PreGE2025 Devota Minja mkutanoni CHAUMMA, asema hakuna nchi iliyowahi kuzuia uchaguzi labda kuwe na vita

PreGE2025 Devota Minja mkutanoni CHAUMMA, asema hakuna nchi iliyowahi kuzuia uchaguzi labda kuwe na vita

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kama chama cha upinzani A kukitoa chama tawala madarakani chama hicho cha upinzani A kinahitaji wafuasi wengi wa kukipigia kura, na kinaweza kupata wafuasi hao kutoka chama kingine cha upinzani B, then it makes sense chama A cha upinzani kukipinga chama B cha upinzani na kuvutia wafuasi kutoka upinzani (chama B).

Huelewi wapi?
Ndio maana toka awali nikasema, sisi wapiga kura tunahitaji sera nzuri za kimaendeleo zitakazoleta ustawi bora kwa mwananchi na nchi kwa ujumla. Na wala sio hayo malumbano.
 
Ndio maana toka awali nikasema, sisi wapiga kura tunahitaji sera nzuri za kimaendeleo zitakazoleta ustawi bora kwa mwananchi na nchi kwa ujumla. Na wala sio hayo malumbano.
Malumbano ni sehemu ya haki ya kujieleza ya wananchi na wanasiasa.

Kama unataka sera na huzioni unaona malumbano, waadhibu wanaoleta malumbano unayoona hayana tija kwenye kibox cha kura.

By the way vyama vyote vya siasa Tanzania vinafanya malumbano.

Wote wanafanya malumbano, CCM, CHADEMA, CHAUMMA, etc.

Sasa kwa nini uwa single out CHAUMMA kwenye hili?
 
Huyu mama azungumzie agenda za chama chake, ajitahidi kuachana kusemea au kujibu agenda za Chadema.

Vv
Kwani yanajitambua basi, wao wanajiendea tu hata wanako kwenda hawakujui.
Kwa akili zao finyu na walivyodanganywa eti agenda yao ni chadema, ni punguani tu ndio anaweza kuwaelewa
 
Suala la ukabila limeanza kuwatafuna kwani hata uwezo wao wa kufikilia tayali umepelekwa kwa pilato, kwa hiyo wao wanachokijua ni chadema tu, wakilala, wakienda kuoga ni chadema tu, watashangaa sana,
Badala waongelee shida za wananchi mnakaa kubwabwaja kutwa nzima, KUMBUKENI WATANZANIA SIO WAJINGA
 
Wakuu

Baada ya kukimbia CHADEMA na kwenda kupewa Ukaimu Makamu mwenyekiti wa chama cha ukombozi wa umma CHAUMMA Devota Minja amesisitiza chama hicho kushiriki uchaguzi akisema hakuna nchi iliyowahi kuzuia uchaguzi pengine pawepo na vita.
View attachment 3340898
 
Malumbano ni sehemu ya haki ya kujieleza ya wananchi na wanasiasa.

Kama unataka sera na huzioni unaona malumbano, waadhibu wanaoleta malumbano unayoona hayana tija kwenye kibox cha kura.

By the way vyama vyote vya siasa Tanzania vinafanya malumbano.

Wote wanafanya malumbano, CCM, CHADEMA, CHAUMMA, etc.

Sasa kwa nini uwa single out CHAUMMA kwenye hili?
Chaubwabwa kwa hoja wanazokuja nazo kwa kuAttack Chadema hawatafikia mbali, Chadema haiko madarakani kusema kwamba wamekuja na hoja na sera mbadala za kufanya mapinduzi.
 
Chaubwabwa kwa hoja wanazokuja nazo kwa kuAttack Chadema hawatafikia mbali, Chadema haiko madarakani kusema kwamba wamekuja na hoja na sera mbadala za kufanya mapinduzi.
Inaonekana post #40 ama hujaielewa, ama una mahaba sana na CHADEMA imekufanya kipofu usiyeona.

Halafu wewe mwenyewe unafanya kosa lile lile unalolikataa la watu wa chama cha upinzani kukisema vibaya chama kingine cha upinzani.

Kama watu wa chama cha upinzani hawatakiwi kukisema vibaya chama kingine cha upinzani, kwa nini wewe unakisema CHAUMMA badala ya kuisema CCM?
 
Mimi sina chama na naona mapungufu mengi kwenye vyama vyote vya siasa Tanzania. Naweka hili wazi ili nieleweke naongea kidhahania si kutetea upande wowote.

Kwa Chama cha siasa kinachopigania ushawishi, kujibu ajenda za chama tofauti ni ajenda ya chama.

Huelewi wapi?

CHADEMA kinaweza kufanya siasa bila kitaja mapungufu ya CCM?
Kwa hiyo ushindani wa CHAUMA ni dhidi ya CHADEMA na siyo CCM?
 
Ni ajabu Chama pinzani kukishambulia chama kingine pinzani! Lengo la chama chochote ni kuchukua madaraka ya kuomgoza nchi hivyo vita zote huelekezwa kwa aliye madarakani. Ukiona mpinzani anamshambulia mpinzani mwenzie anayeikosoa serikali basi jua huyo mpinzani ni pandikizi
Na huyu anayewatetea ni pandikizi au hajitambui
 
Wakuu

Baada ya kukimbia CHADEMA na kwenda kupewa Ukaimu Makamu mwenyekiti wa chama cha ukombozi wa umma CHAUMMA Devota Minja amesisitiza chama hicho kushiriki uchaguzi akisema hakuna nchi iliyowahi kuzuia uchaguzi pengine pawepo na vita.

Wanatumia haki yao lakini sura zimewaporomoka wamekua wazee ghafla shida ni nini😃😃😃😃
 
Na huyu anayewatetea ni pandikizi au hajitambui
Inawezekana kutetea hoja ya wapinzani kuwa na haki ya kupingana na wapinzani wenzao bila kuitetea CHAUMMA, kuwa pandikizi wala kuwa mtu asiyejitambua.

Hii ni hoja dhahanifu tu.

Mtu anaweza kutetea hoja hii hata in the abstract tu.

Tatizo watu wengi hapa hawawezi kufanya abstract thought, na siasa zetu ni za kuangalia watu na makundi, si za kuangakia hoja.
 
Kwa nini ubataka kuwapangia mapungufu wayaone wapi?
Kwa chama cha siasa makini lazima waone mapungufu kwa chama kilicho madarakani ambacho kina impact ya maisha ya wananchi directly.

Kuona mapungufu ya chama kinachopigania haki kwa wapinzani na wananchi na si chama tawala ni hulka ya vyama pandikizi
 
Hakuna sera ya maendeleo isiyojadili mapungufu.

Maendeleo maana yake ni kuangalia mapungufu na kuyaondoa.
Kwahiyo Chadema ndiyo ina hayo mapungufu ya maendeleo ya kuangaliwa na siyo ccm iliyoshika madaraka ?
 
Inawezekana kutetea hoja ya wapinzani kuwa na haki ya kupingana na wapinzani wenzao bila kuitetea CHAUMMA, kuwa pandikizi wala kuwa mtu asiyejitambua.

Hii ni hoja dhahanifu tu.

Mtu anaweza kutetea hoja hii hata in the abstract tu.

Tatizo watu wengi hapa hawawezi kufanya abstract thought, na siasa zetu ni za kuangalia watu na makundi, si za kuangakia hoja.
Huwezi kanusha kweli inayoonekana kuwa kweli, kwa hali ya kisiasa nchini haikanushiki Kuna taharuki kubwa kwa watawala dhidi ya chama kikuu cha upinzani CHADEMA na kiongozi wake.

Hao waliojiengua CHADEMA kwa kumpinga Lissu hadi kusaliti dhamira zao. Kujiunga na chama kingine na press conference yao ya kwanza badala ya kuongea sera zao ni kushambulia CHADEMA inadhirisha ni mapandikizi ya watawala. Kuwatetea ni pandikizi kubwa au kutojitambua, adui wa wapinzani no CCM
 
Back
Top Bottom