Mstahiki Mea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 6,559
- 12,518
Ndoa ni utaratibu wa maisha sio mafanikio.
Sasa hiyo comment umeiona vizuri? Mbona inapingana na falsafa zako, unless leo uwe kigeu geu.
😂😂😂😂
uongo huo mafanikio hayapimwi na mtu kuwa na ndoa ? au familia mafanikio ya kweli ni mtu kuwa na upendo ni wangap wako na familia au ndoa tunasikia kila day mauaji ...mtu aliyefanikiwa ni yule ambaye anafamilia yenye upendo ndoa yenye upendo anayeish kwa upendo ....full stop
Unakimbia kimbia tu, na kila unakozungukia nakujia na mifano hai isiyo na shaka, sasa sijui una maana gani.Kwa uelewa wako unafikiri kwa nini serikali inataka kujua hali yako ya ndoa kama ni jambo lako binafsi? Hujiongezi
Ndoa ni utaratibu wa maisha sio mafanikio.
Sasa huyo mwenzio anataka wanawake wasisome, wala wasiwe na ajira, wala wasiwe na uchumi wao binafsi, kwa kigezo cha kuikimbia ndoa, hata km mwanamke yupo ataitaka ndoa hata akiwa msomi haitakiwi,Falsafa yangu iko wazi.
Watu wapewe elimu kwa usawa. Lakini madai ya watu yanasema wanawake mkipewa elimu baadhi yenu mnakuwa wajinga zaidi. Hamjui mambo muhimu kwenu katika maisha. Mnakimbia ndoa. Na hili kwa sehemu naliona lipo.
Ila kwa wanawake watibeli tangu zamani elimu wanapata na ndoa kwao ni muhimu na lazima hasa kama wanataka kuwa Mama bora
Inawezekana akawa na mafanikio bila ya ndoa, lakini leo anatamani awe na mume sema hawezi kutoka adharani kulionge hilo bali anakufa nalo moyoniKwahiyo mkuu,kwako wewe Oprah Winfrey hana mafanikio ?. Au Ian Khama?
Uongooo!!Inawezekana akawa na mafanikio bila ya ndoa, lakini leo anatamani awe na mume sema hawezi kutoka adharani kulionge hilo bali anakufa nalo moyoni
Sasa huyo mwenzio anataka wanawake wasisome, wala wasiwe na ajira, wala wasiwe na uchumi wao binafsi, kwa kigezo cha kuikimbia ndoa, hata km mwanamke yupo ataitaka ndoa hata akiwa msomi haitakiwi,
Sijui unasemaje hapo? Nakuona nakuona unavyokua kigeu geu.
😂😂😂
Wewe tiyari ulishachagua kuwa bwab.wa na kila mtu humu ndani anaelewa msimamo wako. Hili linalozungumziwa hapa sijui kama utalielewa kama lina mantikiWewe ndio unapotosha hapa, unapotaka kuleta kitu ambacho unaona wewe kwako ni muhimu basi unataka wote waone hivyo.
Ndio maana niliweka neno "LAZIMA" hili neno likishakua haina mjadala tena, lakini Ndoa sio Lazima ni hiyari, watoto ambao unataka wapatikane kwa njia hiyo pia sio lazima, na hata kufanya tendo lenyewe ili mtoto atokee sio lazima.
Wewe km mafanikio yako ni Ndoa, ni wewe wala hujapangiwa au kuzuiwa, ila kupangia na kuzuia wenzio wanaoona Ndoa sio Mafanikio, hapo ndio unakosea.
Mara nyingi umekuwa ukiandika viti vya msingi lakini leo kubali umeandika upuuzi mkuuKila kitu kwenye maisha ni utaratibu. Mafanikio yenyewe ni utaratibu
Mara nyingi umekuwa ukiandika viti vya msingi lakini leo kubali umeandika upuuzi mkuu
Hata maendeleo hayana tafsiri/kipimo kimoja, kama ilivyo ndoa.Mafanikio ni subjective mkuu,ila maendeleo ndiyo Yana tafsiri/kipimo kimoja
Hakuna kipimo kimoja cha mafanikio duniani. Ndio maana wengine wakipata milo mitatu ni mafanikio, mwingine akiwa na afya njema ni mafanikio, mwingine akimiliki ardhi, mwingine nyumba, mwingine akipiga picha na mtu maarufu ni mafanikio n.kNdoa ni moja ya vipimo vya mafanikio ya mtu. Hilo mtu yeyote ambaye anaakili timamu analijua. Sasa mtu umeenda shule mpaka umefika chuo kikuu. Ukaongeza na elimu. Unashindwaje kujua jambo dogo kama hilo?
Kila kitu duniani kinaendeshwa na maoni, unadhani kipindi babu zako wanaoa wake 10 au kuzaa watoto 50 haikuwa mafanikio? lakini leo hii imekuja kuonekana sio sawa je nani aliyesema sio sawa? Si maoni ya watu mbalimbali kama wanasayansi, madaktari na maendeleo ya jamii n.k leo hii huwezi onekana umefanikiwa!!Mafanikio hayaendeshwi kwa maoni ya watu.
Kwamba wewe kutokutaka kwenda shule haimaanishi kusoma sio mafanikio.
Kutokutaka kwako kujenga nyumba na huoni umuhimu wa nyumba haimaanishi kuwa na nyumba sio mafanikio.
Kutokutaka kwako kwenda Marekani au kushindwa kuzurura duniani kisa uwezo mdogo. Haimaanishi kutembea duniani sio mafanikio.
Tatizo la wabongo wengi mnashindwa kutofautisha maoni na hoja.
Mtaendelea kuburuzwa sana. Sana kwenye huu ulimwengu. Kwa sababu hamjui mambo ya msingi ni yapi. Na wanaoongoza huu ulimwengu wanajua wafanye nini ili kuwapotosha
Dkt CHEMICAL ANAFUNDISHA NINI HUKO UDSM KAMA HAJUI NDOA NI SEHEMU YA MAFANIKIO YA MTU BOTH MWANAUME NA MWANAMKE?
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Ndoa ni moja ya vipimo vya mafanikio ya mtu. Hilo mtu yeyote ambaye anaakili timamu analijua. Sasa mtu umeenda shule mpaka umefika chuo kikuu. Ukaongeza na elimu. Unashindwaje kujua jambo dogo kama hilo?
Dkt Chemical anakuambia ndoa sio kipimo cha mafanikio kwa wanawake. Angesema sio kipimo pekee ingekuwa sawa kwa sehemu kwani ni kweli yapo mafanikio mengine na vipimo vingine vya mafanikio
Yapo mafanikio ya aina nyingi.
Yapo mafanikio ya kiuchumi. Kisiasa, kiteknolojia, kijamii n.k.
Ndoa ni mafanikio makubwa. Ni kipimo cha mafanikio. Kwa mtu yeyote sio mwanamke bali hata mwanamke.
Inashangaza mtu aliyefika chuo kwa level ya degree asijue jambo dogo kama hilo.
Hoja ya kusema mtu amefanikiwa maeneo mengine kama mafanikio ya kisiasa, kielimu, kiuchumi haiondoi umuhimu wa ndoa. Na kuifanya kuwa sio kipimo cha mafanikio.
Ni sawa mtu akuambie kusoma sio mafanikio.
Au akuambie kumiliki nyumba au gari sio mafanikio. Ni mjinga huyo. Hana uelewa mzuri.
Kupata elimu ni mafanikio. Na nikipimo cha mafanikio.
Suala la matumizi ya mafanikio hayo, elimu hiyo, teknolojia hiyo hiyo ni ishu nyingine kabisa.
Mtu anaweza kutumia mafanikio yake vibaya. Lakini haimaanishi mtu huyo hajafanikiwa katika eneo hilo.
Hatutaki madokta uchwara wasioweza kufikiri sawasawa.
Dokta unatakiwa uongee kama Elites, mwanafalsafa, mtaalamuna. Sio uongee maoni kama kina Gigymoney au celebrities wengine ambao wao sio wasomi.
Hakuna kupeana moyo. Dokta na profesa lazima muongee mambo kwa ukweli wote.
Kuna mafanikio artificial ndio kama hayo ya kupewa elimu ya mkoloni, ununuzi wa magari, ujenzi wa nyumba.
Na kuna mafanikio ya asili ambayo ndoa ni mojawapo. Ndoa ndio inapelekea watoto na familia.
Sasa mtu anashindwa kuelewa mambo madogo kama hayo.
Kasikia Wazungu wajinga wajinga wakiongea hivi naye anafuata mkumbo anaongea vilevile bila kutafakari.
Nasema wazungu wajinga wajinga maana wapo wazungu wenye Akili pia.
Dkt Chemical, ndoa ni kipimo cha mafanikio yako.
Familia inaundwa kwa ndoa umesikia Dokta.
Sasa kama msomi hujui familia inaundwaje, huko chuo hao vijana unawafundisha vitu gani.
Au unafikiri watoto wanaokotwa?
Au ndio matokeo ya uzinifu. Maana wazinzi wao kwao ndoa sio mafanikio au kipimo cha mafanikio.
Mtu anazaa kama mbwa. Leo huku kabebeshwa na huyu kesho kabebeshwa na yule. Huyo mtu kwake ndoa ndio haina umuhimu.
Watoto wanakuzwa kichokaraa. Leo wapo huku kesho wako kule kama mpira wa rugby. Hao ndio utawaambia ndoa sio mafanikio watakuelewa.
Wewe kila mtoto na baba yake au na mama yake huwezi kuona ndoa kama ni sehemu ya mafanikio.
Malezi ya baba na mama msingi wake mkuu ni ndoa. Alafu mtu anakuambia ndoa sio kipimo cha mafanikio.
FaizaFoxy ndio maana anawatukanaga mmeenda kusomea ujinga huko.
Kuvunja ndoa ilivyo kazi. Wazazi, serikali na taasisi za kidini zinatumia njia nyingi kuzuia watu kuvunja ndoa kutokana na umuhimu wake. Leo msomi mzima hajui hata ndoa ni nini?
Ndoa ni kama serikali. Sasa kuwa na serikali sio kuwa na mafanikio basi sawa.
Unapokuwa msomi, ni muhimu unapotoa maoni yako uyatoe kwa kuangalia elimu yako watu wasije kukudharau. Wakina Doto magari wakiona hii na wale ambao hawajasoma watazidi kuonyesha dharau kwa wasomi.
Angalia familia nyingi, watoto wengi wanaopata shida ni wale ambao hawapo kwenye mfumo wa Ndoa. Yaani wapo kichokoraa hivi. Baba kule, mama kule. Chokoraa.
Ndoa ni mafanikio. Ila sio mafanikio pekee.
Kama ilivyo. Utajiri, elimu, kusafiri ni mafanikio lakini sio mafanikio pekee.
Dkt Chemical uache kupotosha jamii. Acha kupotosha wanawake wenzako.
Mwisho wa kila mmoja wetu atabaki na familia yake. Na familia inaanzishwa kwa ndoa.
Wewe fundisha hapo udsm utakavyofundisha lakini mwisho wa siku mafanikio yako ya mwisho na hatma ya uzee wako itabebwa na ndoa na familia yako.
Fanya siasa zako utakavyo, fanikiwa kama msanii, sijui mwanasheria, sijui upo ughaibuni lakini mwisho wa siku Familia uliyoianzisha ndio itabeba hatma yako na yale yote uliyokuwa unayafanya.
Nimemaliza. Nawatakia Sabato njema.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Ahahahaha wajina mamboNdoa ni mafanikio Kwa mwanamke tu , mwanaume muda wowote akitaka kuoa anaoa ni kma kwenda dukan kununua sukari futa hiyo mafanikio Kwa mwanaume