DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Wafanyakazi wenu hawawajali abiria kabila. Mfano mzuri ni mkaguzi wa tiketi wakati wa kuongia kwenye mabasi aliyeko kituo cha hospitali ya Muhimbili Upanga. Ni mwanamme wa makamo lakini ananyanyasa na kuwafokea hovyo abiria ambao baadhi ni wagonjwa. Anachafua taswira ya UDART
Pole sana kwa kadhia iliyokukuta wakati mwingine piga simu ya huduma kwa wateja bur 0800110147 ili hatua zichukuliwe kwa haraka, aidha usisahau kutaja muda na mahali ambapo tatizo husika limetokea.
 
Tatizo h ili lilitukumba Jana jumatano tarehe 22 Novemba saa moja jioni. Huyo mfanyakazi anafahamika has a kwa abiria wa Muhimbili kwenda Mbezi
 
Pole sana kwa kadhia iliyokukuta wakati mwingine piga simu ya huduma kwa wateja bur 0800110147 ili hatua zichukuliwe kwa haraka, aidha usisahau kutaja muda na mahali ambapo tatizo husika limetokea.
Chalamila aliwapa siku 14 mmalize shida za Mwendokasi. Mbona ndio mmeongeza matatizo?
Na route ya Mbagala inaanza lini?
 
Aongezwe mwekezaji mwingine wa mwendokasi wawe wawili kuleta ushindani. DART kaelemewa. unaweza kukaa kituoni masaa matatu unasubiri gari ukiwa umesimama kwenye mstari wa foleni.
 
Aongezwe mwekezaji mwingine wa mwendokasi wawe wawili kuleta ushindani. DART kaelemewa. unaweza kukaa kituoni masaa matatu unasubiri gari ukiwa umesimama kwenye mstari wa foleni.
sema udart kalemewa sio dart, dart hana mabasi na wala hamiliki mabasi
 
Hapa Mbezi ni kituo cha maombezi. Mmefell big time!! Chalamila zile siku 14 zilikuwa show off? Usafiri Mbezi hovyo kabisa!!
 
View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.

Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku

Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, (X)TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: info@dart.go.tz.

#usafiri wa umma nadhifu

#mwendokasi app
Mmeshaufata ushauri upi kati ya maoni mliyopewa hapa?
 
Sioni umuhimu wa nyie kuwepo hapa Jamii forum! Hovyo kabisa usafiri wenu!!
 
Uchache wa Mabasi ndio unasababisha adha hii ,lakini maelekezo ya serikali ni kutafuta mtoa huduma mwingine ambaye atashindana na huyu wa sasa ili kuboresha huduma, maelekezo hayo yanafanyiwa kazi na baada ya muda mfupi mtaona matokeo.

Mkuu yale mabasi kipindi mradi unazinguliwa yalienda wapi hadi kusababisha upungufu huu uliopo?
 
Hapa Mbezi ni kituo cha maombezi. Mmefell big time!! Chalamila zile siku 14 zilikuwa show off? Usafiri Mbezi hovyo kabisa!!

[emoji28][emoji28] kutokana na kero ya kusafiri abiria kupanga foleni muda mrefu wajasiria injili wamegeuza kanisa na ombaomba wamegeuza baggers street.
 
Uchache wa Mabasi ndio unasababisha adha hii ,lakini maelekezo ya serikali ni kutafuta mtoa huduma mwingine ambaye atashindana na huyu wa sasa ili kuboresha huduma, maelekezo hayo yanafanyiwa kazi na baada ya muda mfupi mtaona matokeo.
Nyie dart kazi yenu nini?
 
Back
Top Bottom