Daraja la Tanzanite kufungwa kuanzia Januari 2, 2023 mpaka Januari 9, 2023

Daraja la Tanzanite kufungwa kuanzia Januari 2, 2023 mpaka Januari 9, 2023

TAARIFA KUTOKA TANROADS KUHUSU DARAJA LA TANZANITE​

051C65BE-F3C5-4506-8F3C-8D9E3806EDC3.jpeg
 
Nembo imetugharimu bei gani sisi walipa kodi wazalendo?
Gharama thabiti za uboreshwaji wa nembo katika Daraja la Tanzanite kwa sasa hazipo wazi ingawa hili linalotekelezwa kwa sasa ni moja ya agizo kutoka kwa Mh. RAIS Dr. Samia Suluhu kwenda kwa waziri wa ujenzi pamoja na wakandarasi wa Daraja hilo..

Daraja hilo limekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Dar es Salaam kwa kupunguza foleni pamoja na kuwa kivutio cha utalii kwa wananchi ndani na nje ya Dar es Salaam.

Hadi kukamilika kwa daraja hilo gharama za ujenzi ni takribani Sh243 bilioni likifadhiliwa na Serikali ya Korea Kusini na kujengwa na kampuni ya ujenzi ya GS E&C, lilianza kujengwa mwaka 2018 na lilizinduliwa mwaka 2022.

Urefu wa daraja hilo ni kilomita 1.03, ikijumuisha njia nne za magari na njia mbili za watembea kwa miguu, pamoja na barabara unganishi zenye wa kilomita 5.2 na linaunganisha Hospitali ya Aga Khan na barabara za Obama, Kenyatta na Toures .
 
Back
Top Bottom