Dkt. Diallo: Sisi Mwanza ndio Wasukuma original na Rais Samia ni Chifu wetu, hao wanaoitwa Sukuma Gang hatuwatambui

Dkt. Diallo: Sisi Mwanza ndio Wasukuma original na Rais Samia ni Chifu wetu, hao wanaoitwa Sukuma Gang hatuwatambui

Wasukuma halisi tunataka kujua ni kina nani wapo nyuma ya kifo cha mpendwa wetu Dr. Magufuli. Vinginevyo huyo chifu wenu na washirika wake wataiona Kanda ya Ziwa chungu. Tupo hapa.
 
Dah... Hivi mmatumbi akitaka kuwa msukuma ...mchakato wake ukoje?....kuuliza si ujinga 🤭
 
Wasukuma halisi tunataka kujua ni kina nani wapo nyuma ya kifo cha mpendwa wetu Dr. Magufuli. Vinginevyo huyo chifu wenu na washirika wake wataiona Kanda ya Ziwa chungu. Tupo hapa.

Wanasemaga ni ugonjwa wa moyo[emoji848]
 
Nilikuwa sijawaelwa wanaosema "acha inyeshe tujue panapo vuja" sasa naanza kuwaelewa.

Huu ni ushahidi mwingine hata kwa wenye uelewa mdogo kabisa kuwa hiki sio chama cha siasa tena bali ni genge lisilokuwa na dira na lengo lake kubwa likiwa ni kuendelea kuishikiria hazina.

Sasa kati ya Jobo na huyu sijui ni nani mkubwa katika chama na endapo mnada utapigwa ni nani atabaki nje ya set kati yao.
 
Naona Diallo kajibu swali kisiasa na si kiuhalisia.
Dialo tuna mfahamu kwa kuwa ni straight talker, na si wengine tunamfahamu tok akiwa kijana.

Kwanza lazima Dialo akubali kueleza kuwa Magufuli hakuwa msukuma, ni mtu aliyelowea toka Burundi huko , na ana historia ya ukimbizi.
Pili, Ili kupata backing ya kisiasa, Magufuli amewatumia sana wasukuma na jina la wasukuma ili aptae mizizi ya kisiasa.
Hilo halina ubishi.

Tatu, Sukuma gang si lazima mtu awe msukuma.
Sukuma Gang ni wale wafuasi wa karibu wa Magufuli, wengine abao wala si wasukuma kama kina kalemani, Doto n.k.
Sukuma ganag is a political coinage ya wafuasi wa Magufuli, wengi wao wanaotoka kanda ya ziwa.

Lkini Mbaya zaidi Sukuma Gang vile vile ni kielelezo cha UKABILA ambao Magufuli alifanikiwa kuujenga, kwa kuteua watu waliokaribu naye na wa kwao.
Hivi kuna umuhimu gani wa kuwa wafuasi wa marehemu?
 
Diallo alipe kwanza vimeo vya TRA. Hizo porojo za kujipendekeza kwa huyo bibi isine kuwa kigezo cha kukwepa kulipa.
 
Chifu mwanamke wapi na wapi wasukuma hawanaga hizo labda malenga wanawake ndo wako kibao
 
Back
Top Bottom