DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

DART nyie ni kansa na nimaandui wa maendeleo, hamuwezi kuwaweka watu lisaa na nusu kituoni wanasubiri mwendoka, yaani hata ukisema upande ukageuke nalo, napo workdone equals to zero.
 
Mabasi sio ya mwendo kasi tena hayo. Hayo muyaite magari yanayopita kwenye njia maalum
 
NJIA ya Mbagala itaanza kutumika oni kwa mabasi ya mwendo Kasi kwani imekuwa ni matamko tu ya wanasiasa ya CHAMA tawala pasipo utekelezaji
 
View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.

Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku

Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, (X)TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: info@dart.go.tz.

#usafiri wa umma nadhifu

#mwendokasi app
Punguzeni bei ya card
 
Acheni kutukalisha vituoni kama midoli yenu yani saiv vituo vimegeuka vijiwe vya simba na yanga asee so sad magari hamna watu wanpiga story lisaa lizima bado tu kuuzwe kahawa kabisa
 
Nyie jamaa naona ruti ya Mbezi_Posta inawalipa zaidi kiasi cha kutuletea dharau watu wa Kimara. Haiingii akilini watu wa Kimara tumeganda vituoni masaa mawili, basi zimepita mbili huku zaidi ya basi tano za Mbezi na nne za Morocco zikipita kupakiza abiria.

Hii ni dharau mnatuletea watu wa Kimara huku mkijisahaulisha mfumo rasmi wa njia za huo usafiri wenu unaishia Kimara na hiyo ruti ya Mbezi ni nyongeza tu. Na bado watu wa Mbezi wanayo option ya kupata magari ya kuunganisha kwenda Mbezi ikiwa wameshukia Kimara. Yaani abiria anapanda Basi ya Mbezi Posta ya Zamani mpaka anafika Mbezi, abiria wa Kimara bado ameganda Kituoni. Huu ni ufala mnatuletea huku mkiendelea kupima ustahimilivu wetu. Acheni ungese nyie mbwa.
 
Taarifa kwa Umma.
 

Attachments

  • F9BD7EAE-5733-4FC2-A535-6140E77BB26E.png
    F9BD7EAE-5733-4FC2-A535-6140E77BB26E.png
    1.1 MB · Views: 1
Hebu tupeni taarifa kamili na yauhakika! Ruti ya mbagala kwa mabasi ya mwendokasi itaanza lini?! Maana tangu jpm yuko hai alisema atazindua 2021 lakini tangu samia ameingia mpaka leo 2025 mabasi ya mwendokasi mbagala imekuwa ni mfupa mgumu uliomshinda fisi...?!

Imefikia wakati mpaka miundombinu yake imeanza kuharibika kabla hata ya kuanza kutumika! So sad indeed...!!

Au ndio mnataka kuja kuzindua mwaka wa uchaguzi mkuu kwaajili ya kampeni za uraisi...?!
 
Back
Top Bottom