Daraja la Tanzanite kufungwa kuanzia Januari 2, 2023 mpaka Januari 9, 2023

Daraja la Tanzanite kufungwa kuanzia Januari 2, 2023 mpaka Januari 9, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Dar es Salaam anawatangazia watumiaji wa daraja la Tanzanite kuwa daraja litafungwa siku ya Jumatatu tarehe 2 Januari 2023 kuanzia saa 12 asubuhi na kufunguliwa siku ya tarehe 9 Januari 2023 saa 12 asubuhi.

Sababu ya kufungwa ni ili kuweka nembo ya Tanzanite

1672548552469.png
 
Unafunga njia siku 7 kisa unaweka nembo?! Wajinga sana Makandarasi wetu hapo kinachoendelea ni wizi tu nembo inaweza kuwekwa usiku na asubuhi njia ikawa wazi. Ujinga ni ugonjwa mbaya sana.
Tumerogwa na alieturoga kafa! Si wangefunga saa nne usiku hadi saa 12 asubuhi wafanye kazi hayo masaa nane kila siku ?
 
Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Dar es Salaam anawatangazia watumiaji wa daraja la Tanzanite kuwa daraja litafungwa siku ya Jumatatu tarehe 2 Januari 2023 kuanzia saa 12 asubuhi na kufunguliwa siku ya tarehe 9 Januari 2023 saa 12 asubuhi.

Sababu ya kufungwa ni ili kuweka nembo ya Tanzanite

View attachment 2465081
Kuwa na wazee kwenye nafasi za maamuzi ni tatizo litakalo isumbua sana nchi hii.
 
Nahisi huenda Tanzania inaongozwa na watu waliolaaniwa sana. Tanzania haitatokea kuweza kuendelea milele chini ya hii serikali ya Mambuzi.

Kweli ufunge barabara muhimu kwa taifa kwa siku saba mfululizo kisa kuweka nembo tu?
 
Hili taifa liko nyuma kimaemdeleo sio kwa bahati mbaya, ni kwasababu ya mentality zetu, zimedumaa sana, na hii ni kwa wote hadi wasomi, japo wana vyeti vya kupendeza makabatini, lakini vichwani mwao hakuna kitu, kwa hali hii naona bado umasikini utaendelea kututoa jasho kwa miaka mingi sana ijayo.
 
Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Dar es Salaam anawatangazia watumiaji wa daraja la Tanzanite kuwa daraja litafungwa siku ya Jumatatu tarehe 2 Januari 2023 kuanzia saa 12 asubuhi na kufunguliwa siku ya tarehe 9 Januari 2023 saa 12 asubuhi.

Sababu ya kufungwa ni ili kuweka nembo ya Tanzanite

View attachment 2465081
Kwann hamkuweka hyo nembo wakat wa ujenz mnakuja sasa hiv kuleta usumbufu ambao hatuna tija?
 
Tumerogwa na alieturoga kafa! Si wangefunga saa nne usiku hadi saa 12 asubuhi wafanye kazi hayo masaa nane kila siku ?
Kwingineko duniani wachina waliwahi kubadili daraja lenye traffic ya magari 200,000 linalounga Beijing na route nyingi pale mjini ndani ya masaa 36. Kwa bongo huu ni mda unaohitajika kuhamisha faili kutoka meza moja kwenda kwa kiongozi ofisi ya juu
 
Back
Top Bottom