Roving Journalist,
Hebu acheni kututisha na kutuweka roho juu.
Wakati Mo Dewji amefungua kesi ya kutekwa Polisi..., Kituo cha haki za binadamu wamefungua kesi dhidi ya kamanda Mambosasa cha ajabu sio kwa kosa la utekaji bali kumzuia lupango Tito Magoti bila kumpeleka mahakamani.
Kumbe kisheria watu hawa hawajatekwa ila huku Kwenye social media mnatulisha Matango pori na kutujaza sumu eti wametekwa.
Tuache kupotoshana makusudi, ni vema tuwe wakweli ili tuweze kuaddress matatizo ya ukweli ambayo kimsingi yapo makubwa tu, nasio kudanganyana eti Katekwa.
Watu wote tunajua namna Polisi wanakamata watuhumiwa ikiwemo kutumia nguvu ikibidi kulingana na mazingira, pia huenda mbali kwa kutesa watuhumiwa na wengine hupata ulemavu na hata kufa.
Wanavunja sheria na kanuni nyingi lakini kama tutaacha kusema ukweli badala yake tunaleta kosa lusilokuwepo haisaidii.
Jamaa mmoja humu amesema huwezi kuibiwa kitochi 4g smart halafu ukatangaza umeibiwa iPhone 11 pro. Watu hawatokuelewa.
Kama mtu katekwa halafu anapatikana kituoni Polisi basi tuwashitaki polisi kwa utekaji.