Bro kusema "Field zote ni equally top," lakini ukweli ni kwamba si kweli kwamba taaluma zote zina uzito sawa katika kila muktadha wa maisha your statement is false bro please clarify it again.
Ni lazima tukubali kuwa kuna taaluma ambazo ni msingi wa maisha ya binadamu kwa ujumla, kama vile udaktari na computer science Hatuwezi kusema udaktari uko sawa na tourism sijui hotel management kwa mfano, kwa sababu afya ni msingi wa uhai, ilhali tourism ni sekta ya huduma inayosaidia uchumi lakini siyo hitaji la msingi kwa maisha.
Mfano mzuri ni huu: Kama kuna nchi isiyo na madaktari, watu wake watakufa kwa magonjwa ambayo yanaweza kutibika. Ila kama nchi hiyo haina tour guide au watu wa hotel management, bado itaendelea kuwepo bila tatizo kubwa. Vivyo hivyo, dunia ya sasa haiwezi kuendelea bila computer science kwa sababu kila kitu, kutoka afya, communication, fedha, hadi elimu, kinategemea Technology.
Kwa hiyo, kusema "taaluma zote ni sawa" si sahihi. Ukweli ni kwamba taaluma zote zina umuhimu kwa kiasi fulani lakini Kuna top tàaluma, ila zina viwango tofauti vya umuhimu kulingana na mchango wake katika maisha ya binadamu.