Dawa gani ilikusaidia kwenye ugonjwa wa vidonda vya tumbo?

Hongera sana
 
Usiku wa kuamkia tarehe 17 Mwezi November mwaka jana niliugua maumivu makali ya tumbo.

Asubuhi nikajitosa moja kwa moja kwenda zahanati kupima.

Vipimo vikaja kama ifuatavyo

Kwa maelezo ya daktari ni kuwa nikisumbuliwa na magonjwa mawili. Vidonda vya tumbo na Typhoid.

Nilipata ukakasi kwenye Typhoid kwasababu circle yangu ya maisha nimekuwa mtu makini sana kwenye usalama wa vyakula na maji.

Nikaandikiwa dawa hapo kama shilingi 25K kwa ajili ya kutibu magonjwa yote mawili, lakini nikawajibu kuwa kwa saizi sina hela ngoja nikajipange.

Nilipotoka hapo nikachukua boda kwenda kwenye hospitali binafsi kwenda kupima tena kuhakiki.

Nilipofika pale nilichukuliwa vipimo vya damu na vipimo vilikuwa kama hivi.

Daktari akanipa ufafanuzi wa kinacho nisumbua akiniambia kuwa ni vidonda vya tumbo pekee, hakuna ugonjwa mwingine zaidi ya huo.

Dawa akaniandikia gharama zake kuwa ni 99,000 nikasema ngoja nikajipange.

Nikaongea na ndugu yangu akanipa ushauri wa dawa moja ambayo aliwahi kuitumia mke wake.

Dawa hiyo ilikuwa inajina linalofanana na "morpezoel"

Lakini mimi mwenyewe sikuacha kujiongeza. Nika Google nikakutana na link ya uzi wa mtu ambaye alitoa ushauri wa kutumia bamia kama dawa.

Bamia unaziloweka kwenye maji zinakaa kwenye maji kwa muda wa masaa 8 kisha unakunywa yale maji yake kwa kutwa mara mbili.

Kwa kufanya hivyo ndio nimejikuta nimepona vidonda vya tumbo.
 
Brother asante sana pia pole sana , ulitumia Kwa muda Gani? Ratiba ilikuaje asubuhi , mchana na jioni au? Ulikuwa unatumiaje na Kwa muda Gani?
 
Brother asante sana pia pole sana , ulitumia Kwa muda Gani? Ratiba ilikuaje asubuhi , mchana na jioni au? Ulikuwa unatumiaje na Kwa muda Gani?
Wiki Moja tu nilianza kuona changes

Asubuhi na jioni ndio ilikuwa dozi yake wakati huo ukiendelea kuepuka ulaji wa vyakula visivyo rafiki.

Lakini hayo yote yanaweza yasifanye kazi ikiwa wewe ni mtu wa stress muda mwingi.

Jitahidi kujichanganya na watu sehemu ambayo hautakuwa mpweke ili usiyape nafasi mawazo.
 
P
Mkuu usihangaike na hii kitu. Kuna jamaa yangu alinipa dawa free ikaniponya kabisa, naweza nikamuomba akusaidie na wewe.
Kama atakutoza haiwezi shilingi 5000. Nakutumia namba inbox.
ost namba zake
 
Kama bado vinasumbua nicheki inbobo
 
Kinachosababisha vidonda vya tumbo ni Helicobacter pylori na sio stress wala aina ya chakula unachotumia.

Ninauza dawa za uhakika kutibu kabisa vidonda vya tumbo na kiungulia chote kinaisha.

Ukitumia hizi dawa unapona kabisa na utaweza kula chakula chochote ukipendacho.

Hii ni biashara, anayetaka aje PM
 
Mkuu usihangaike na hii kitu. Kuna jamaa yangu alinipa dawa free ikaniponya kabisa, naweza nikamuomba akusaidie na wewe.
Kama atakutoza haiwezi shilingi 5000. Nakutumia namba inbox.

Mkuu Chivundu , nami nahitaji msaada wako kwenye hili la vidonda vya tumbo.
 
95% of my patients with PUD h pylori was negative
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…