Dawa gani ilikusaidia kwenye ugonjwa wa vidonda vya tumbo?

Dawa gani ilikusaidia kwenye ugonjwa wa vidonda vya tumbo?

Ni sahihi kabisa milikuwa naumwa tambazi hadi meno n kichwa kuuma nikatafuta dawa sana baadae nikamwomba mlinzi mmasai anitafutie dawa aliitafuta akasema 80k nikasema kama nitapona nalipa na mzee muuza dawa yupo moro kijijini alisema utalipa ukipona wiki moja tu sijapata maumivu tena
Wana bei Sana dawa zao, lakini kupona uhakika
 
Tatizo watu hawapimi ili kujua ni aina gani ya vidonda mtu husika anavyo, ili kutumia dawa husika.

Mimi vikianza kuniwasha nakunywa hiyo Omeprazole na vinanyamaza hata mwaka mzima na Bia nakunywa freshi tu.
Kuna jamaa huko juu kasema tangu aanze kunywa bia amepona 😂😂
 
Tatizo watu hawapimi ili kujua ni aina gani ya vidonda mtu husika anavyo, ili kutumia dawa husika.

Mimi vikianza kuniwasha nakunywa hiyo Omeprazole na vinanyamaza hata mwaka mzima na Bia nakunywa freshi tu.
Sema vipimo kama ultrasound hakiwezi kutoa majibu ya aina gani au viko kwenye stage ipi,, ndiomana nataka nikapime na endoscopy ili nipate majibu sahihi zaidi
 
Aisee hivi vidude vinanitesa nimekunywa kila aina ya matakataka ya dawa za hospitalini na tiba mbadala lakini bado vinanisumbua, angalau kidogo dawa zinaitwa legal kit zinisaidia lakini zingine ni kama natupa hela na kutesa tumbo kwa madawa.

Na ni bora vingekuwa vinasumbua tumboni lakini mimi vinanitesa zaidi kwa maumivu ya vichomi mgongoni na kifuani upande wa moyo, yaani hata kukohoa kucheka au kutikisa mkono wa kushoto ni maumivu makali sana.
Pole sana. Nianze kukuuliza, unauhakika una vidonda vya tumbo? Ulifanyiwa vipimo vya aina gani au ni kwa nini unadhani kuwa una vidonda vya tumbo? Nauliza hivi kwa sababu Bongo ni watu wengi sana wanakunywa dawa kwa kitu kinachodaiwa kuwa ni vidonda vya tumbo lakini wengi unakuta hawana. Ningekushauri kwa uhakika zaidi jaribu kufanya gastroscopy uhakikishe.
 
Hawa wa mjini wanakuwa na kidumu kichafu cha dawa unauliza dawa bawasili, vidonda vya tumbo, presha, kisukari, nguvu za kiume, tambazi zote zipo kwa dumu moja kweli hapo ukinunua utakuwa huna akili
Hata ambaye aliniletea, aliniambia ukitaka dawa niambie nikienda nyumbani nikakuletee usinunue Kwa wanaotembeza.. Nimeamini alichokua anakisema
 
Sema vipimo kama ultrasound hakiwezi kutoa majibu ya aina gani au viko kwenye stage ipi,, ndiomana nataka nikapime na endoscopy ili nipate majibu sahihi zaidi
Safi sana. Nimemshauri mleta mada akafanye hii ili awe na uhakika. Mimi ni miongoni mwa watu waliowahi kujihisi kuwa na vidonda vya tumbo, na nilikuwa nafuata masharti na kunywa dawa kama nina vidonda tumboni. Kuna kufanya hiyo endosscopy nikakuta sina vidonda bali uzalishaji wa nyongo ulikuwa mkubwa.
 
Yeah ni kweli,,, Hongera pia Kwa kulishinda hili tatizo maana linatesa sana
 
Pole sana. Nianze kukuuliza, unauhakika una vidonda vya tumbo? Ulifanyiwa vipimo vya aina gani au ni kwa nini unadhani kuwa una vidonda vya tumbo? Nauliza hivi kwa sababu Bongo ni watu wengi sana wanakunywa dawa kwa kitu kinachodaiwa kuwa ni vidonda vya tumbo lakini wengi unakuta hawana. Ningekushauri kwa uhakika zaidi jaribu kufanya gastroscopy uhakikishe.
Hayo majibu nilipewa na madaktari wa hispitali tatu baada ya kupima kuwa nina vidonda vya tumbo na aleji kwa upande wa aleji nilipona lakini hili bado msisitizo ni kuwahi kula kutokuwaza na kula vyakula visivyo na gesi, hiyo gastroscopy sijajua kama nilipima naomba nielekeze mkuu
 
kama una ndugu au rafiki msambaa mwambie akutumie dawa kutoka Lushoto kijiji cha Soni mzee mmoja amespecialize kwenye ugonjwa huo anaitwa Chakua Chakua na siku rahisi kumpata ni siku ya jumanne na ijumaa ni mzee maarufu ukimuuliza mtu yyete hapo Sokoni Soni anamjua bei ya dawa ni 5000 na unaweza kumlipa baada ya kupona kama huna hiyo hela
 
Hayo majibu nilipewa na madaktari wa hispitali tatu baada ya kupima kuwa nina vidonda vya tumbo na aleji kwa upande wa aleji nilipona lakini hili bado msisitizo ni kuwahi kula kutokuwaza na kula vyakula visivyo na gesi, hiyo gastroscopy sijajua kama nilipima naomba nielekeze mkuu
Gastroscopy ni mpira mwembamba mrefu unaoingizwa kinywani, unashuka kupitia kooni mpaka tumboni. Huu mpira una lensi ndogo kwa mbele yenye taa. Mpira unapofika tumboni ile lensi inaonyesha kule ndani ya tumbo na utumbo mdogo kama kuna vidonda kwa kutumia screen iliyounganishwa na huo mpira. Unaambiwa usile chakula asubuhi kabla ya kwenda kwenye kipimo ili tumbo liwe wazi na lensi iweze kuonyesha. Pia kwa kutumia huo huo mpira wanaweza kuchukuwa maji maji (sample )kutoka kwenye tumbo ili kwenda kupima. Hiki ni kipimo cha uhakika zaidi kuliko kupima choo au kukisia kwa kutumia dalili anazosema mgonjwa. NB: kipimo kinafanyika bila kuwekewa nusu kaputi na hakina shida i.e. hujisikii vibaya kama unavyoweza kudhani kabla ya kufanyiwa.
 
Back
Top Bottom