DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Ingieni makubaliano na gari binafsi ili wasaidie kusafirisha watu, kwa hali ilivyo sasa huu usafiri ni mateso makubwa sana.
 
View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.

Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku

Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, (X)TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: info@dart.go.tz.

#usafiri wa umma nadhifu

#mwendokasi app

Binafsisheni mradi
 
BASI LA MWENDOKASI (KIMARA _KIVUKONI) LAPITA NA ABIRIA WA KOROGWE HADI KIBAHA

Leo 30/11/2023 basi la mwendokasi limeenda na abiria waliopanda korogwe ili wageuze na basi kutokana na changamoto ya mabasi asubuhi ya leo!
Mabasi yalikuwa yanatoka kimara mwisho yakiwa yamejaa hivyo abiria kusubiri kituoni kwa muda mrefu!!
Basi lilipo fika kimara mwisho licha ya wingi wa abiria kituoni, supervisor aliwataka abiria kushuka na kukata tiketi upya ili waweze kuendelea na safari!
Wengine walioweza kukata tiketi walishuka pamoja na wanafunzi walio kuwa na mitihani iliwabidi wawahi shule!
Wengine tuliobakia tulihitaji kufaulishwa basi jingine bila tiketi mpya au la basi liendelee na safari!
Supervisor akabadili basi route kwenda KIBAHA
Abiria tuliopandia korogwe tukachanganywa na wa KIBAHA !
Njiani tuliomba msaada kwa traffic akampa maelekezo dereva wa basi kuwa akifika mbezi Luis aingie ili supervisor wa mbezi atufaulishe basi la mjini, lakini tulivyo fika mbezi Luis dereva alikaidi hakuingia, akapitiliza!!
Tumefika KIBAHA tukatakiwa tena kukata tiketi ya kurudi mjini kama ilivyo awali na ustaarabu wetu tukamuita askari ili kutatua mzozo, haikuwa rahisi mpaka alivyo kuja kiongozi wa LATRA mkoa wa Pwani kuja kutatua mzozo!!
Ni kweli tumefika makazini kwa kuchelewa (kucheleweshwa) lakini tulikuwa tunasimama kwenye haki, unaweza vipi kukaa dk45 kituoni kusubiri mwendokasi, na magari yanakuja hayasimami???
Wasimamizi walishindwa nini kutoa taarifa kuwa kituo cha korogwe kimejaa watu zije gari tupu kuondoka kadhia???
Supervisor aliona hasara gani sisi abiria wa KOROGWE kupandia basi kimara mwisho??
Ukweli hakuna asiye jua changamoto iliyopo sasa kwenye mwendokasi, lakini hakuna anaye taka kutatua!
Pamoja na uchache wa mabasi kwa sasa lakini bado asubuhi unakuta mabasi yame_paki na abiria wanapata shida!!
Tunalazimika kupanda mwendokasi kwasababu daradara ziliondolewa kwenye route ya mwendokasi, sasa kama mzigo umekuwa mkubwa waruhusu daradara kama awali!
 
Oktoba hii tunakabidhiwa miundombinu ikiwa imekamilika kabisa, baada ya hapo utasikia kutoka kwetu kuwa ni lini tutaanza huduma endelea kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii ikiwemo JF.
Pale kigogo sambusa hapasomeki mpaka kesho
 
View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.

Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku

Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, (X)TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: info@dart.go.tz.

#usafiri wa umma nadhifu

#mwendokasi app
Mabasi ni machache,watu wa nakaa vituoni zaidi ya Masaa ma3 Mabasi mengi mabovu, wahudumu wanaochana tiketi wakati mwingine hawazichani zinarudi kuuzwa tena, wakata tiketi kubaki na 50 50 za abiria kisingizio hawana change . Kiufupi huduma ni mbovu kwa 80% Bora daladala za Mbezi posta na mbezi Kariakoo via Morogoro road ziruhusiwe kuweka ushindani
 
Takukuru wachunguzeni wakata tiketi wa dart, wanakula RUSHWA.. potelea pote, siwezi kutoa elfu tano useme huna chenchi huo ni wizi
 
Mabasi ni machache,watu wa nakaa vituoni zaidi ya Masaa ma3 Mabasi mengi mabovu, wahudumu wanaochana tiketi wakati mwingine hawazichani zinarudi kuuzwa tena, wakata tiketi kubaki na 50 50 za abiria kisingizio hawana change . Kiufupi huduma ni mbovu kwa 80% Bora daladala za Mbezi posta na mbezi Kariakoo via Morogoro road ziruhusiwe kuweka ushindani

Marathon day umechambua vizuri sana.
 
J3 asubuhi hali ya Korogwe inatisha sana mradi ni mzuri sema umezidiwa na population mnaitaji msaada ASAP...!
 
Habari viongozi
Nashauri mtafute njia mbadala ya kuwasaidia abiria wa vituo hivi vya katikati kama bucha baruti kona na baruti maana unakuta mtu anakaa kituoni masaa mawili hadi aanamua kutoka kwenda kutafuta njia nyingine na nauli hairudi hili mliangalie

Kingine cha kusikitisha magari sasa yamekuwa kama mashindano kisa ni express/ordinary na unakuta gari halijajaa ,dereva anaona abiria wamejaa kituoni anapita bila kujali najiuliza huyu dereva anahisi ni nani anapaswa kuwasafirisha hawa abiria

Lingine hata kama huu mradi ni wa serikali tujaribu kuhisi ni wa mtu binafsi ,wewe mfanyakazi chukulia kwamba mradi ni wako ,magari ni yako kwahiyo abiria ni wako ili uvae viatu vyao ili uone umuhimu wa kuwasaidia

Abiria wa vituo hivi wanapata tabu sana ,tukumbuke hawa abiria wa vituo hivi wanaenda maeneo mbalimbali kama hawa wa kimara mwisho na mbezi mwisho wanaopata huduma non stop ,tukifika mbele tunaacha mwendo kasi tunapanda usafiri mwingine sasa hebu fikiri unaponiweka kituoni masaa mawili itakuwaje

Zamani tulikuwa tunaamka saa 10 usiku kwenda kariakoo tukasema alhamdullillah mwendo kasi imetuokoa lakini nahisi sasa tunarudi kulekule

Ushauri
Nauli ya kimara mwisho hadi kwingineko kariakoo au kivukoni ni 750/= lakini hata kutoka kwenye hivyo vituo nauli ni ileile ,basi zikitoka gari 5 ,angalau mbili zianzie kwenye vituo vya kati ,wala hamtapata hasara nauli ni ileile
 
Mimi nasikitika kuwa magari yenu hayatoshi kusafirisha abiria mnachokifanya ni kutunyima haki ya kusafiri bila bugdha. Kwanini hamkufanya research kabla hamjazuia wenye daladala ili mfanye kwa ushindani?
 
Kulikuwa na pendekezo la kujumuisha sekta binafsi kwa kualika wadau wa usafirishaji kkama wamiliki wa daladala na wamiliki wa mabasi ya mikoani. Wigo ukipannuliwa mtapata mtaji na mbinu za uendeshaji.
Kama watu wana uwezo wa kununua basi 50 mtu 1 wakiungana si mtafurahi?

Acheni ubinafsi..wananchi wanataka huduma nzuri na za uhakika
 
Huduma mbovu kabisa, kimara mtu anasimama foleni Masaa matatu, wakatisha ticket hawachani tickets zinatumika zaidi ya mara moja. mabasi machache walinzi kutokusimalia msururu ya foleni. kiufupi huduma ni mbovu kwa 100%
 
Ni Nani aliewashauri kwenda kuweka ofisi yenu kwa makazi ya chura. Maana mvua ikipiga pale si majengo Wala si magari Huwa yanageuka vyombo vya majini badala ya nchi kavu
 
View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.

Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku

Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, (X)TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: info@dart.go.tz.

#usafiri wa umma nadhifu

#mwendokasi app
Vituo vya katikati kuanzia maeneo ya Bucha , Baruti hadi Kibo abilia wanapata taabu sana. mabasi yakitoka huko yanakoanzia yanakuwa yamejaa sana. nashauri baada ya dakika zisizozidi 15 gari angalau 1 tu ianzie Bucha ili kusaidia abiria wa hivyo vituo kuwahi makazini.
 
Hawana mabasi, hao abiria wa kimara tu wanakaa mistari masaa matatu na bus likija ni kupigana vikumbo, suluhisho waruhusu mabasi ya daladala ya mbezi posta na mbezi kariakoo via morogoro road hiyo ndio suluhisho, kazi imewashinda. Waruhusu daladala waone nani atang'ang'ania kusubiri hayo mabasi yao. Tunajuta sana kuondolewa daladala zetu pendwa na kutuletea haya matatizo
 
Back
Top Bottom