mlima wa mizeituni
JF-Expert Member
- Sep 7, 2019
- 1,385
- 2,460
Ungemtia kofi kumuweka sawa!Najua vijana ni wabishi. Nakumbuka siku moja kulikuwa na msongamano na kijana kama 45 years akawa anachomekea. Nikafungua kioo nikamweleza kistaarabu kuwa utanigonga. Yeye naona bilauli ilishaingia kichwani, akaanza, we mzee Acha ushamba, endesha gari, mara nyie ndiyo mmejifunzia magari uzeeni. Mie kimya tu, sijakaa sawa akanigonga. Mimi nikazima gari, nikatoka nje; si akanivaa mara atake kuongea kwa kunigusa, nikamweleza tafadhali usiniguse maana nipo loaded. Ha ha ha, ilikuwa ni balaa, mara aseme huyu anataka kuniua mara anaringa kuwa ana pistol! Mpaka anaeleza watu kuwa nimemuonesha pistol wakati ukweli sikuwa nayo wakati ule. Mimi nilikuwa namthale tu, ingawa sikuwa nasubiri Kithibiti. Kijana alikuwa na maneno ya shombo yule na ulevi wake, nadhani ningelikuwa Alex nami sijui ila uzee Achana nao.
Kwa mantiki hiyo si ajabu Zawadi -gift au kichagga jifuti, alijitoa Zawadi kwa maneno ya shombo na Alex akafanya kweli. Midomo ni hatari
Ilitakiwa atambue anaongea na nani.. [emoji16][emoji16][emoji16]