DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu.

Kuna taarifa za uongo na uzushi zinasambaa kwenye baadhi ya kurasa za mitandao ya kijamii kwamba moja ya Basi la Mwendokasi lilisababisha ajali jana tarehe 14/6/2023 na kuua mama mjamzito eneo la Kariakoo, taarifa hizo ni zaa uzushi, uongo na uzandiki zenye lengo ovu la kuchafua Wakala na Serikali kwa ujumla , tunaendelea kufuatilia chanzo cha taarifa hizo ili tuweze kuchukua hatua za kisheria. Aidha Unapoona taarifa yoyote ama jambo la DART linalohitaji ufafanuzi tafadhali tembelea Ofisi za Wakala Ubungo Maji Dar es Salaam kwa ufafanuzi zaidi. pia tumia namba zetu za huduma kwa wateja ambazo ni za bure 0800110147 ili kupata ufafanuzi zaidi .# DART usafiri wa umma Nadhifu.
 
Samahani ningependa kuuliza Mfumo wa usafishaji wa Mabasi ya BRT ukoje maana unakutana na mabasi mjini machafu especially katikati kwenda chini vumbi , moshi mtupu!Dunia ya leo mbona kuna system nyingi tu za kisasa na huchukua muda mfupi tu sana basi linakuwa safi?! Asante!
 
Hivi haiwezekani kuweka njia za chini kutoka kwenye vituo vyenu mpaka nje ya barabara sababu hii kukatiza barabara ndio ufuate kituo imekaa weird.
 
Utaratibu ni kwamba Mabasi yanatakiwa kuwa masafi kabla hayajaanza kutoa huduma asubuhi, aidha wakati wa mchana kwenye kubadilishana shift pia usafi hufanyika na Mabasi yanatakiwa kuwa masafi wakati wote, jukumu hili liko kwa mtoa huduma wetu kampuni ya UDART, tunaendelea kumsimamia kwa karibu kuhakikisha anawajibika kutunza usafi wa Mabasi wakati wote.
 
Hivi haiwezekani kuweka njia za chini kutoka kwenye vituo vyenu mpaka nje ya barabara sababu hii kukatiza barabara ndio ufuate kituo imekaa weird.
Njia za chini zina changamoto zake lakini kwa hapa kwetu tumejaribu kuweka madaraja ya juu ya waenda kwa miguu ili kuwavusha abiria kutoka katika vituo vyetu kwenda nje ya barabara, changamoto ni kwa baadhi ya abiria wanaona tabu kupanda ngazi kutumia madaraja hayo kwa ajili ya kuvukia na badala yake wanaamua kupenya hata kwenye uzio uliowekwa jambo ambalo ni hatari kwa usalama. Tuendelee kuelimishana juu ya umuhimu wa kutumia madaraja ya juu pamoja na vivuko vya waenda kwa miguu ili kuepukana na ajali za mara kwa mara.
 
Katika Msimu huu wa maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba, Jumanne tarehe 27/6/2023 DART itazindua huduma ya usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka kutoka Kituo Kikuu cha Gerezani hadi Mbagala, huduma hiyo itadumu hadi tarehe 14 Julai 2023 baada ya kumalizika kwa maonesho ya sabasaba.

Huduma itaanza saa 12.00 Asubuhi hadi saa 3.00 Usiku, vituo vya Kati vitakavyotumika kushusha na kupakia abiria ni (1) Sabasaba (2)Mbagala Mission (3) Zakhem (4) Mbagala Rangitatu.

Nauli ni Tsh 750. Mtu Mzima na Tsh.200 Mwanafunzi. Ikumbukwe kuwa huduma hii ni kwa kipindi cha kunzia tarehe 27/6/2023 hadi tarehe 14/7/2023 tu, baada ya hapo huduma itasitishwa ili kumpisha mkandarasi aendelee kumalizia baadhi ya kazi ambazo hazijakamilika.
 
Sawa
 
Je kuna sheria gani sasa mtu anakuja kituoni asb saa 12 asb anajitangaza ni muhubiri na kukusanya sadaka eti kwenda kueneza neno la Mungu? Saa 3 anaondoka kwenda kupata supu na sadaka alizochukuwa wa wasafiri Udart na ina kuwa ni mazoea je hii sera iko kifungu gani? Udart ondoeni huu upumbavu inakera abiria wenu
 
Kuna taarifa za uongo na uzushi zinasambaa kwenye baadhi ya kurasa za mitandao ya kijamii kwamba moja ya Basi la Mwendokasi lilisababisha ajali jana tarehe 14/6/2023 na kuua mama mjamzito eneo la Kariakoo, taarifa hizo ni zaa uzushi, uongo na uzandiki zenye lengo ovu la kuchafua Wakala na Serikali kwa ujumla , tunaendelea kufuatilia chanzo cha taarifa hizo ili tuweze kuchukua hatua za kisheria. Aidha Unapoona taarifa yoyote ama jambo la DART linalohitaji ufafanuzi tafadhali tembelea Ofisi za Wakala Ubungo Maji Dar es Salaam kwa ufafanuzi zaidi. pia tumia namba zetu za huduma kwa wateja ambazo ni za bure 0800110147 ili kupata ufafanuzi zaidi .# DART usafiri wa umma Nadhifu.
Msikimbilie kujitetea, kweli kariakoo msimbazi ni tatizo kubwa Kwa watumiaji WA miondombinu na uwepo WA biashara, kama haijatokea mjue ipo njiani, vurugu ni nyingi, nawaomba muwasiliane na mamlaka nyingine ifanyike law and order ili matumizi ya miumdombinu iwe kama ilivyosanifiwa
 
View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.

Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku

Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: info@dart.go.tz.

#usafiri wa umma nadhifu

#mwendokasi app
Ondokeni muwawachie Dubai Public Transport, watuwekee mabasi ya umeme na waendeshe wao hilo shirika.

Nyinyi ni wezi watupu mmejazana hapo.

Tazameni mambo ya kisasa haya:

1688244450729.png
 
Pia Kuna hii miundombinu inayojengwa eneo la uwanja WA karume machinga complex, Kuna daraja la juu mmekwepa Kwa kuhatarisha watumiaji WA Magari Wakati WA matumizi, ila Cha kusikitisha zaidi Kuna sehemu mmeshindwa kuweka njia ya waenda Kwa miguu kutokana na uwanja WA karume, mmeshindwa nini kuwasiliana na wahusika WA uwanja na ukuta ukavunjwa na kupata njia iliyo sawa ili kuepusha ajali!? Fikiria kama Mtu ni mlemavu WA baiskeli atapitaje pale!? Ataingia barabara kubwa ndio arudi Kwa waenda Kwa miguu!? Nimeangalia ndani ya uwanja eneo hili Kwa ndani zimejaa taka TU, Wasimamizi na Tanroads watumie Weledi kidogo, fanyeni mazungumzo tunajenga nyumba Moja, ni Bora ikawa salama
 
Je kuna sheria gani sasa mtu anakuja kituoni asb saa 12 asb anajitangaza ni muhubiri na kukusanya sadaka eti kwenda kueneza neno la Mungu? Saa 3 anaondoka kwenda kupata supu na sadaka alizochukuwa wa wasafiri Udart na ina kuwa ni mazoea je hii sera iko kifungu gani? Udart ondoeni huu upumbavu inakera abiria wenu
kuna watu bado mnachanganya kati ya DART na UDART ni vitu viwili tofauti ila vyote vinafanya kazi katika BRT
 
Hii route ya Gerezani to Mbagala, muiache indelee hata baada ya 77, inatuheshimisha
 
Asante kwa kuja.
Ni lini hayo mabasi mtayapeleka Mwanza pia ili wananchi wapate huduma ya usafiri..??
Sababu jiji la Mwanza limekua na tayari limechangamka na mkituletea hizo Bus zikaanzia route ya Kisesa, Igoma, Neshno, Buzuruga, Mabatini, Nata, Pepsi, Mkuyuni, Nyegezi, Buhongwa, Nyashishi hadi Usagara and Return.
Mwanza anzisheni yenu. Unaiona frsa mbele yako unataka wengine waje kuanzsha, wewe poyoyo kweli kweli.

Unafahamu kuwa daladala zilianzia Mwanza? zilikuwa zinaitwa wahiwahi. Ndiyo zikashika Tanzania nzima. Hat bodaboda zilianza kwa Baiskeli mwanza. Wasukuma kwa Baskeli nimewavulia kpofia.

Hili ni shirika lililopo Dar tu.
 
Wasitufanyie kama TTCL walivyo tuachia vumbi hapa ndani
Hawa watu hawawezi kitu. Hili shirika wapewe Dubai Oublic Transpot, muone kazi zinafanywaje.

Watanzania ni wezi, wavivu, wazembe, hawajuwi maana ya huduma kwa jamii ni nini. Au wapewe wanaotoa huduma London, Au Toronto.

Toronto sijawahi kusubiri basi zaidi ya dakika tano.

Dubai sasa hivi wameweka mpaka ""detector za kikwapa", ukiwa una kikwapa mlango wa basi haufunguki, unaoneshwa bafu ziko wapi na dawa za kuzuia kikwapa ziko wapi. Ni uchafuzi mkubwa wa mazingira na hatari kwa usalama wa abiria wengine.

Tanzania unakuta mtu ananuka kikwapa mpaka kinapalia, basi linakuwa na harufukuliko banda la nguruwe. Basi linatakiwa linuke upya wakati wote.
 
Faiza una ujinga aisee. Nimecheka sana rafiki yangu.

Bahati yako huwa unajifunika kigume gume. Vinginevyo usingewahi kwa harufu ya jasho lako.

Njoo nikutibu Mkuu.
 
Back
Top Bottom