Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 122,494
- 96,074
Binafsi nimeshindwa kumuelewa kabisa huyu bwana mkubwa wa CCM.
Maneno aliyo yaongea na elimu aliyo nayo sidhani kama vinaendana.
HOTUBA YA DR. BASHIRU KWA UFUPI
CCM inatoa salamu za mwaka mpya 2020, niwahakikishie watanzania kuwa tutaongoza siasa safi,ni mwaka wa kuheshimu maoni na uamuzi wa Umma, na tutashinda kwa kishindo kwa kuwa wananchi walihitaji huduma ya maji, elimu bure, afya na sasa wanapata huduma hizo,wananchi sio wanafiki.
CCM inapingana na udhalilishaji unaojitokeza ktk chaguzi, Wanawake kabla ya kugombea wanaitwa majembe, wakichukua fomu za kugombea wanaanza kuchimbwa na kupewa kashfa,wanajazwa hofu na wanaogopa, awamu hii CCM haitakubali wanawake wadhalilishwe na haki ni lazima itendeke kwa wote.
Wapo wanaolilia tume huru iwasaidie kupata ushindi, tume haipigi kura bali inasimamia uchaguzi, chama kisicho na wapigakura kisitegemee tume iwape ushindi, CCM imetafuta wapigakura kwa kutoa elimu bure, afya, maji na barabara, wao waseme wapiga kura wamewapataje.
Wenyeviti wa vijiji na mitaa, ninyi ni wajumbe wa vikao vya CCM kwenye Matawi na Kata, mtusaidie kupata wagombea bora, ikiwa mnaona kuna watu wanawazidi nguvu na kupendekeza wagombea wasio na sifa kwa maslahi yao, leteni taarifa haraka kusaidia Chama.