David Kafulila: Hakuna siku Serikali itaacha kukopa kwani hata Marekani na China nao wanakopa zaidi ya Tanzania

David Kafulila: Hakuna siku Serikali itaacha kukopa kwani hata Marekani na China nao wanakopa zaidi ya Tanzania

Kama kawaida ya Kafulila uzi unaaznishwa na ID anazozilipa nyingine zinakuja kutoa comment na hata hapa naona amekuja na ID yake kujibu.

Anafikiri humu wote ni wajinga kama yeye.
 
===
Akiongea katika Kipindi cha DAKIKA 45 kinachorushwa "LIVE" na kituo cha runinga cha ITV Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi PPPC David Kafulila alikuwa na haya ya kuwaambia Watanzania,

Akifafanua kuhusu Tanzania kuendelea kukopa na kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo alisema "Kiuchumi na Kibiashara huwezi kukopeshwa kama huna uwezo wa kukopesheka ili mtu au taasisi akopesheke kwa masharti mazuri Lazima awe vizuri Kiuchumi hili ni Sayansi ipo kuanzia ngazi ya familia mpaka Ile ya Taifa" alisema Bwana David Kafulila.

Tanzania imepimwa kwa vigezo vyote ukianzia na na vile vya World Bank, IMF na hata taasisi za credit rating kama Moody's na Fitch wote wanasema Tanzania deni lake ni himilivu na stahimilivu ndio maana hakuna siku Serikali itaacha kukopa hata Marekani, China, Urusi wote hawa wanakopa alisisitiza Kafulila.

China Taifa lenye dhahabu nyingi kuliko Taifa lolote Dunia inakopa, Urusu yenye gesi nyingi duniani nayo inakopa tatizo sio kukopa labda tatizo liwe unakopa kwaajili ya kufanya nini ila kukopa ili kujenga miradi ya Maendeleo ndio haswa tunapashwa kuendelea kukopa- alisema David Kafulila Mkurugenzi Mtendaji wa PPPC-Tanzania.

Sasa msikilize mpaka mwisho.



View attachment 3224599


===
Ukiona mtu kaalikwa kwenye mdahalo Alafu anajifananisha nchi yake na marekani ujue hana AKILI.ni chawa tu huyo.Na huyu kafulila alikuwa na Akili huko nyuma siku hizi anatembea kichwa chini miguu juu.
 
Kafulila , Hivi ni kiongozi yupi alimuita Tumbili, kipindi kile wakuu,? na alifikilia nini kutumia jina la mnyama uyu?

Maana Tumbili huwa na vituko sana, ana weza kubanwa na chatu akawa anapiga kelele huku anafanya vituko
 
Hivi watu wanajua the mechanics of How the likes USA operates ?!! Au wanajisemea tu kama Mapunguani ?



Mkuu hebu dadavua vizuri naona kama unahoja ya maana sana
 
Kafulila , Hivi ni kiongozi yupi alimuita Tumbili, kipindi kile wakuu,? na alifikilia nini kutumia jina la mnyama uyu?

Maana Tumbili huwa na vituko sana, ana weza kubanwa na chatu akawa anapiga kelele huku anafanya vituko
Wewe Jenga hoja acha maneno
 
Tuna kopa kwa sababu Marekani na China wanakopa au tuna kopa kwa sababu tuna ulazima wa kukopa?
 
Back
Top Bottom