Dkt Chemical anafundisha nini huko UDSM kama hajui Ndoa ni sehemu ya mafanikio ya mtu both Mwanaume na Mwanamke?

Ndoa ni mafanikio kwa conservative people kama wewe
Na conservative people wanaenda kuisha duniani generation zinazokuja zitakua tofauti kabisa
 
Kwani wapi nimekuambia kuna sheria inakulazimisha kufanikiwa?😀😀😆

Hakuna sheria yoyote dunia hii inakulazimisha kufanikiwa kwa jambo lolote. Iwe kununua gari, kujenga nyumba, kuwa tajiri, n.k.

Unaanza kuumia kijana
Mafanikio binafsi sio mafanikio ya jumla, na kwenye mafanikio kila mtu ana kipaumbele chake.

Kuna mwingine kujenga nyumba, kuwa na gari, hayo sio mafanikio kwake. Inategemea na muhusika mwenyewe.
 
Ndoa ni mafanikio kwa conservative people kama wewe
Na conservative people wanaenda kuisha duniani generation zinazokuja zitakua tofauti kabisa

Kwa Elite na familia zinazotawala dunia wao zitabaki. Wanaondoa kwenu msiojua mambo madogo kama hayo.

Wazungu hapo ulaya wanatafutana kwa Waarabu. Na sababu kubwa ni suala hilihili la ndoa. Lakini wenye upeo mdogo hawalioni
 
Mpaka umeamdika yote hayo,ina maana haujui changamoto yake?
 
Mafanikio binafsi sio mafanikio ya jumla, na kwenye mafanikio kila mtu ana kipaumbele chake.

Kuna mwingine kujenga nyumba, kuwa na gari, hayo sio mafanikio kwake. Inategemea na muhusika mwenyewe.

Mafanikio binafsi ndio huleta mafanikio ya kitaifa. Mzee vipi huelewi mambo haya mbona alafu ni madogo sana.

Mafanikio ya jumla unazungumzia nini?
Mimi nimesema mafanikio binafsi au mafanikio ya kitaifa. Wewe hayo ya jumla ndio kitu gani?
 
Sijasema watu.
Nenda popote sehemu official. Hilo swali linaulizwa sio kama fasheni. Wanamaana zao.

Siku ukianza kuajiri watu utaelewa maana yake. Kwa sasa utaona ni mazoea
Narudia tena ni Mazoea, mbona Serikali ina ajiri hawaulizi umeoa au kuolewa? Na ukiwa kazini hiyo serikali haikuulizi utaoa au kuolewa lini ukiwa na ajira tayari hapo.

Ila hilo swali utaulizwa na watu wanao kuzunguka, mtaani, uraiani au wafanya kazi wenzio hapo kazini.

ni MAZOEA.
 
Mafanikio binafsi ndio huleta mafanikio ya kitaifa. Mzee vipi huelewi mambo haya mbona alafu ni madogo sana.

Mafanikio ya jumla unazungumzia nini?
Mimi nimesema mafanikio binafsi au mafanikio ya kitaifa. Wewe hayo ya jumla ndio kitu gani?
Ewaa!! Mtu ana gari na nyumba kali km unavyodai wewe, ila Hana Ndoa, vipi ana Mafanikio au hana??
 

Serikali gani haiulizi? Hiihii ya Tanzania au serikali nyingine?

Unapoomba kazi CV yako huoni cha marriage status?
Ajira portal ukijaza hakuna hicho kipengele?
 
Kwa hiyo mkuu kwako mafanikio na maendeleo unaona ni maneno tofauti?😆😀
Mafanikio ni kipaumbele binafsi, ila maendeleo ni Yale yanayoonekana kwa umma.

Mtu anaweza kuwa na gari, nyumba, na mali nyingi, ila anaona bado hajafanikiwa, lakini umma ukamuoma mtu huyo ameendelea sana. Au ana maendeleo zaidi.

Sijui unaelewa??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…