Dkt Chemical anafundisha nini huko UDSM kama hajui Ndoa ni sehemu ya mafanikio ya mtu both Mwanaume na Mwanamke?

Sasa hiyo comment umeiona vizuri? Mbona inapingana na falsafa zako, unless leo uwe kigeu geu.
😂😂😂😂

Falsafa yangu iko wazi.

Watu wapewe elimu kwa usawa. Lakini madai ya watu yanasema wanawake mkipewa elimu baadhi yenu mnakuwa wajinga zaidi. Hamjui mambo muhimu kwenu katika maisha. Mnakimbia ndoa. Na hili kwa sehemu naliona lipo.

Ila kwa wanawake watibeli tangu zamani elimu wanapata na ndoa kwao ni muhimu na lazima hasa kama wanataka kuwa Mama bora
 

Unazungumzia ishu nyingine kabisa. Japokuwa upo sahihi.
 
Kwa uelewa wako unafikiri kwa nini serikali inataka kujua hali yako ya ndoa kama ni jambo lako binafsi? Hujiongezi
Unakimbia kimbia tu, na kila unakozungukia nakujia na mifano hai isiyo na shaka, sasa sijui una maana gani.

Nimekuambia Serikali ina ajiri watu wenye vigezo na masharti kulingana kazi au ajira inataka, hiyo ya ndoa ni suala binafsi la muajiriwa.

Mbona wasio oa au kuolewa hawaondolewi kwenye ajira. ikiwa wamekaa kwenye ajira muda mrefu, na hawana ndoa.?
 
Sasa huyo mwenzio anataka wanawake wasisome, wala wasiwe na ajira, wala wasiwe na uchumi wao binafsi, kwa kigezo cha kuikimbia ndoa, hata km mwanamke yupo ataitaka ndoa hata akiwa msomi haitakiwi,

Sijui unasemaje hapo? Nakuona nakuona unavyokua kigeu geu.
😂😂😂
 
Kwahiyo mkuu,kwako wewe Oprah Winfrey hana mafanikio ?. Au Ian Khama?
Inawezekana akawa na mafanikio bila ya ndoa, lakini leo anatamani awe na mume sema hawezi kutoka adharani kulionge hilo bali anakufa nalo moyoni
 
Sawa dada lazima useme uongooo maana ujanani mwako ushapigwa vibuti kadhaa kutokana na tabia yako mbovumbovu . Na sasa uliekuwa nae ni mume wa mtu
 

Mtibeli sio kigeugeu.
Msimamo wetu uko wazi.

Kwanza mtibeli hawezi kuwa na mwanamke maskini asiye na elimu
Ukishajua hilo utaelewa msimamo wangu
 
Wewe tiyari ulishachagua kuwa bwab.wa na kila mtu humu ndani anaelewa msimamo wako. Hili linalozungumziwa hapa sijui kama utalielewa kama lina mantiki
 
Mara nyingi umekuwa ukiandika viti vya msingi lakini leo kubali umeandika upuuzi mkuu

Hakuna siku nitaandika jambo la msingi

Hilo nililoandika ukaliona la msingi ku na makumi na mamia waliliona ni upuuzi.

Mtibeli atabaki kwenye ubora wake siku zote. Pasipo kutegemea akili zenu wasomaji
 
Ndoa ni moja ya vipimo vya mafanikio ya mtu. Hilo mtu yeyote ambaye anaakili timamu analijua. Sasa mtu umeenda shule mpaka umefika chuo kikuu. Ukaongeza na elimu. Unashindwaje kujua jambo dogo kama hilo?
Hakuna kipimo kimoja cha mafanikio duniani. Ndio maana wengine wakipata milo mitatu ni mafanikio, mwingine akiwa na afya njema ni mafanikio, mwingine akimiliki ardhi, mwingine nyumba, mwingine akipiga picha na mtu maarufu ni mafanikio n.k

Kwahiyo usilazimishe maoni ya mtu yafanane na yako, ndoa zenyewe hizi kila siku zinavunjika unadhani hao wanandoa ukiwaambia ndoa ni mafanikio watakuelewa?

Tujifunze kuheshimu maoni ya mtu
 
Kila kitu duniani kinaendeshwa na maoni, unadhani kipindi babu zako wanaoa wake 10 au kuzaa watoto 50 haikuwa mafanikio? lakini leo hii imekuja kuonekana sio sawa je nani aliyesema sio sawa? Si maoni ya watu mbalimbali kama wanasayansi, madaktari na maendeleo ya jamii n.k leo hii huwezi onekana umefanikiwa!!

Hata dini za mababu zako zilikua zinakutibu magonjwa na kuita mvua ila maoni ya wazungu yalikuaminisha kuwa ni uganga na imani potofu. Ndio maana leo hii wewe ukienda kanisani unajiona umefanikiwa kuliko anayeenda kuomba mizimu yenu.

Kwahiyo tunarudi pale pale kuwa maoni ndio yamezaa mtazamo wa mafanikio
 
Haya ni matunda ya we kubinywa kwenye mwendokasi andiko reeefu
 

Ndoa ni mafanikio, kipimo cha mafanikio au vyote kwa mpigo?

Anaandika, Robert Heriel, Mtibeli: "Yapo mafanikio ya aina nyingi. Yapo mafanikio ya kiuchumi. Kisiasa, kiteknolojia, kijamii n.k. Ndoa ni mafanikio makubwa. Ni kipimo cha mafanikio..."

Nimemsoma. Lakini, sijaelewa hoja yake.

Anataka kusema nini kuhusu Dkt. Chemical?

Kila jamii ni mfumo wenye mifumo midago lukuki,

Lakini jamii nyingi zinayo mifumo midogo ipatayo 17, yaani:
  1. Mifumo ya kifedha (financial systems)
  2. Mifumo ya mahusiano ya kimapenzi, ndoa na uzazi (relational and reproductive sexual systems)
  3. Mifumo ya kiutawala (administrative systems)
  4. Mifumo ya maliasili (natural environment systems)
  5. Mifumo ya kiutamaduni (cultural systems)
  6. Mifumo ya nguvu kazi (human labour systems)
  7. Mifumo ya kukusanya, kukoboa, kutunza na kupashana wa habari (information systems)
  8. Mifumo ya asasi za kijamii (social networks systems)
  9. Mifumo ya kimaadili (ethical systems)
  10. Mifumo ya kazi za mikono ya watu (designed systems)
  11. Mifumo ya tunu za kiutu (axiological systems)
  12. Mifumo ya kisiasa (political systems)
  13. Mifumo ya kuweka, kutekeleza na kufuatilia mipango ya mandeleo (praxiological systems)
  14. Mifumo ya kikatiba na kisheria (legal systems)
  15. Mifumo ya kibiashara (enterprising systems)
  16. Mifumo ya kitekinolojia na ubunifu (technological and innovation systems)
  17. Mifuo ya ulinzi na usalama (security management systems)
Mifumo yote hii inaitwa mitaji ya kijamii (social capitals).

Huwa naikumbuka kwa msaada wa kifupisho hiki: "FRANCHISED APPLETS," kama tukichukua herufi ya kwanza kwenye majina yake ya Kiingereza.

Na kila mfumo unavyo vigezo maalum vya ufanisi.

Yaani Key Performance Indicators (KPIs)

Ni wazi kuwa, uzi wake unaongelea mtaji wa kijamii namba mbili hapo juu.

Yaani, "Mifumo ya mahusiano ya kimapenzi, ndoa na uzazi (relational and reproductive sexual systems)"

Katika mfumo huu kuna ndoa (coital society) na familia (parental society).

Ndoa inatokana na tendo la ngono ya jenitalia kwa jenitalia kati ya mwanamke na mwanamume.

Familia inatokana na ndoa baada ya mtoto kupatikana.

Hivyo tunapokuwa tunapima ustawi wa kijamii (community welfare), tunapima ufanisi kwenye kipengele cha "relational and reproductive sexual capital" kwa kuangalia matrimonial rate, birth rate, divorce rate, STI infection rate, GBV rate, transactional sex rate, family size.

Lakini, kama ulivyosema, ustawi wa jamii unapimwa sio kwa kuangalia sekta ya ujinsia pekee, bali sekta zote 17.

Baada ya kuweka msingi huo, sasa hebu nisaidie kuelewa:

Hoja yako ilikuwa ni ipi hasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…