Matatizo mengi walionayo wanafunzi wanTanzania yanasababishwa na jamii i.e. watu wazima. Infact naweza kusema bila shaka kabisa kuwa tatizo siyo hao watoto bai tatizo ni jamii. Kwa wale walibahatika kuishi nchi zilizoendlea wanajua kuwa kwa maisha ya sasa simu ni kifaa muhimu sana na wanafunzi karibu wote humiliki simu mara wanapofikisha miaka 9 na kuendelea. Mbona hawana haya matatizo? Kwenye jamii yetu, inaonekana kama kumnunulia mtoto simu ni kumtuma afanye mahusiano ya ngono lakini ukweli ni kwamba jamii yetu ndiyo inaona/inatumia simu kama chombo cha mawasiano ya ngono. Hivyo basi watoto wanachofanya ni kuiga kutoka kwa wazazi wao. Siku hizi, asilimia kubwa kabisa ya wamiliki wa simu wanadhani na huzitumia kwenye mambo yanayohusiana na ngono.