Dawa ya Vumbi la Kongo 'hensha' yapigwa marufuku Tanzania

Dawa ya Vumbi la Kongo 'hensha' yapigwa marufuku Tanzania

unauliza majibu
Nguvu za asili ni zipi? Mcongo sio nguvu za asili?
Imeshapigwa marufuku sasa umkute mwenzio anamkuja mkeo kisha wewe uinue mkono kumgusa uende jela uache watu wakijigongea mtaani.

Wewe wakati wa babu zako waliijua hii mikongo?mnajiharibu mkiwa hamjui.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] nacheka lakini nalia, maana heshima ya kitandani ya baadhi ya wanaume itageuka kilio
 
Mwenyekiti wa Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala , Professor Malebo Hamisi amesema Baraza hilo limeifungia dawa inayoitwa Hensha maarufu kama mkongo yenye namba za usajili TZ17TM0027. Professor Malebo amesema dawa hiyo imekutwa imechanganywa na dawa ya kisasa ya nguvu za kiume inayoitwa Sildenafil kwa jina maarufu la biashara ni Viagra na kusema kuwa Baraza litaendelea kuwafungia wote wanaokiuka Sheria. Aidha akasema Ameagiza dawa hiyo iondolewe mara moja sokoni kabla hatua zaidi za kisheria hazijachukuliwa.

Je unalipi la kusema ? Unahisi ni wanaume wa kundi lipi wataathirika zaidi?
View attachment 2305942WATUMIAJI WA MKONGO WAANGUA KILIO
Vumbi la Congo Limefungiwa Usishangae Vumbi la Msumbiji Likaja Watu Hawapoi na hawaboi.
 
Wakuu,

Nimepata habari kuwa, vumbi la Kongo limefungiwa.

Hili suala linahitaji kujadiliwa kitaifa.

Vumbi la Kongo limekuwa mkombozi kwa wengi. Kulifungia tu bila kufanya critical analysis ya effects zake ni kosa kubwa.

Tunahitaji kupaza sauti ili vumbi la Kongo lirudi sokoni.

Asantee

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Hahaha, wazee wa puturu kazi mnayo asee!!
 
Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Tanzania, limepiga marufuku matumizi ya dawa aina ya Hensha maarufu kama Mkongo kwa binadamu, na kwamba tayari limekwishaifutia usajili baada ya kubaini imechanganywa na dawa za kuongeza nguvu za kiume (Viagra).

Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Prof. Hamisi Masanja Malebo, ametoa kauli hiyo Julai 27, 2022 mjini Morogoro wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Profesa Malebo alisema baraza katika uchunguzi wake, lilibaini dawa iitwayo Hensha maarufu Mkongo, yenye usajili namba TZ17TM0027, ilikutwa imechanganywa na dawa ya kisasa ya nguvu za kiume iitwayo sildenafil, kwa jina maarufu la biashara Viagra ama Erecto.

Alisema kitendo hicho ni kinyume cha sheria na miongozo ya usajili wa dawa za tiba asili na mbadala.

Alisema kituo hicho kimetakiwa kuhakikisha kinaiondoa sokoni mara moja dawa hiyo, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mmiliki.

CHanzo: Habari Leo
KUHARIBIANA SIKU TU HUKO, HUYU PROFESA NAE ZENGWE TU
 
Mtakunywa pweza hadi msahau kama kuna maji duniani, pumbafu kabisa wote mliowahi kutumia hayo makofii oromide.
 
Vumbi la Kongo limekuwa mkombozi kwa wengi. Kulifungia tu bila kufanya critical analysis ya effects zake ni kosa kubwa.

Hujasikia kwamba sababu ya kufungiwa ni vile wanachanganya na viagra?
 
Hivi mwanaume timamu au rijali unatumia huo upuuzi ili ugundue nini.
Mnafeli wapi asee, hamjui mazoezi hamjui diet au hivyo mnaviona vigumu,

ndo maana mashosti wanaongezeka kwa fujo.
F*ck it heal the world dear God
 
Back
Top Bottom