Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukiona mtu kaalikwa kwenye mdahalo Alafu anajifananisha nchi yake na marekani ujue hana AKILI.ni chawa tu huyo.Na huyu kafulila alikuwa na Akili huko nyuma siku hizi anatembea kichwa chini miguu juu.===
Akiongea katika Kipindi cha DAKIKA 45 kinachorushwa "LIVE" na kituo cha runinga cha ITV Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi PPPC David Kafulila alikuwa na haya ya kuwaambia Watanzania,
Akifafanua kuhusu Tanzania kuendelea kukopa na kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo alisema "Kiuchumi na Kibiashara huwezi kukopeshwa kama huna uwezo wa kukopesheka ili mtu au taasisi akopesheke kwa masharti mazuri Lazima awe vizuri Kiuchumi hili ni Sayansi ipo kuanzia ngazi ya familia mpaka Ile ya Taifa" alisema Bwana David Kafulila.
Tanzania imepimwa kwa vigezo vyote ukianzia na na vile vya World Bank, IMF na hata taasisi za credit rating kama Moody's na Fitch wote wanasema Tanzania deni lake ni himilivu na stahimilivu ndio maana hakuna siku Serikali itaacha kukopa hata Marekani, China, Urusi wote hawa wanakopa alisisitiza Kafulila.
China Taifa lenye dhahabu nyingi kuliko Taifa lolote Dunia inakopa, Urusu yenye gesi nyingi duniani nayo inakopa tatizo sio kukopa labda tatizo liwe unakopa kwaajili ya kufanya nini ila kukopa ili kujenga miradi ya Maendeleo ndio haswa tunapashwa kuendelea kukopa- alisema David Kafulila Mkurugenzi Mtendaji wa PPPC-Tanzania.
Sasa msikilize mpaka mwisho.
View attachment 3224599
===
We jamaa una akili sana.Kwenye kukopa wanashindana na marekani na china ila kwenye maendeleo ukiwauliza utajikuta umetekwa 🤣🤣
Mkuu hebu dadavua vizuri naona kama unahoja ya maana sanaHivi watu wanajua the mechanics of How the likes USA operates ?!! Au wanajisemea tu kama Mapunguani ?
Majibu ya hata Ulaya; USA wanafanya ni kupotoka (Statistics are like bikinis. What they reveal is suggestive, but what they conceal is vital.')
Tuliambiwa hata United Kingdom Bandari wamewapa watu.., ni kweli UK hata uzalishaji siku hizi hawafanyi kama zamani magari yao yote ni mali za wengine..., UK baada ya ukoloni kuisha ilijikita kwenye Service industry (pamoja na kuuzia watu silaha); ila muhimu kabisa walijikita kwenye Service ya...www.jamiiforums.com
Mfumo wa USA Dollar ulivyoanza kutumika Duniani, na Kupelekea Dunia Kuchezeshwa DECI (Ponzi Scheme)
Utangulizi: Baada ya vita vya Pili vya dunia mataifa mengi ya Ulaya yalikuwa katika hali mbaya ya Uchumi, Wawakilishi wengi wa Mataifa haya ya Ulaya na dunia (Jumla Mataifa 44) walikutana Bretton Woods, mwaka 1944 kuangalia ni jinsi gani wanaweza kuwa na Uchumi bora na wa Uhakika, Mataifa haya...www.jamiiforums.com
Kwanini Serikali Ikope Kuendesha Miradi, Wakati inaweza Kutengeneza Pesa ?
Kabla hatujaitana vichaa, kwanza kabisa tukubaliane kwamba ndicho kinachotokea sasa hivi duniani (creating money from thin Air) ingawa ni Benki ndio zinafanya hivyo... Pesa inavyotengezwa na kuongezwa kwenye Mzunguko na Benki Wewe ukienda kuomba mkopo Benki unapewa pesa ambayo Benki haina wala...www.jamiiforums.com
Wewe Jenga hoja acha manenoKafulila , Hivi ni kiongozi yupi alimuita Tumbili, kipindi kile wakuu,? na alifikilia nini kutumia jina la mnyama uyu?
Maana Tumbili huwa na vituko sana, ana weza kubanwa na chatu akawa anapiga kelele huku anafanya vituko
Nimeuliza nipe jibu kwanza ndo nijenge hoja yangu, ebu muulize Mzee Mgaya kama kumbukumbu hunaWewe Jenga hoja acha maneno
Mzee Wassira na Kafulila ni watu makini sana toka Upinzani nakubaliana na weweKama Kuna watu Upinzani tulipoteza basi ni huyu Kafulila na Mzee Wassira
Umeuliza swali gani mkuu nikujibu?Nimeuliza nipe jibu kwanza ndo nijenge hoja yangu, ebu muulize Mzee Mgaya kama kumbukumbu huna
Umeambiwa wanakopa sio misaadaKafulila ana tatizo la afya ya akili, Marekani wanaomba misaada kama sisi?
Nimeuliza kipindi kile mkuu ni nani Bungeni alimuita Kafulila Tumbilili , na ni kwa nini alitumia mnyama Tumbili kumuita KafulilaUmeuliza swali gani mkuu nikujibu?
Ni Marehemu Werema aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wakati wa Mzee JakayaNimeuliza kipindi kile mkuu ni nani Bungeni alimuita Kafulila Tumbilili , na ni kwa nini alitumia mnyama Tumbili kumuita Kafulila
Nimekupata sana, Tumbili ni wanyama wenye makeke, mikwara ,kibao, ila akibanwa kwenye kumi na nane huwa anatia uzuni sanaNi Marehemu Werema aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wakati wa Mzee Jakaya
Sio tumbili ni wanyama woteNimekupata sana, Tumbili ni wanyama wenye makeke, mikwara ,kibao, ila akibanwa kwenye kumi na nane huwa anatia uzuni sana
Usawa wapi mbona kama jamaa anachapa kazi sanaHuyu tangu awe registered tumbili hajawahi kuwa sawa tena