Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Rebeca Sanga amemporomoshea matusi ya nguoni Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina akimuita ni mwanamke (MWALI) huku wananchi wakipigwa na butwaa kubwa kulikoni tena DC kiongozi wa serikali kuanza kutukana watu hadharani.
"Namuagiza Luhaga Mpina huko aliko kama yeye amesema hiki ni kikao cha harusi basi MWALI atakuwa yeye MPINA" Tarehe 29/05/2023 kwenye mkutano wa hadhara kijiji cha DALA.
---
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Rebeca Nsemwa ameunda timu ya wataalamu nakuipa siku 14 kuchunguza malalamiko ya wananchi wa Vijiji Vitatu vya Dalla ,Mbwade na Kongwa wilayani Morogoro baada ya kudai kuvamiwa kwa njia za udanganyifu ardhi yao yenye ukubwa wa zaidi wa ekari 1000 na mwekezaji Luaga Mpina.
Mkuu huyo wa wilaya amesema hayo ikiwa ni siku moja baada ya taarifa za wananchi hao kusambaa katika vyombo mbalimbali vya habari wakiomba Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt SAMIA SULUHU HASSAN kuingilia kati mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka 12 bila ya mafanikio.
Akizungumza na wananchi hao mara baada ya kupokelewa kwa mabango yanayoshinikiza kumkataa mwekezaji huyo LUAGA MPINA wananchi hao wamelalamika kukosa ardhi ya kilimo kwakuwa asilimia kubwa wamekuwa wakitegemea kilimo kuendesha maisha yao ya kila siku.
Aidha wameiomba serikali kupima ardhi yote inayoshikiliwa na mwekezaji huyo pamoja na mipaka ili kujua ukubwa halisi wa ardhi anayoikalia kwa njia za udanganyifu tangu mwaka 2009.
Kufuatia malalamiko hayo,mkuu wa wilaya ya Morogoro REBECA NSEMA amelazimika kuunda timu ya wataalamu watakaofanya kazi ya kupima eneo lote linalokaliwa na mwekezaji huyo ndani ya siku kumi na nne ili kuweza kutoa haki kwa pande zote mbili.
Aidha mkuu huyo wa wilaya ametaka mwekezaji Luaga Mpina kutoa ushirikiano kwa timu hiyo na kuwasilisha nyaraka zote zinazompa uhalali wa kumiliki aradhi hiyo inayolalamikiwa na wananchi kwa muda mrefu.