Dawa gani ilikusaidia kwenye ugonjwa wa vidonda vya tumbo?

Dawa gani ilikusaidia kwenye ugonjwa wa vidonda vya tumbo?

Inbox kufanya nini? Unashindwa Vipi kupost hapa?

Ili iweje? Umezuiwa na Nani kushare hapa?

Shangaa wewe, miye ndio nashindwa kuwaelewa kabisa.
mimi sitibu na wala sina elimu yoyote ya utabibu chief
Ila kuna mtalaamu mmoja namfahamu alisaidia ndugu yangu kwa hiyo nimemwambia lee akiendelea kupata changamoto anione nimpe mawasiliano ya huyo mtaalamu huwenda akamsaidia
sioni kama ni busara kuweka mawasiliano ya mtaalamu hapa kwa kuwa sijamuomba kufanya hivyo chief
 
Aisee hivi vidude vinanitesa nimekunywa kila aina ya matakataka ya dawa za hospitalini na tiba mbadala lakini bado vinanisumbua, angalau kidogo dawa zinaitwa legal kit zinisaidia lakini zingine ni kama natupa hela na kutesa tumbo kwa madawa.

Na ni bora vingekuwa vinasumbua tumboni lakini mimi vinanitesa zaidi kwa maumivu ya vichomi mgongoni na kifuani upande wa moyo, yaani hata kukohoa kucheka au kutikisa mkono wa kushoto ni maumivu makali sana.
Mbona zipo na ni za kutumia mboga au matunda...
 
Wamasai dawa zao nzuri sana Ila sio hawa WA mjini sikuizi wanachakachua Hadi wao.. Inabidi uwatafute wale WA porini kabisa..
Nakumbuka Nilikuaga na ugonjwa WA ngozi nilisumbuka nao Sana mahospitali karibu miaka mitatu kama sio minne.. Kuna mmasai mmoja alikua mpangaji wetu aliniambia nikienda nyumbani nitakuletea dawa,, kweli alinitelea unga flani hivi nikawa nakunywa kila siku asubuhi na jioni ndani ya mwezi mmoja tu nilipona na makovu yote yalifutika, nimekua na ngozi nyororo kama ya mtoto mdogo.., na ninaitunza dawa ninayo Hadi Leo Hua nakunywaga mara chache chache isiishe[emoji3526][emoji3526]
Ngozi ilikuwa ina changamoto gani?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Mimi vilinisumbua Sana kiasi nikianza kupata maumivu, mpaka ninywe dawa ndio vinatulia. Nilishauriwa nipunguze mawazo, nile chakula kwa wakati yaani nisisikie njaa na pia nifanye mazoezi. Kwakweli mpaka Leo hii, vidonda vya tumbo nasikia Tu wengine wakilalamika lakini Mimi sina.
 
Ngozi ilikuwa ina changamoto gani?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Nilikua naota vipele vidogo vidogo nikikuna vinatoa maji halafu vinasambaa nakua kama nimeungua moto,, hospitali walikua wananiambia fungus.. .
Nilipewaga huo apo unga hua natumia kama majani ya chai, hadi leo ngozi yangu iko soft hadi miguuni mwanzo nilikua na madoa doa ila saizi yamefutika yote
 
Gastroscopy ni mpira mwembamba mrefu unaoingizwa kinywani, unashuka kupitia kooni mpaka tumboni. Huu mpira una lensi ndogo kwa mbele yenye taa. Mpira unapofika tumboni ile lensi inaonyesha kule ndani ya tumbo na utumbo mdogo kama kuna vidonda kwa kutumia screen iliyounganishwa na huo mpira. Unaambiwa usile chakula asubuhi kabla ya kwenda kwenye kipimo ili tumbo liwe wazi na lensi iweze kuonyesha. Pia kwa kutumia huo huo mpira wanaweza kuchukuwa maji maji (sample )kutoka kwenye tumbo ili kwenda kupima. Hiki ni kipimo cha uhakika zaidi kuliko kupima choo au kukisia kwa kutumia dalili anazosema mgonjwa. NB: kipimo kinafanyika bila kuwekewa nusu kaputi na hakina shida i.e. hujisikii vibaya kama unavyoweza kudhani kabla ya kufanyiwa.
Hicho kipimo kikigusa tumbo kuchukua hayo maji maji lazima uitikie Mjomba, ni balaa tupu japo ni kipimo sahihi kabisa

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Naona tatizo limekuwa kubwa hasa Bongo, Mimi sina dawa ya kuponya lakini kings ukitaka usiumwe vidonda vya tumbo kinga ipo.

Ukitaka usipatwe kabisa na vidonda vya tumbo tumia anti gas, na matunda yanayosaidia kuondowa gesi tumboni, hata ndizi mbivu ni nzuri haina citric acid, kwenye chai na maji tumia limao hii ni nzuri sana.

Kwa sasa Mimi natumia vidonge Anti ,acid huwa naletewa kutoka Marekani, ni vidonge viwili kila baada ya wiki mbili unaweza kuvimezea na maji au kuvimezea na bia, issue ya gas tumboni Marekani,walishamalizana nayo kitambo Tu.

Kama Una mtu Marekani akutumie Kwa wingi vidonge hivi upati vidonda vya tumbo kamwe.

Halafu muelewe kujamba ni ahuweni Kwa tumbo lako, mbaya wa tumbo ni gas.
Maziwa mtindi ni mbabe wa kutoa gesi tumboni, ukigonga glasi 1 au 2 asubuhi na jioni kila siku lazima ujambe vya kutosha na kutoa haja kubwa mara 2 kwa siku ambapo ndiyo utaratibu sahihi kiafya, ukishindwa sana juisi ya ukwaju nayo ni njema sana.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Nilikua naota vipele vidogo vidogo nikikuna vinatoa maji halafu vinasambaa nakua kama nimeungua moto,, hospitali walikua wananiambia fungus.. .
Nilipewaga huo apo unga hua natumia kama majani ya chai, hadi leo ngozi yangu iko soft hadi miguuni mwanzo nilikua na madoa doa ila saizi yamefutika yote
Huyo Mtu unamfahamu ili sote tushee naye matibabu? Maana kuna Mdogo wangu ana changamoto kama hiyo kitambo sana na bado hajapata tiba.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nilitumia mkaa wa magome ya mkaratusi kwa kuchanganya na asali ya nyuki wadogo nikapona kabisa.

Wapo pia walionidokeza kuwa mafuta ya ubuyu yanatibu though sikutumia.

Pole sana mkuu!
 
Pole mkuu mimi vilikuwa vinanipa homa ya kuanzia chini ya mgongo kuoanda juu kupima nikaambiwa ni vyenyewe nikamwmbia dk kuna dawa naijua acha nikatumie hiyo nitarudi nikatumia
Unga wa manjano mpya [huu nguvu inakuwa kubwa ] vijiko 8
Unga wa pilipil manga vijiko 2
Asali robo 250ml
Unamix huo unga kwanza vizuri alafu unaweka hiyo asali yote
Matumiz vijiko 3 kutwa mara 3
Dozi unatengeneza huo mchanganyiko kwa mara 2 tu dozi inakamilika
NB NILIPONA mpaka leo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niko na majani nayatumia saizi kutoka umasaini huko ndanindani naona walau yanafanya vizuri.. Ila hizi za hospitali nimehangaika sana bila mafanikio
Chukua na ndizi mbichi, zikate Mara 2- Kisha zianike juani.
👉Tumia katika chai isiyo na sukari ni 🔥🔥🔥.
👉Tafuta amoxicillin, tridamol na trinidazole uta kaa poa mno Interlacustrine R
 
Mkuu usihangaike na hii kitu. Kuna jamaa yangu alinipa dawa free ikaniponya kabisa, naweza nikamuomba akusaidie na wewe.
Kama atakutoza haiwezi shilingi 5000. Nakutumia namba inbox.
 
Back
Top Bottom