Dawa ya Vumbi la Kongo 'hensha' yapigwa marufuku Tanzania

Ni dawa zote zinazotangazwa zinaongezewa sildenafil, hata supu ya pweza huwekewa
 
Inchi hii ina watu wa hovyo sn.
Kweli kabisa mkuu. Watu wanakimbilia miti shamba sijui vumbi la Kongo wakati Kuna Viagra na Cialis wataalam wamekaa maabara miaka na kufanya utafiti natokeo yake iyo vumbi la Kongo usikute ilikuwa unga wa muhogo tu wakawa wanachanganya na Viagra. Hata ile miti shamba ya kimasai yote feki. Dawa zote za asili zote feki kwasababu ni kubahatishabahatisha tu. Halafu Viagra ni effective na bei rahis kuliko hizo vumbi la Kongo.

Ndo maana CCM itatawala muda mrefu Sana.
 
Poleni sana japo mjiandae kupigwa kwani lazima wataibuka wenye dawa mbadala ambazo si ajabu zikawa ndo hatari zaidi.
 
Mkongo umefutiwa usajili na serikali. Kosa ni kuchanganywa na sildenafir, kemikali mama inayotengeneza dawa za kutibu changamoto ya nguvu za kiume maarufu zaidi kwa majina ya kibiashara kama erecto na viagra.
 
Mkuu kuanzia leo naanza kupiga zoezi !! Nirudishe nguvu za asili [emoji3][emoji3][emoji3] nikanunue kamba na raba.

Nitafute na madame mmoja wa demonstration niwe najipima uwezo ulipofikia !!
Nimecheka sana mpaka mama mkwe kamwaga mboga [emoji23][emoji23]
 
Itafahamika, Itajulikana...

Wa baridi watatengwa na walio vuguvugu! Hakika yametimia! Mbeengoo zimefongoooka!
 
Sio zote kwa mfano mti wa quinine ulikuwa ukitumika kutibu Malaria kwa muda mrefu

Na mifano iko mingi sana.
Ndio mkuu. Lakini utafiti waliufanyia wakakaa maabara. Wenzetu hawabahatishi. Kumbuka tu ujinga na upuuz wa kikombe Cha babu. Dawa nyingi hata za kisasa zinatoka kwenye mimea, sumu ya nyoka na kadhalika. Lakini tafiti ya muda mrefu.
 
Hizo viagra ni kwa ajiri ya wagonjwa kama wa kisukari tena inatakiwa wapimwe pressure zao kabla ya kutumia.
 
Ndio mkuu. Lakini utafiti waliufanyia wakakaa maabara. Wenzetu hawabahatishi. Kumbuka tu ujinga na upuuz wa kikombe Cha babu. Dawa nyingi hata za kisasa zinatoka kwenye mimea, sumu ya nyoka na kadhalika. Lakini tafiti ya muda mrefu.
Uko Sahihi kabisa sisi ni wavivu wa kufanya tafiti tumekalia Uchawi zaidi kuliko jambo lolote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…