Dawa ya mtu aliyeziba masikio ni kumuwekea loud speaker, kazi iendelee

Nini tofauti ya makubaliano na mkataba?
 
Kwamba huamini kama rais kasoma mkataba ?
 
Kwamba huamini kama rais kasoma mkataba ?
Inahitaji uwe mkatili sana kuwauza waTanganyika wazima wazima

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Watanzania wengi wajinga mnapiga kelele bila uelewa mngesubiri utekelezaji muone kwa vitendo.
  • Tuone kwa vitendo namna ambavyo kampuni imepewa mamlaka juu ya BANDARI ZOTE ZA BAHARI NA MAZIWA.
  • Unaweza kuwa wewe ndio mjinga kiongozi ambaye hata hujasoma kilichoandikwa, bali unasubiri uone utekelezaji. Ndio wavivu wa kusoma mlivyo. Je unakumbuka hata gesi ilinadiwa kwa ahadi kama hizi, na sasa kimya?
  • Msingi wa DP kupewa BANDARI ZOTE ni ziara ya siku moja, je hiyo si ishara ya 'state capture'?
 
Yaani hadi sasa, hakuna hata hoja moja waliyoweza kujibu
 
Uchumba? Mnatia saini makubaliano? Uchumba wa wapi huo? Henu weka hata clip moja watu wanapovishana pete ya uchumba wakatia saini cheti cha uchumba, labda mi nimepitwa na wakati..

Boss umepitia finance.

Unajua manufaa ya uchumba ktk finance.

Wenzio hiyo ni heshima kwao na faida kwa upande wa usimamizi wa pesa.

Haya si makubaliano ya uchumba wa kwampalange.
Sasa kama hujui masuala ya finance nikupe hongera kwa misimamo ulionayo na Umeshinda wewe.
 
Wewe si ndio umelinganisha hayo makubaliano na uchumba? Au sio wewe? Sasa uchumba huwa kuna makubaliano yanayotiwa saini baina ya wachumba? Sasa unakimbia nini we mbwa? Rudi hapa! Eleza tofauti ya ‘majubaliano’ na ‘mkataba’, maana hiyo ya uchumba unashindwa kuitetea
 
Hii nchi ni yetu sote. Kila MTU ana haki ya kusikilizwa.
Sudan kuko kulivyo kwasababu Kuna kikundi kilikua hakisikilizwi.

Elimu nyingine sio lazima ufike form six. Hata form foo inaweza kukusaidia.
Toka lini watanganyika tukasikilizwa chief? Wanajua sisi ni waoga,thus why wanatugeuzageuza kama chipsi na hatuna cha kuwafanya.Ingekuwa Nigeria hapo wangekinukisha mbaya hadi wasaniii,kwetu ni kinyume wakina Diamond wanawakatia viuno haohao mabwana
 
Mama anaona Watanzania wana kelele na sio maoni kaamua kama ni mbwai iwe mbwai

Huyu maza ana dharau, utawazibia vipi masikio watu unaosema unawatumikia?
Kama hataki kusikiliza maoni ya wananchi ni vyema ajiuzulu
 
 
Huyu maza ana dharau, utawazibia vipi masikio watu unaosema unawatumikia?
Kama hataki kusikiliza maoni ya wananchi ni vyema ajiuzulu
Hawasikilizi na wala hajiuzulu tuone sasa mtamfanya nini zaidi ya kuishia kupiga mikelele tu humu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…