Mimi sijui chochote na Sina Elimu yeyote ya kupambanua Mambo zaidi ya kuzozana na akina fulani hapa Ila kwa maelezo haya ya DCI hapa tumepigwa mchana kweupe, huhitaji kidgree Cha chuo Cha Amazon Ila narudi Tena kusema tumepigwa hakuna mtu humo
 
Mbowe nae si gaidi,kwa hio nae anaweza akabeba bunduki vile na kupambana na mapolisi kwa style ya Hamza?
 
Hilo swali la kwanini aliwinda police tu jamaa wanajifanya Kama hawalioni.Wanaruruka tu Kama maharage ya mbeya yanapotaka kuiva.
 
Nilijua tu majibu yatakuwa ya namna hii.

Mnakanusha kuwa hakuwa anamiliki migodi halafu mnakiri kuwa alikuwa na migodi.
 
Definition ya "kuishi kisiri siri" inasemaje?
 
Matangazo mengine ni kuichafua nchi tu, nadhani Tz saizi tunashida ya lidashipu
 
Nilijua tu majibu yatakuwa ya namna hii.

Mnakanusha kuwa hakuwa anamiliki migodi halafu mnakiri kuwa alikuwa na migodi.
Natamani kujua hio office ya CCM aliwajengea lini ili nijue anaposema jamaa mambo ya madini alikua ametoka tangu zamani alimaanisha zamani ipi?
 
Hili nalo mmeamua kujichafua ili mpate kwa kumukamatia mbowe munaamua kuuaminisha umma kua kuna ugaidi tanzania yani hamuelewi tu nyie ccm kweli????
Kuna kazi maalum aliyopewa Hamza na lile kundi lililoratibu kesi ya Ugaidi Kwa Mbowe. Hamza kakosea au kaamua Kwa makusudi kutekeleza tofauti na makubaliano yao. Polisiccm sio wakumuamini hata kidogo.

Tujiulize kwanini tukio lile linalosenwa na Polisi ni la kigaidi lilifanyikia mbele ya ubalozi wa Ufaransa?? Tujiulize pia kwanini Polisi hao hao wameshindwa kufanya uchunguzi dhidi ya shabulio la Mh Lissu? Wakati ule walisema hawakupewa ushirikiano na Dereva wa Mh Lissu. Je ni nani aliyewapa ushirikiano kwenye tukio la Hamza??

Polisiccm endeleeni kujianika mkishakauka tutawaanua.
 
kweli alikuwa gaidi kwa uchunguzi ulio ona vip hujatuambia bastola alitoa wapi
pia ailkuwa anaishi kwa siri
kama aliishishi kwa siri ujumbe wa chama fulani aliuupataje? mbona picha na clip zake ziko mitandaoni huo usiri ni upi si mlisema mkazi wa upanga? au ok ngoja tuamini tulio wapa zamana
 
Mjumbe wa mkutano Mkuu wa CCM ngazi ya wilaya, Hamza (R. I. P) bado naamini umekufa na siri nzito sana kuhusu kitu kati ya wewe na Jeshi la polisi.
Narudia kutazama ile video clip, kwa hekima anaitazama daladala iliyojaa raia abiria wenye hofu kubwa. Anaiacha, anakwenda katikati ya barabara anaanza kuongoza magari yapite haraka. Anachagua kushughurika na askari tu!

Magaidi Duniani wa kujitoa muhanga wasinge acha ile daladala vile maana njia pekee kwao kutuma ujumbe kwa Serikali huwa ni kuua innocent souls ili mamlaka zipakazwe tope la lawama.

Kesi ya Zombe na wenzake, Tume ya polisi ilikuja na matokeo kwamba wale wafanya biashara walikuwa MAJAMBAZI. Baada ya kelele nyingi ikaundwa Tume Huru ya majaji ikabaini hawakuwa MAJAMBAZI.

Polisi yajichunguza!
 
Hilo halina Ubishi.
Hamza alikuwa Gaidi namba 2.
ndio maana karibia wafuasi wote wa Chadema walimtangaza Hamza kama shujaa wao, inathibitisha kuwa Chadema wanaunga mkono kwa 100% vitendo vya kigaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…