DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Hawa watu hawawezi kitu. Hili shirika wapewe Dubai Oublic Transpot, muone kazi zinafanywaje.

Watanzania ni wezi, wavivu, wazembe, hawajuwi maana ya huduma kwa jamii ni nini. Au wapewe wanaotoa huduma London, Au Toronto.

Toronto sijawahi kusubiri basi zaidi ya dakika tano.

Dubai sasa hivi wameweka mpaka ""detector za kikwapa", ukiwa una kikwapa mlango wa basi haufunguki, unaoneshwa bafu ziko wapi na dawa za kuzuia kikwapa ziko wapi. Ni uchafuzi mkubwa wa mazingira na hatari kwa usalama wa abiria wengine.

Tanzania unakuta mtu ananuka kikwapa mpaka kinapalia, basi linakuwa na harufukuliko banda la nguruwe. Basi linatakiwa linuke upya wakati wote.
Acha kutusem San we jamaa kapande Ubba au bolt Acha ubahiri I [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Acha kutusem San we jamaa kapande Ubba au bolt Acha ubahiri I [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
Public transport ikiendeshwa sawa ni nzuri kuliko uber nna bolt.

Hivyo vingine ni vya dharura tu. Matanzania wengi hawawezi ku afford uber na bolt.

Tuwe na reality.
 
Hivi hii njia ya mbagala ndiyo itaendelea au mtasitisha safari hiyo tarehe 13 July?
 
Ni kweli mnahitahiji maoni tatizo ktk kutia huduma zenu hamjali muda, ninyi mnajali kukusanya fedha lakini sio ubora WA huduma,unakuta watu wengi stendi lakini Hari zinapita tu, ule ukasi mliouanza nao hamnao siku hizi, toka Ferri hadi Kumara DK.30 lakini sasahivi SAA nzima
 
Maoni yangu ni haya pichani.
1.Morocco ni sehem ya kupumzikia madereva wakija wanalalamika hamuwapi muda wa kupumzika.so kama hapo watu tumejaa na gari zimepaki madereva wapo chini wanachati wengine wamekaa vyumbani.
2.Askari wa kusimamia usalama na foleni wapo bussy na mambo yao tu
20230711_193849.jpg
 
Maoni yangu ni haya pichani.
1.Morocco ni sehem ya kupumzikia madereva wakija wanalalamika hamuwapi muda wa kupumzika.so kama hapo watu tumejaa na gari zimepaki madereva wapo chini wanachati wengine wamekaa vyumbani.
2.Askari wa kusimamia usalama na foleni wapo bussy na mambo yao tuView attachment 2688962
Asante kwa maoni yako tunaomba jina lako na namba ya simu iili utupe maelezo kamili msaada wako ni muhimu katika utekelezaji 😋
 
Kwann mna paki gari na mnaona folen ni kubwa vituoni?
 
Tunakamilisha mfumo wa ITS (inteligent transport system) ambao utasaidia sana katika upangaji wa route na ugawaji wa mabasi kulingana na mahitaji ya kituo husika, kwa sasa mambo mengi yanafanyika manually ndio maana wakati mwingine changamoto zinakuwepo.
Ni nyinyi wenyewe ndio mlaumiwe kwa hilo. Kadi za Electronic zilishakuwepo mkaona mtoe muweke watu wakate kwa mikono
 
KUMRADHI:

Leo asubuhi kuanzia majira ya saa moja na robo kumetokea hitilafu ya umeme katika kituo chetu kikuu cha Kimara jambo ambalo limesababisha huduma ya kukata tiketi kuzorota kwa muda, aidha backup system yetu pia ilipata changamoto kutokana na kuzidiwa na kazi, kwa sasa umeme umerejea na huduma inaendelea kutolewa kama kawaida, tunashukuru kwa wale wote waliopaza sauti kuhakikisha huduma inarejea kama kawaida. Tunawaomba radhi abiria wetu na wale wote waliokumbwa na kadhia hii.
# DART Usafiri wa umma nadhifu.
 
Gari za Mloganzila zinaporudi Kimara elekezeni zipitie Kibamba Njiapanda, maana kunakuwa na abiria wengi halafu gari za Kibaha zikipita hazisimami sababu zinakuwa zimejaa abiria. Gari la Mloganzila linaporudi Kimara linakuwa na abiria wachache, hivyo linaenda na siti tupu huku kituo cha nyuma (Kibamba Njiapanda) kuna msululu wa abiria.
 
Tunashukuru kwa maoini na ushauri wako,tunaliangalia suala hili kwa ukaribu kuona namna bora ya kulishughulikia.
 
Lisaa la tatu mtu unasubiri gari hapa gerezani... yaani kufupi mwendokasi ni ukishapanda ila kwa muda unaosubiri hadi kupanda ni bora uchukue daladala tu... Gaddemit
 
Tafadhali sana rudisheni mfumo wa kuscan na ikiwezekana mlete kadi za DART kama wanavyofanya kwenye kivuko. Hii itazuia sana upotevu wa fedha na usimamizi mzuri wa huduma.
Mfumo wa kadi unakamilishwa hivi karibuni kwa sasa kadi zimekamilika tunasubiri mageti ya kuingilia vituoni ili tufanye configuration na kuanza kutoa kadi hizo kwa wateja wetu , ni suala la muda tu huduma hii itakuwa nzuri sana kuliko unavyofikiria. Serikali sikivu ya Mh. Samia Suluhu Hassan iko kazini yajayo yanafurahisha. Aidha suala la uchache wa Mabasi nalo limeshapatiwa mwarobaini wake stay tuned.
 
Back
Top Bottom