Uchaguzi 2020 Dar: Jeshi la Polisi lasitisha wito wake kwa Tundu Lissu, lamtaka aendelee na Kampeni zake

kama nime elewa vizuri wito bado uko pale pale ila anatakiwa kuripoti mkoa wa kipolisi Kilimanjaro, na hii ni Zaidi ya ngonjera ya policcm
1. Kwa hiyo barua za wito zilikuwa mbili ya RPC K"njaro na Dsm kwa kosa moja?.
2. Sirro alivyodai aliongea na Mbowe naye alikuwa anasisitiza Lissu ashauriwe aitikie wito gani?.
3. Ni barua gani Lissu anayodai haijataja kosa kati ya hizo mbili?
4. Mambosasa anaposema aendelee tu na kampeni mpaka 28 Oct. ina maana amefuta hata wito wa RPC mwenzake wa Kilimanjaro?.
Nashauri maagizo, wito na maelekezo kwa ngazi ya wagombea Urais yakawa yanatolewa na Ofisi ya IGP tu hata kama mgombea atafanya kosa akiwa mkoa wowote. RPCs wawe wanapeleka malalamiko kwa IGP na kupokea maagizo ya kutekeleza toka kwake kutaepusha mkanganyiko huu.
 
Kwa hali ya kawaida Lissu huyu ana ratiba ya mikutano, Mahera anamumhitaji, polisi wamhitaji. Lengo ni kumtoa kwenye reli . Acheni uchaguzi ufanyike Watanzania waamue hatima yao.
 
[emoji2]
Jamani narudia tena Lissu sio Slaa, Lissu sio Lowasa Lissu sio Mbowe,
Tundu Lissu is Another level..... ndio maana waliona namna pekee ni kumuua lkn kumbe mbeba maono wataifa anapitishwa tu kwenye tanuli la moto ili arudi akiwa imara zaidi
 
Ukiingia JF waweza kudhani Lissu atashinda kuwa Raisi. Ukweli ni kwamba Lissu hatakaa awe Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Sio 2020 ni kamwe(NEVER), hatakaa awe Raisi wa nchi hii. Ila kikatiba mnaruhusiwa kujitekenya na kucheka wenyewe mitandaoni masaa 24(24/7). Tarehe moja mwezi ujao ndo mtaelewa ninachomaanisha hapa.
 
Sasa tume kama kuwatuwengine wanatuchanganya kutoka nyie tume ni police tafadhalini msituharibie nchi yetu sasa nyie mmekosea na police pia wamekosea naniawajibike hapo?
 
Kama ni kweli wamechukua hayo maamuzi basi wametumia Busara.
 
Mh Tundu Lissu & Wafuasi wako
mnayo kila sababu kusherehekea "USHINDI" huu wa kishindo!

Hongereni sana Makamanda kwani Jeshi la Polisi "LIMEWAOGOPA" nyie na Mgombea wenu ambaye ni Mwanasheria Mbobezi!

Sisi tumekubali kushindwa kwenye mechi hii na nyinginezo zote zitakazochezwa KABLA YA OKTOBA 28, 2020!
 
Sasa tutaacha lini kuwategemea kama kila tukitaka kujikwamua tuache kuwategemea, kina Lisu wanakuja na kauli kwamba hatuwezi kuishi bila wao mabeberu? Na huyo mtu kumbuka anataka kuwa rais lakini ana akili za nama hiyo,!
Ndio unaona sasa hadi hao beberu wake wamejitokeza hadharani kabisa wanampigania awe rais ili sasa rasmi tusifanye chochote bila wao kuamua!

Nakwambia hivi, oktoba hii Tutampiga yeye Lisu na huyo bebru wake,
 

mwenye mpira ndiye anachagua nani na nani wacheze.
 
Wananchi wenye busara wamewashauri polisi kuachana na Lisu kwakua uu uchaguzi amesha shindwa kwaiyo anatafuta pa kuangushia lawama.
Ameshashindwa!!!! Kwani tumeshapiga kura, kura zimeshahesabiwa na matokeo yameshatangazwa?
 
Wananchi wenye busara wamewashauri polisi kuachana na Lisu kwakua uu uchaguzi amesha shindwa kwaiyo anatafuta pa kuangushia lawama.
Kweli huu mwaka mtaimba hadi kichina kura zinepigwa wapi na zimehesabiwa wapi mkiambiwa mambulula mnavimba na badoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…