Naingia kwenye mada moja kwa moja. Mvua kubwa sana inanyesha mahali hapa sijapata kuona. Haki tangu nizaliwe sijawahi kushuhudia mvua kubwa kiasi hiki.
Serikali ijiandae kukabiliana na adhari za mafuriko zitakazsababishwa na mvua hii kwani kadri muda unavyoenda mvua inazidi kuongezeka
Mara ya mwisho mvua iliponyesha ilingo'a madaraja na kuua watu watatu. Safari hii tujiandae kwa maafa zaidi.
Tuambie mahali ulipo hali ikoje na nini tutarajie baada ya mvua hii.
Nawasilisha.
UPDATES
Mawasiliano kati ya Tegeta na Kunduchi yamekatika baada ya daraja la Kunduchi-Mtongani kukatika. Magari, nyumba na mali za raia zimesombwa na maji. Nguzo za umeme zimeanguka na baadhi ya raia wamefariki. Tatizo watu wamejenga karibu na mto kwa kupewa vibali na maofisa ardhi wa serikal.
Hadi sasa mvua inaendelea kunyesha baadhi ya maeneo hapa Dar. Serikali itoe tahadhari kwa wananchi na ichukue hatua kukabiliana na mafuriko.
Nitaendelea kuwapa updates na picha kadri nitakavyozipata.........