Dereva wa basi la shule adaiwa kumnajisi Mtoto wa miaka 5

Dereva wa basi la shule adaiwa kumnajisi Mtoto wa miaka 5

Alafu hautawahi kuona mbwa kaenda kwa mbuzi, punda kwa ng'ombe nk. Wanadamu ndio tunatumikishwa na shetani lakini wanyama wako vzr tu.
... Shetani anamwonea wivu mwanadamu kwani, kwanza ndiye kiumbe pekee aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu; hata malaika hawakupewa heshima hii ya ajabu; pili, Mungu mwenyewe (Yesu Kristo) kashuka kumkomboa wakati Shetani hata nafasi ya kusema "samahani" hakupewa; tatu baada ya maisha haya, makao yake ni Mbinguni (kwa watakatifu).

Shetani akikumbuka uzuri wa Mbinguni (maana mwanzo alikuwa huko) anafura kwa hasira; anafanya kila afanyalo ili "tukose wote". "Wanyama wako vizuri" kama unavyodai maana, Shetani hana muda nao maana baada ya maisha haya habari zao zinakuwa zimepotea - hawakuumbwa kwa sura na mfano wa Mungu; hawakukombolewa; Mbinguni hakuwahusu.
 
nasema kila siku ,,,,hawa wapuuzi wahasiwe...then waachiwe huru...
 
Hatari sana hii, wazazi hatuna budi kuwa makini,

Hizi habari hua unazitoa wapi Miss Zomboko, wewe na Beth habari zenu ni huzuni tuu.
Atakuwa mwandishi wa habari huyu,habari zake nyingi huwa naziona pia Mwananchi......imeripotiwa Mwananchi leo nadhani
 
Wapo wanawake watu wazima wanaofanya ngono na vijana wadogo kwa kuwarubuni....
Mkuu hii haina shida sana. Ukisikia mtoto wako wa kiume kabakwa na mdada wa shule. Mimi kama mzazi ntatembea kifua mbele mabega juu kwamba nimezaa kidume kweli kweli
 
Utakuta wazazi wanawahamisha watoto. Huo sio uamuzi sahihi keani dreva hakutumwa na shule kufanya hayo
 
Dunia iko hivyo miaka na miaka, wakati huu taarifa zinaenea kwa haraka tu.
Tunaishi kwenye nyakati ngumu sana.....

Ni nyakati ambazo wanadamu wameshaachana na matumizi ya fahamu badala yake waanaenenda kama wanyama.....

Ni nyakati ambazo zimejaa mashaka, hofu ,wasi wasi na majuto kuliko furaha.....

Ni nyakati ambazo uaminifu na utu vimekuwa vitu adimu sana kiasi kwamba watu wema wanaonekana wajinga na jamii inawashangaa....

Kuishi nyakati hizi na kubaki salama kunahitaji bahati pamoja na kudra za muumba pekee maana mioyo ya watu imejaa chuki na visasi ili hali nyuso zao zinatabasamu na kucheka......
 
Huu mchezo wa madereva kukaa peke yao na watoto kwenye gari bila kua na mdada (awe kama matron) kwenye gari sio wa kuvumilika. Kila bus liwe na dereva Ila na mdada wa kuwaongoza watoto.
we acha tu, wadada wa kazi usiseme wana wagegeda kanini, yaani uncle akifika utashangaa dada anavyokurupuka ndani,
 
Huu mchezo wa madereva kukaa peke yao na watoto kwenye gari bila kua na mdada (awe kama matron) kwenye gari sio wa kuvumilika. Kila bus liwe na dereva Ila na mdada wa kuwaongoza watoto.
Mimi shule wanangu wanasoma kila gari linakua na mwalimu,sinaga ujinga wa kusomesha shule za bora liende
 
Nadhani hii Ni fursa mwa mabinti kusomea udereva wa hizi school bus.

Bora kumpa Binti aendeshe school bus kuliko mwanaume. Na ninaiona ni fursa ya wazi sidhani Kama Kuna mdada akiomba kazi atakosa.
Hata kama basi litaendeshwa na mwanamke bado kuna umuhimu wa kuwa na mtu wa kuwaangalia hao watoto. Dereva hawezi kuendesha gari huku akiangalia watoto. Huyo mwenye mtoto aliyebakwa aishtaki shule au serikali iunganishe shule kwenye mashtaka. Mtoto wa miaka mitano hawezi kuwa kwenye gari bila uangalizi. Muda wote mtoto anapokuwa kwenye basi yuko chini ya uangalizi wa shule. Chochote kinachotokea shule inawajibika.
 
Back
Top Bottom