Dkt. Emmannuel Nchimbi afukuzwa uanachama wa CCM

Dkt. Emmannuel Nchimbi afukuzwa uanachama wa CCM

Kama Nchimbi aliyezaliwa, kukua, na kuzeekea ndani ya TANU/CCM bila waa lolote hana maadili, wenye maadili ni akina nani sasa?

Au sifa za kuwa muadilifu ndani ya chama ni zipi?
Kwa hyo zile ziara yalikuwa maandalizi ya kuaga... ila mkumbuke nchimbi ni mwanachama wa kudumu wa nyumba nyeupeee... kwa hyo hlo kwake litaendelea amependa au hajapenda linamhusu
 
Mawardat Msitufanyie hivyo wana 🦁 mbona kila sehemu ni maelekezo
 
Attachments

  • FB_IMG_1787800289226.jpg
    FB_IMG_1787800289226.jpg
    88.3 KB · Views: 8
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imemfutia uanachama wa Chama hicho leo Agosti 26, 2026 aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Emmannuel Nchimbi ambaye alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kustaafu siasa jana Agosti, 25, 2026.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro leo Agosti 26, 2026 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba.

Dkt. Migiro ameeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa mara baada ya kukaliwa kwa vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya chama hicho ambavyo vilijadili suala la maadili ya Dkt. Nchimbi na vikaazimia kwa pamoja kumfuta uanachama mwanachama huyo.

Soma Pia: Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Ni maadili gani ameyavunja?
Nchimbi alikuwa Makamu wa Rais, Kiongozi wa 2 mkubwa kitaifa,
Wananchi tuna haki ya kujua.
 
Ni maadili gani ameyavunja?
Nchimbi alikuwa Makamu wa Rais, Kiongozi wa 2 mkubwa kitaifa,
Wananchi tuna haki ya kujua.
Sahihisho: Nchimbi hakuwa makamu wa Rais halali.

Alikuwa ni makamu wa Rais haramu na Samia siyo Rais.

Hakuna aliyewachagua wawe Rais na makamu wa Rais.

Oktoba 29 hakukuwa na uchaguzi uliofanyika.

Au wewe unakubali kuwa Oktoba 29, 2025, Watanzania milioni 32+ walijitokeza kumpigia kura Samia?
 
Ana roho mbaya sana aliona mwenzake akiwa mwanachama anafaidi?Hivi ccm ni mali ya Rais au wanachama wa ccm?Eti maadili yeye aliyeua Oktoba 29 ndio ana maadili huyu mama ataishia pabaya ni swala la muda
 
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imemfutia uanachama wa Chama hicho leo Agosti 26, 2026 aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Emmannuel Nchimbi ambaye alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kustaafu siasa jana Agosti, 25, 2026.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro leo Agosti 26, 2026 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba.

Dkt. Migiro ameeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa mara baada ya kukaliwa kwa vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya chama hicho ambavyo vilijadili suala la maadili ya Dkt. Nchimbi na vikaazimia kwa pamoja kumfuta uanachama mwanachama huyo.

Soma Pia: Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Atarejea tu...
 
Wenye inferiority complex kila mtu humuona tishio.

Huyu jamaa alikuwa na nafasi ya kupiga tu goli la Nape hapo akawa top.

Sasa hivi atafuatiliwa kama nini na si ajabu naye akapotea mazima maana ataanza yaleyale ya Polepole.

MY TAKE:CDM fuateni njia hii muipige chini ile pipo,ni either upo na sisi au upo na wale,hakuna kuwa huku na kule.
 
Sahihisho: Nchimbi hakuwa makamu wa Rais halali.

Alikuwa ni makamu wa Rais haramu na Samia siyo Rais.

Hakuna aliyewachagua wawe Rais na makamu wa Rais.

Oktoba 29 hakukuwa na uchaguzi uliofanyika.

Au wewe unakubali kuwa Oktoba 29, 2025, Watanzania milioni 32+ walijitokeza kumpigia kura Samia?
Huku kwetu hakuna aliyeenda kupiga kura😹😹😹
Hadi Bibi zetu wale wazee wa Tanu, tulikuwa nao nyumbani.
Mimi mitaa yangu ilikuwa karibu na kituo cha kupiga kura,,Balozi alitufuata nyumbani tukapige kura,,wengine wakamwambia hawana ID .

Ila najiuliza
Nchimbi amefanya nini, mbona hawasemi makosa yake specifically tuelewe alipokosea.
Yaani CCM wana vituko sana.
Hako kamama kanavyotangaza yaani hadi kanatia hasira,
Ngoja nikae kimya kapuku mimi😹😹😹
 
Was it Lissu or Lema, wakimalizana na upinzani watageukana wenyewe. Look what's happening now.

Hata hivyo jamaa alishasema anastaafu na hizo siasa uchwara, hilo limama sijui hata linaweza nini, watu zaidi ya watano kukaa pembeni kwa nyakati tofauti says a lot. Hakuna kiongozi hapo.
 
Huku kwetu hakuna aliyeenda kupiga kura😹😹😹
Hadi Bibi zetu wale wazee wa Tabu, tulikuwa nao nyumbani.
Mimi mitaa yangu ilikuwa karibu na kituo cha kupiga kura,,Balozi alitufuata nyumbani tukapige kura,,wengine wakamwambia hawana ID .

Ila najiuliza
Nchimbi amefanya nini, mbona hawasemi makosa yake specifically tuelewe alipokosea.
Yaani CCM wana vituko sana.
Hako kamama kanavyotangaza yaani hadi kanatia hasira,
Ngoja nikae kimya kapuku mimi😹😹😹
Hata hapa kwetu Bariadi, Simiyu, Wanyantuzu hawakuhangaika na kwenda kupiga kura.

Samia na CCM wenzake wanalazimisha tu kutawala kwa sababu wana bunduki.

ISijali sana kuhusu huyo Nchimbi. Ila wakimuua au wakimteka na kumpoteza kama walivyofanya kwa Polepole, basi wawe tayari kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe.
 
Mi nilimwambia Balozi kadi ninayo na kura sipigi maana mgombea ninayempenda hayupo.😊Nilikuwa siamini kwamba wao wenyewe ndio watekaji,
Sasa naanza kuamini.
Ona Sasa mtu waliyemchagua😹😹😹😹
Hili taifa aliyeturoga ameshafariki😹😹😹😹🙌
Kwa mara ya kwanza top leaders wote elimu mbalimbali za hapa na pale, halafu vichwa kama Nchimbi, Tulia, vipo pembeni🙌

Ngoja nikae kimya mimi
Familia ishanikataza kuongelea siasa😹,Huko social media nyingine nikienda tu kulike au kucheka kwenye comment ya upinzani,,wanascreenshot na kuja kuanza kunitisha kuwa nikafute.Hadi nimeacha Sasa hata kucheka.
Ni vile tu hawajui kama natumia Jf.
 
Back
Top Bottom