Dawa ya nywele zilizokazwa sana ni nini?

Dawa ya nywele zilizokazwa sana ni nini?

Jamani hapa nataka nifumue ila hela yangu inauma, lakini naumia kila upande haufai kwa kulala yani nikilalia paji la uso ndo naona afadhali....

Usiku wa leo ukiisha sitakaa kusuka tena nywele za kuumiza hivi aisee. Au nyie warembo mnazipoozaje? Maana
Paka ile Diclopar ya tube

Kanda Kanda na maji ya vuguvugu pembeni.
 
Hizi nywele zenu za kuvuta kama mnataka kung'oa kichwa zinaharibu sana uoto wa nywele hadi mnapata vipara temporary.
Mm sipendi kuvutwa ila leo ndo nimepatikana. Kuna video moja mdada wa naigeria amevutwa nywele yani wakigusa analia kwa yowe nilimshangaa nikasema huyu mbona chizi unasukwaje nywele za hivyo. Mm zangu za kawaida tuu sijui mkono wake mchungu lol.
 
Siku noliyosukwa nikavutwa balaa ikawa hata kucheka siwezi, ndio siku niliyonyoa na sijawahi suka teeena hadi leo.
 
Siku noliyosukwa nikavutwa balaa ikawa hata kucheka siwezi, ndio siku niliyonyoa na sijawahi suka teeena hadi leo.
Mm nilikua nimenyoa nimeanza tena kusuka. Ila duu ngoja nitazitwist tuu kienyeji nikae nazo nisihangaike kusuka
 
Umenikumbusha wakati tunakua kina mama walikua wanapasha machanuo ya chuma moto wanapitisha kwny nywele eti zilainike ila wanawake tuna kazi sana
Usisahau na wengine walithubutu Hadi kuchemsha mafuta ya mawese na kujipaka usoni ikiwa nia ni kujichubua.Ilienda sambamba na kutumia sabuni za mkorogo kama JARIBU,MEKAKO nk.Bila kusahau kupaka nywele kitu iliitwa ZAZUU.Mna mambo mazito ninyi.😂😂😂😂
 
Pana mafuta yanaitwa MpL yanapatikana saba saba Kariakoo hayo ni medicated na pia kwa wale wenye matatizo ya mba au mtu yeyote anaetaka kutumia mafuta ya nywere mazuri basi hayo ni mafuta mimi nimeyapitisha mafuta kwa ajili ya Ngozi ni Nivea sema sio ya Nairobi tumia Nivea ya made Humburg,Spain au SA hiyo nivea ya Nairobi kopo linang'aa tuu ukitumia kama wametwanga mihogo harafu inatengeneza chunusi kwa watumiaji...ni hayo tuu
 
Thanx kwa ushauri mkuu.
 
Back
Top Bottom