Dar: Mvua kubwa sana imenyesha usiku wa kuamkia leo 21/01/2024

Dar: Mvua kubwa sana imenyesha usiku wa kuamkia leo 21/01/2024

Nipo zangu moro mie nimetulia zangu. Huku mvua imepiga toka saa kumi alfajiri mpaka sasa ngoma inaendelea tuu. Wenye wake na mademu zao wanabingirika tuu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna nabii alitabiri, Dar kufikia mwezi Mei mwaka huu, itafunikwa na maji, kwamba kuna Tsunami itaipiga Dar.
Huenda hizi mvua ni maonyo ya mwisho. Watu wa Mungu watamuuliza Mungu ukweli wa unabii huu. Ila walio wengi waliposikia unabii huo, walimdhihaki mtoa unabii.

Biblia inasema "msiutweze unabii, bali zipimeni roho kama zimetokana na Mungu au la!
Ila taunami sio mvua.. ni kimbunga cha baharini..!! Unaweza ukawa na jua kali mikoa ya pwani ila taunami ikapiga. Ni mawimbi makubwa yenye nguvu ambayo yanatembea kwa kasi mpaka kutoka kwenye kingo zake na kuvamia nchi kavu...
 
[emoji23][emoji23][emoji23] week ilopita niliitwa home nikasabahi, nikajifanya mjanja kubaki mjini, woiiiiih

Leo naelea tyuuh hapa, uzuri mie kuogelea naweza wala sipati shida kupiga mbizi.
Mweeeeh
Kuelea hakutakusaidia cho chote mjukuu. Kitakachokuua ni mabati, mbao na makorokocho mengine yenye ncha kali yaliyomo humo kwenye maji. Liubao mchongoko likikukita kifuani na kutokeza upande wa pili hata kama unamzidi Michael Phelps katika uogeleaji ni kazi bure! Bado na electrocution kutoka kwenye nyaya zilizoanguka. Kimbia urudi Songea sasa hivi kama unaweza mjukuu! 🖐
 
Back
Top Bottom