Kukichwa kutapambazuka..!Lijuakali , Nassary , Silnde na wasaliti wengine jiandaeni
Kila kitu alichotia mkono Ndugai kitaporomoka tu.Leo hii saa 8 Mchana, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam itatolea uamuzi Mapingamizi yaliyowekwa na Mawakili wa Chadema dhidi ya waliotimuliwa kwenye chama hicho wanaoongozwa na Halima Mdee , ikiwa kama walistahili kufungua kesi hiyo au la.
Halima Mdee na kikundi chake wamefungua kesi kwenye Mahakama hiyo wakipinga kufutwa uanachama .
=====
Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imeitupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Halima Mdee na Wenzake 18 kupinga kuvuliwa uanachama na CHADEMA, ikikubaliana na pingamizi la CHADEMA lililopinga kufunguliwa kwa shauri hilo kinyume cha sheria.
Ni Kesi ya Madai namna 13 ya Mwaka 2022 iliyofunguliwa na Halima Mdee na wenzake 18 wakipinga CHADEMA kuwavua uanachama kitu kinachopelekea kupoteza Ubunge wao
Pia, soma;
Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi
CHADEMA yaweka Mapingamizi 6 Kesi ya Ubunge wa Halima Mdee na wenzake. Mahakama Kuu kuamua 22/06/2022
Wabunge 19 kufungua kesi, vigogo CCM na ofisi ya Spika wahusishwa katika uratibu
Yaliyojiri kesi ya Wabunge 19 waliovuliwa uanachama Vs CHADEMA. Mahakama yaridhia Ubunge wao uendelee wakati kesi ikiendelea
🤣🤣🤣Huwezi kupata ujaji kama sio mwanachama hai.Kwa mahakama ya Tanzania, tusitegemee miujiza... Majaji wote ni Ccm.
Hawawezi kuwahadaa kirahisi namna hiyo. Kitakachofuata ni kwamba serikali itabidi irejeshe kile kiwango cha mchango wa nchi husika zinazotoa kwa ajili ya ku-support demokrasia katika nchi maskini. Lakini kuna uwezekano kwa sasa kuliongelea na kulilainisha baada ya mabadiliko yaliyotokea.Wanawahadaa wafadhili
Upo sahihi kabisaaa, na ndo kinachofanyika sasa.Unadhani Jaji atakuwa against na Maamuzi ya serikali. Ataiondoa then atawapa order ya kurekebisha maombi Yao within 7 days
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Ngoja tumsikie Tulizwa aksoma atasemaje...
1. CCM imeridhia mchakato wa KATIBA mpya uanze.Leo hii saa 8 Mchana, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam itatolea uamuzi Mapingamizi yaliyowekwa na Mawakili wa Chadema dhidi ya waliotimuliwa kwenye chama hicho wanaoongozwa na Halima Mdee , ikiwa kama walistahili kufungua kesi hiyo au la.
Halima Mdee na kikundi chake wamefungua kesi kwenye Mahakama hiyo wakipinga kufutwa uanachama .
=====
Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imeitupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Halima Mdee na Wenzake 18 kupinga kuvuliwa uanachama na CHADEMA, ikikubaliana na pingamizi la CHADEMA lililopinga kufunguliwa kwa shauri hilo kinyume cha sheria.
Ni Kesi ya Madai namna 13 ya Mwaka 2022 iliyofunguliwa na Halima Mdee na wenzake 18 wakipinga CHADEMA kuwavua uanachama kitu kinachopelekea kupoteza Ubunge wao
Pia, soma;
Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi
CHADEMA yaweka Mapingamizi 6 Kesi ya Ubunge wa Halima Mdee na wenzake. Mahakama Kuu kuamua 22/06/2022
Wabunge 19 kufungua kesi, vigogo CCM na ofisi ya Spika wahusishwa katika uratibu
Yaliyojiri kesi ya Wabunge 19 waliovuliwa uanachama Vs CHADEMA. Mahakama yaridhia Ubunge wao uendelee wakati kesi ikiendelea
Nchi inafunguka, hofu inazidi kutoweka miongoni mwa waliopewa dhamana ya kuamua kwa haki.
Maana wengi walikuwa na khofu ya kutoa maamuzi ambayo yangemuudhi aliyewateua kushika nyadhifa hizo kubwa na nyetu ktk ofisi za umma au mihili inayojitegemea.
Jaji Siyami si ndiye Jaji m mchongo mwandamizi aliyehongwa cheo baada ya kuwafsnyia mtimanyongo kina Mbowe?Mambo yanaenda kwa kasi, hadi jaji kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania anasema kuwa vyombo vya habari vinaanza kuchukua nafasi yake ktk kazi ya kuripoti kesi mbalimbali ili wananchi wapate ufahamu
Jumatano, 22 Juni 2022
‘VYOMBO VYA HABARI DARAJA MUHIMU KWA MAHAKAMA NA WANANCHI’
Na Faustine Kapama– Mahakama, Lindi
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani amesema vyombo vya habari ni daraja muhimu baina ya Mahakama na wananchi, hivyo vinapaswa kushiriki katika kujenga taswira chanya ya Mahakama kwa kuuhabarisha umma kuhusu mambo mazuri yanayotokea mahakamani ili kukuza imani ya wananchi.
Mhe. Jaji Kiongozi Siyani ameyasema hayo katika siku ya pili ya ziara ya Tume ya Utumishi wa Mahakama chini ya Mwenyekiti wake, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ambayo leo tarehe 21 Juni 2022 imetembelea Mkoa wa Lindi kuzungumza na watumishi na wadau wa Mahakama.
“Vyombo vya Habari ni daraja muhimu baina ya mahakama na wananchi. Msiishie kukosoa mambo yanapokwenda mrama, lakini tusemeeni kwa kuyatangaza zaidi mazuri yanayofanywa na Mahakama zetu ili kujenga na kukuza imani ya wananchi kwa vyombo hivi vya haki,” amesema.
Mhe. Jaji Kiongozi Siyani amesema vyombo vya habari ni wadau wakubwa wa Mahakama na katika kutimiza jukumu lake la kutoa haki, ni lazima wananchi inayowahudumia wawe na imani na chombo hicho na wanapaswa kufahamu juhudi zinazofanywa na Mahakama katika kuboresha huduma zake za kutoa haki.
Kwa mujibu wa Mhe. Jaji kiongozi Siyani, vyombo vya habari vina mchango wa kujenga taswira ya Mahakama kwa umma ambapo dhamira ya vyombo hivyo kupitia kazi zao inaweza kujenga picha chanya au hasi kwa Mahakama.
Aliotoa mfano kuwa kama vyombo vya habari vitajikita kuandika mabaya pekee, imani ya wananchi itashuka na hilo likitokea Mahakama itapoteza uhalali wa uwepo kwake na watu wataamua kujichukulia sheria mkononi.
Hakuna mtu atakayekuwa salama kuishi kwenye nchi ambayo watu wake wanajikulia sheria mkononi,” ameonya Jaji Kiongozi.
“Kwa hiyo, bila kuathiri uhuru wa vyombo hivi katika kutoa habari zinazofichua uovu kwa lengo la kurekebisha na kuboresha, matarajio yetu pia kuwa vyombo vya habari vitatumia nafasi yake kushiriki katika kujenga taswira chanya ya Mahakama kwa kuuhabarisha umma kuhusu mambo mazuri yanayotokea mahakamani ili kukuza imani ya wananchi kwa mahakama zao,” amesema.
Jaji Kiongozi pia alizungumzia kuhusu Ofisi ya Mwendesha Mashtaka ambapo Mkurugenzi wa Mashtaka na wote wanaofanya kazi chini yake wanapaswa kuongozwa na misingi iliyowekwa na Katiba ya nchi kupitia ibara ya 59B (4) ambayo ni kutenda haki, kutokutumia madaraka vibaya, kuzingatia maslahi ya umma.
Amesema hayo ni mambo ambayo kila anayefanya kazi chini ya ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka anapaswa kuyaishi.
“Mahakama inatarajia kwamba ofisi ya Taifa ya Mashtaka itafanya kazi kwa kuzingatia misingi hiyo na kama hilo litafanyika na kwa kuwa ofisi hii ndiyo inayosimamia upelelezi wa makosa ya jinai, basi hakutakuwa na mlundikano wa mahabusu wa muda mrefu magerezani. Aidha kukamilika kwa upelelezi ndani ya muda mfupi kutawezesha Mahakama pia kusikiliza mashauri husika kwa kasi,” amesema.
Jaji Kiongozi pia amewataja Afisa Huduma kwa Jamii kuwa ni mdau muhimu katika kupendekeza adhabu mbadala kwa watuhumiwa waliotiwa hatiani kwa makosa ambayo adhabu husika ni chini ya miaka mitatu kama inavyobainishwa katika kifungu 3(1) (4) cha Sheria (the Community Services Act (Cap. 291 R.E. 2019).
Amesema maafisa huduma kwa jamii wana jukumu la kuwasilisha uchunguzi wa kijamii wa watuhumiwa ambao wanastahili adhabu mbadala kwa makosa ya jinai kabla ya adhabu husika kutolewa kwa mujibu wa kifungu 3(1)(4) cha Sheria (the Community Services Act (Cap. 291 R.E. 2002).
Soma zaidi : source : ‘VYOMBO VYA HABARI DARAJA MUHIMU KWA MAHAKAMA NA WANANCHI’
Ndungai ana kimaviKila kitu alichotia mkono Ndugai kitaporomoka tu.
Inaweza ikawa spinning ndani ya spinning!!1. CCM imeridhia mchakato wa KATIBA mpya uanze.
2.Mahakama imetupilia mbali pingamizi la wabunge feki 19.
3. Treni imepata ajali na kuanguka na kuua watu zaidi ya Saba, TRC wadai ni HUJUMA.
Ipi hapo ni habari Hasa.?
Tushangilie bila kujisahau. Hujuma kivp? Tuchimbe zaidi. Amen
Pia oparesheni ya ngoro ngoro imetangazwa rasmi! spinning ndani ya spinning1. CCM imeridhia mchakato wa KATIBA mpya uanze.
2.Mahakama imetupilia mbali pingamizi la wabunge feki 19.
3. Treni imepata ajali na kuanguka na kuua watu zaidi ya Saba, TRC wadai ni HUJUMA.
Ipi hapo ni habari Hasa.?
Tushangilie bila kujisahau. Hujuma kivp? Tuchimbe zaidi. Amen
Mnapomtaja Pasco kama Mwanasheria huwa nasikitika Sana.Kabisa mkuu, Halima hakumbuki chochote kwenye sheria zaidi ya kujisifia kuwa ana degree ya sheria. Na hapo alipo anaogopa hata kuomba kazi kwenye law firm maana anajua ataumbuka. Huko nje Mbowe alikomuombea kwa vyovyote Mdee angegoma maana hana uwezo tena zaidi ya kupiga porojo kwenye majukwaa ya siasa na bungeni.
Huyu Halima Mdee namafananisha na member mkongwe huku jf Paskali Mayalla, zaidi ya kujisifia kuwa ana degree ya sheria, hajawahi kufanya hiyo kazi popote zaidi ya kupiga porojo huku mtaani. Na sasa hivi ukisema aende mahakamani ataishia kuwa kituko.
Lijualikali nimemuona wiki mbili zilizopita eti kawa cheki Bob!Lijuakali , Nassary , Silnde na wasaliti wengine jiandaeni
Nimeona application Yao Ambayo ni mpya Jana Jioni still Bado Kuna P.O asa asa kwenye verification clauseJambo la msingi ni kwamba wanayo nafasi ya kupeleka tena maombi yao upya.
Hiyo sio fatal.Nimeona application Yao Ambayo ni mpya Jana Jioni still Bado Kuna P.O asa asa kwenye verification clause
Wanarekebisha au wanafile fresh suit? Kumbuka affidavit haiwezi kuwa amended, mm mwanzo nilijua Baada ya kugundua Yale makosa Wangeomba ku-withdraw in order to refile a fresh suit Ila wakakomaa halafu pia nilijua watafile joint affidavit.Wanarekebisha maombi yao halafu wanayarejesha tena.
Ngoma bado mbichi.