DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Hili jambo limekaa kiuwajibikaji sana
 
Huo msongamano wa abiria kwenye kituo chenu cha Kimara mida ya asubuhi,inaashiria jinsi gani kazi ya uendeshaji wa huo mfumo wa mabasi ya mwendo Kasi imeishawashinda,achieni ngazi mwachieni muwekezaji.
Hivi hawajapata mabus mapya hawa, zile bus zilizopigwa picha hazikuwa kwaajili ya huu mradi?
 
Nimerudi jana mjini kumbe ishu ya huu usafiri haijaisha bado!!!
Niliona picha za mabus nashangaa siyaoni barabarani
 
Mnaomba pongezi ?

Pongezi huwa inaombwa ?

Mwafrika hanaga logic, hata angesoma kiasi gani.
 
Wale wafanyabiashara wanaopanga bidhaa daraja la Kimara na kuzuia watumiaji wa daraja nani anafaidika na kadhia ile?
 
Kwa nini mnakata watu nauli ya 1000 badala ya 750!? Lini Hii ilitangazwa!? Kwa nini!? Huu ni wizi wa mchana kweupe na haukubaliki.
 
uzi umefufuka. sasa ivi akuna mwendokasi kuna mwendo polepole na tumesha piga kiberiti vituo vyote
 
Tunapenda kuwafahamisha wateja wetu wa Mabasi Yaendayo Haraka kuwa hairuhusiwi kulipa pesa taslimu kwenye ulipaji wa nauli abiria unatakiwa kulipa nauli yako kwa kutumia Kadi Janja ama Programu tumizi (App) ya Mwendokasi pekee. Kumejitokeza baadhi ya watumishi wasio waaminifu ambao kwa makusudi wanachukua pesa taslimu kutoka kwa wateja jambo hilo ni kinyume na utaratibu wa uendeshaji wa mradi wa BRT, kama abiria mzalendo kwa nchi na kwa maendeleo ya mradi tafadhali ukiona ama kukutana na uhalifu huo toa taarifa mara moja kwa Mamlaka (DART) kwa namba yetu ya bure 0800 110 147 ili hatua stahiki na za haraka za kisheria ziweze kuchukuliwa.
 
Ruti ya Kibaha mnairudisha lini? Mlete hata mabasi yale ya zamani
 
Ruti ya Kibaha mnairudisha lini? Mlete hata mabasi yale ya zamani
Mara bada ya kukamilika kwa miundombinu huduma hiyo itarejea , na taarifa rasmi itatolewa tafadhali endelea kutufuatilia kwenye mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Instagram, X ama zamani Twitter na Linkedin kwa anuani ya @DARTMwendokasi, pamoja na DART TV kwenye YouTube.
 
Huu mradi ni wa mabillion ya pesa
Phase 1 ya mwendokasi mlioperate kwa hasara mkashindwa kununua magari mapya na huduma ikawa mbovu kupindukia

Suluhisho
1.Badilisheni nauli kituo hadi kituo iwe TZS 1,300 - 1,500
2.Ongezeni operator mwingne kuwe na ushindan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…