Dar: Mvua kubwa sana imenyesha usiku wa kuamkia leo 21/01/2024

Mtihani kwa serikali ya mkoa wa Dar es Salaam kuwa na viongozi wabunifu, badala ya kuwaza kuzuia maandamano ya tarehe 24 January 2024

Picha : RC Albert Chalamila mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam


Kingo za mito na vijito vinaweza kabisa kuimarishwa na kuzuia majumba ya wakaazi wa Dar es Salaam kuanguka kutokana na maporomoko ya kingo za mito

Picha ikionesha kingo za mifereji, vijito ilivyoliwa jijini Dar es Salaam na kupelekea makalavati, madaraja kujaa mchanga
Wanafunzi wa kitivo cha uhandisi chuo kikuu tajwa kongwe UDSM kwa kushirikiana na halmashauri ya Ubungo TAMISEMI wangeweza kutumia kodi za wananchi vizuri na wanafunzi wa UDSM kujifunza kwa vitendo kujenga kuimarisha kingo za mifereji, vijito na mito ya maji hatimaye majina yao kuingia ktk rekodi kumbukizi tukuka kuwa elimu imewezesha kutatua changamoto katika jamii .

Picha chini toka maktaba ikionesha changamoto endelevu zinazolikabili jiji na pia mkoa wa Dar es Salaam
 
Tatizo watu wamejenga karibu na mto kwa kupewa vibali na maofisa ardhi wa serikal.[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nabii wa mchongo [emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Tsunami na mvua ni vitu viwilli tofauti...
 
Huyo nabii mchumiatumbo kweli. Hahaha!
 
Watu wengi wamejenga kwenye njia za maji, Dar ina vijimilima upande wa magharibi na kaskazini ambavyo wakati wa mvua hukusanya maji na kuyapitisha kwenye mikondo na mabonde kadhaa kwenda baharini...

Sasa ujenzi holela umeingilia hizo njia za maji, na kama ilivyo ada iwe isiwe lazima maji yatafute njia mbadala ya kwenda uwanda wa chini...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…