Dar: Mvua kubwa sana imenyesha usiku wa kuamkia leo 21/01/2024

Dar: Mvua kubwa sana imenyesha usiku wa kuamkia leo 21/01/2024

Mtihani kwa serikali ya mkoa wa Dar es Salaam kuwa na viongozi wabunifu, badala ya kuwaza kuzuia maandamano ya tarehe 24 January 2024
1705814793830.png

Picha : RC Albert Chalamila mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam

Kingo za mito na vijito vinaweza kabisa kuimarishwa na kuzuia majumba ya wakaazi wa Dar es Salaam kuanguka kutokana na maporomoko ya kingo za mito

Picha ikionesha kingo za mifereji, vijito ilivyoliwa jijini Dar es Salaam na kupelekea makalavati, madaraja kujaa mchanga
1705814519581.png

Wanafunzi wa kitivo cha uhandisi chuo kikuu tajwa kongwe UDSM kwa kushirikiana na halmashauri ya Ubungo TAMISEMI wangeweza kutumia kodi za wananchi vizuri na wanafunzi wa UDSM kujifunza kwa vitendo kujenga kuimarisha kingo za mifereji, vijito na mito ya maji hatimaye majina yao kuingia ktk rekodi kumbukizi tukuka kuwa elimu imewezesha kutatua changamoto katika jamii .

Picha chini toka maktaba ikionesha changamoto endelevu zinazolikabili jiji na pia mkoa wa Dar es Salaam
1705814201397.png
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja. Mvua kubwa sana inanyesha mahali hapa sijapata kuona. Haki tangu nizaliwe sijawahi kushuhudia mvua kubwa kiasi hiki.

Serikali ijiandae kukabiliana na adhari za mafuriko zitakazsababishwa na mvua hii kwani kadri muda unavyoenda mvua inazidi kuongezeka

Mara ya mwisho mvua iliponyesha ilingo'a madaraja na kuua watu watatu. Safari hii tujiandae kwa maafa zaidi.

Tuambie mahali ulipo hali ikoje na nini tutarajie baada ya mvua hii.

Nawasilisha.

UPDATES
Mawasiliano kati ya Tegeta na Kunduchi yamekatika baada ya daraja la Kunduchi-Mtongani kukatika. Magari, nyumba na mali za raia zimesombwa na maji. Nguzo za umeme zimeanguka na baadhi ya raia wamefariki. Tatizo watu wamejenga karibu na mto kwa kupewa vibali na maofisa ardhi wa serikal.

Hadi sasa mvua inaendelea kunyesha baadhi ya maeneo hapa Dar. Serikali itoe tahadhari kwa wananchi na ichukue hatua kukabiliana na mafuriko.

Nitaendelea kuwapa updates na picha kadri nitakavyozipata.........
Tatizo watu wamejenga karibu na mto kwa kupewa vibali na maofisa ardhi wa serikal.[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna nabii alitabiri,Dar kufikia mwezi Mei mwaka huu,itafunikwa na maji,kwamba kuna Tsunami itaipiga Dar.
Huenda hizi mvua ni maonyo ya mwisho.Watu wa Mungu watamuuliza Mungu ukweli wa unabii huu.Ila walio wengi waliposikia unabii huo,walimdhihaki mtoa unabii.

Biblia inasema "msiutweze unabii,bali zipimeni roho kama zimetokana na Mungu au la!
Nabii wa mchongo [emoji3]

Tsunami na mvua ni vitu viwilli tofauti...
 
Kuna nabii alitabiri,Dar kufikia mwezi Mei mwaka huu,itafunikwa na maji,kwamba kuna Tsunami itaipiga Dar.
Huenda hizi mvua ni maonyo ya mwisho.Watu wa Mungu watamuuliza Mungu ukweli wa unabii huu.Ila walio wengi waliposikia unabii huo,walimdhihaki mtoa unabii.

Biblia inasema "msiutweze unabii,bali zipimeni roho kama zimetokana na Mungu au la!
Huyo nabii mchumiatumbo kweli. Hahaha!
 
Watu wengi wamejenga kwenye njia za maji, Dar ina vijimilima upande wa magharibi na kaskazini ambavyo wakati wa mvua hukusanya maji na kuyapitisha kwenye mikondo na mabonde kadhaa kwenda baharini...

Sasa ujenzi holela umeingilia hizo njia za maji, na kama ilivyo ada iwe isiwe lazima maji yatafute njia mbadala ya kwenda uwanda wa chini...
 
Back
Top Bottom