Deni la Taifa lafika TZS trilioni 91.03

Sahivi wanakopa kila cku, na unategemea nn
 
Mama mama mama weeeeee hakika unaupiga mwingi hadi unamwagika
 
Hivi tumeshindwa kuchukua maamuzi magumu kwa ukopaji huu?
Tuelekee Bungeni
Kama wananchi tunahitaji maelezo
Kikundi cha watu au mtu mmoja anaamua hatma ya Tanganyika ?
Kwa tumelogwq

Mods tafadhalini msifute comments zetu… Sisi ndio walipa kodi tuna haki ya kuhoji……
 
HIVI NI KWELI DENI LA TAIFA LIMEFIKA TRILLIONI 91.?

Uko Twitter na Jamii forum kuna watu washaanza kumsingizia Hayati Rais Magufuli, sasa niliweke sawa jambo hili, baada ya kifo cha Hayati Rais Magufuli,Waziri wa fedha alitoa taarifa kuhusu deni la Taifa nami nanukuu;-

"Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba leo amewasilisha bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Dkt. Mwigulu Nchemba amesema hadi Aprili 2022, deni la Serikali lilikuwa shilingi trilioni 69.44 ikilinganishwa na shilingi trilioni 60.72 kipindi kama hicho mwaka 2021."

Shame on you mnaemsingizia Marehemu.
 
Uko Twitter na JamiiForums kuna watu washaanza kumsingizia Hayati Rais Magufuli, sasa niliweke sawa jambo hili, baada ya kifo cha Hayati Rais Magufuli, Waziri wa fedha alitoa taarifa kuhusu deni la Taifa nami nanukuu;-

"Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba leo amewasilisha bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Dkt. Mwigulu Nchemba amesema hadi Aprili 2022, deni la Serikali lilikuwa shilingi trilioni 69.44 ikilinganishwa na shilingi trilioni 60.72 kipindi kama hicho mwaka 2021."

Shame on you mnaemsingizia Marehemu.
 
Inamaana inchi inaongozwa kwa kukopa sasa isee..mbona deni linapaa sana..
 
Wanaomnanga marehemu!

Wamekata tamaa ya namna ya kumpigania Mama na kumuokoa na yanayoendelea!

Sasa wanapiga KELELE kama chura !
 
Naomba kujuzwa, Jiwe aliacha deni kiasi gani ili tujue na Bi Tozo naye kakopa kiasi gani?

Kama, kwa mfano 2021, Feb, deni lingekuwa 76t, ina maana 91.03 - 76 = 15.03

Kwa mwaka mmoja itakuwa tumekopa 15t, Jiwe alikopa ngapi kwa miaka 5?

Zote kwa ujumla wake tumefanyia nini? Tangible?

Spain walipiga pasi 1055 dhidi ya 359 za Morocco, ni kweli waliupiga mwingi ILA ndo hawakuwa wakiona goli.
 
Hii nchi ni masikini jamani hata wewe ukapewa uwaziri wa fedha au urais sahivi utakopa tu.

Hii nchi wananchi wengi vipato ni vidogo sana na tunaishi maisha ya kudunduliza kiasi serikali inashidwa hata kukusanya kodi maana hakuna cha kuchukua.

Na wananchi wenyewe wanalawama balaaa..
 
nifahamishe... Deni la ndani linatokana na nini?????? au ni ndani ya Africa au Ndani ya Tanzania???? na kama ni ndani ya Tanzania How? Jamani mimi poyoyo wa elimu ya uchumi nielimishwe
Deni la ndani ni Bonds za BOT
 
Ndo shida ya kukimbia hesabu.
 
Taifa la wapiga kelele. Kura hata hampigi kazi kulalamika tu
 
Kuna mamna nyingi ya kupunguza makali ila tuna viongozi ambao hawana upeo., fikiria nchi haina vifaa vya uokoaji ila kila mwaka wizara zinapitisha bajeti ya kununua magari ya milioni 500, waziri analuka na helikopta nchi nzima kufanya kazi ambayo ingewezekana kufanywa na wajumbe wa nyumba 10 hivi unajua gharama za kurusha helikopta angani kwa saa moja tu achilia mbali posho na gharama zingine za msafara wa waziri

Mimi ningekua rais kwa uchache tu ningefanya yafuatayo
1. Ningeondoa mishahara na kiinua mgongo cha wabunge pamoja na kupunguza 75% ya posho zao za vikao. Ubunge ingekua kazi ya kujitolea serikali itagharamia maradhi na posho kipindi cha mikutano ya bunge mikutano ikiisha wabunge wote wanarudi mtaani kuendelea na shghuli zao za kuwaingizia kipato

2. Ningesomesha wanafunzi chuo kikuu kwa kuangalia uwiano wa fursa za ajira zilizopo kwa wakati husika na idadi ya wanafunzi wanahitimu. Kwann nipoteze pesa kusomesha injinia au mhasibu alafu baada ya kuhitimu eti ajiajiri kuwa machinga au bodaboda hv tushawahi kupiga hesabu kujua gharama tunazoingia kusomesha hizi degree ambazo zipo mtaani bila kutumika.

3. Ningefatilia background ya mikopo yote kama kuna pesa ilitapanywa iwe kwa uzembe wa kiongozi au ufisadi basi wahusika wote wangehusika kuilipa au laah mali zao zinataifishwa.
 
Ukiona picha ya Mwigulu tu, ujue anasaini mkopo.
Hawa watu wetu wana idea tutalipaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…