda kosa la UHAINI ambalo ndilo kosa kubwa kuliko yote nchini kwa mujibu wa ibara ya 28 ya Katiba yetu.

Sheria inasema kwamba kama ukifanya yafuatayo utakuwa umefanya uhaini katika Jamhuri ya Muungano:

(a) Kifungu cha 39 (1) cha kanuni za adhabu kinasema kuwa mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote akajaribu kumuua Rais, atakuwa ametenda uhaini.

(b) Mtu yeyote aliye ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote akaanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano atakuwa naye ametenda kosa la uhaini.

(c) Mtu yeyote ambaye yuko ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri, kuhusu kifo, kumlemaza, kumzuia, au kufungwa kwa Rais atakuwa ametenda uhaini.

(d) Mtu yeyote ambaye yuko ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kumwondoa Rais madarakani visivyo halali atakuwa ametenda kosa la uhaini.

(e) Mtu yeyote ambaye yuko ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kumwondolea Rais heshima na jina la mkuu wa nchi, amiri jeshi mkuu, au kiongozi mkuu wa serikali atakuwa ametenda kosa la uhaini.

(f) Mtu yeyote ambaye yuko ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kupindua serikali iliyo madarakani, kutishia serikali, bunge au mahakama atakuwa ametenda kosa la uhaini.

ADHABU
Kwa mtu yeyote atakayekutwa na hatia ya kutenda kosa la uhaini, adhabu yake ni kifo; na sheria hiyo ya kifo imeelezwa katika kifungu cha sheria namba 39 na 40 cha kanuni za adhabu.

Hivyo, Watanzania kwa umoja wetu tunapaswa kuzijua sheria za nchi yetu ili kuweza kujiepusha kutenda makosa ya jinai dhidi ya nchi yetu.
 
Huyo ACP aache uzushi wakishamba, anaanzaje ku flip maneno kutoka "maandamano ya amani" kuwa "vurugu"?
Maandamano ya amani ni yale pekee yenye kibali. Niambie haya maandamano yenu kibali chake kipo wapi?
 
Unafukuza Watu kazi kwa vyeti FEKI Halafu Unaingia Madarakani Kwa Kura FEKI [emoji23][emoji23]
IMG-20201101-WA0032.jpg
 
Huyo ACP aache uzushi wakishamba, anaanzaje ku flip maneno kutoka "maandamano ya amani" kuwa "vurugu"?

Hapo ndipo penye Sababu ya Msingi ,Maandamano ambayo yapo kisheria yanakuwaje ni vurugu !?.Ume wakamata kabla ya kuandamana una thibitishaje nia yao ilikuwa ni ovu !?.

Afrika yetu hiyo Mkuu.
 
Hatukutaki humu Leo, nenda kaandamane hujaambiwa uwe ripota [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] saa mbil kasoro hii
Hivi kuwa msukule wa mbogamboga ni lazima usiwe na ubongo!?
Kuna mtu aliyekupa kuwa msemaji wake humu JF!?
Siki nyingine zungumzia nafsi yako pekee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maandamano ya amani ni yale pekee yenye kibali. Niambie haya maandamano yenu kibali chake kipo wapi?
Hili nalo la kuuliza?

Kwa serikali ilicho kifanya kwenye uchaguzi huu ulitegemea watakua tayari kutoa kibali?

Kama adui wa huu uchaguzi ni serikali, na serikali ndio inayo authorized hicho kibali we kwa akili yako ulitegemea kupatiwa kibali katika mazingira hayo?
 
Kwamba........
Waliokuwa wanatakiwa kuandamana wametakiwa kuchoma matairi barabarani, kuchoma magari, vituo vya mafuta na masoko wameahidiwa pesa.

Pia watu wanaotumika kushawishi wanaambiwa wawatafute vijana wasio waoga, wanaotumia dawa za kulevya..🤨😲😲
Duhhhhhhh....
Nimejikuta nasikitika sana
Wewe unawaamini maccm?!
Huo ni uzushi tu Kama kawaida yao
 
Hili nalo la kuuliza?

Kwa serikali ilicho kifanya kwenye uchaguzi huu ulitegemea watakua tayari kutoa kibali?

Kama adui wa huu uchaguzi ni serikali, na serikali ndio inayo authorized hicho kibali we kwa akili yako ulitegemea kupatiwa kibali katika mazingira hayo?
Ulitaka ashinde nani ili uone haki imetendeka?
 
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ACP Lazaro Mambosasa amesema wamewashika watu watatu zaidi kwa tuhuma za kuwashawishi watu kuandamana...
Huu ni upumbavu mtu kuwakata watu kwa vitu ambavyo havijafanyika na isitoshe ni maandamano ya Amani siyo fujo
 
Ulitaka ashinde nani ili uone haki imetendeka?
Ashinde aliye stahili kushinda, na sio kwa ushindi wa kura za wizi ambao hata mtoto mdogo huwezi kumdanganya kuwa ni ushindi wa halali
 
Hili nalo la kuuliza?

Kwa serikali ilicho kifanya kwenye uchaguzi huu ulitegemea watakua tayari kutoa kibali?

Kama adui wa huu uchaguzi ni serikali, na serikali ndio inayo authorized hicho kibali we kwa akili yako ulitegemea kupatiwa kibali katika mazingira hayo?
Hao wa kuandamana wako wapi ?
Nenda kwnye page za viongozi wako uone wanavyojibiwa
 
Back
Top Bottom