DUBULIHASA
JF-Expert Member
- Nov 26, 2016
- 6,138
- 11,989
Haya mambo yanavyoendelea huko Ccm na Serikalini imefikia kipindi nimeacha kufuatilia maana nimeona naweza pata ugonjwa wa moyo ni kisukari bila sababu... Haya majitu yanakera sana.
Acha uhafidhina mambo yanabadiliaka, ule ubabe wa kizamani hauna nafasi tena. Hakuna nafasi isiyozibika na amini nakwambia na sub yake inaweza fanya maajabu. Uspecial mliompachika mzee wa watu umemghalimu haya ni mambo ya aibu diplomats, very senior officer unafukuzwa kwa utovu wa nidhamu.Wataamini tu siku moja. Tuliwaambia kwa sasa ccm ni genge la wahuni! Hawakuamini. Matokeo wameanza kuyaona.
Hapana. Amepimwa kwa mizania ya chama hafai! What else do you want? Katibu Mkuu amemalizia taarifa yake isiyozididi dakika 3; POKEENI TAARIFA HIYO! Not for discussion.
Mm nitaendelea kumlaumu mabeyo, aliona kama amefanya jambo sahihi ila katutumbukiza kwenye shimo lililo na Simba kwa ndani.,...ametukosea sana kwa kuruhuru utaratibu kufuatwa, Bora angeenda kinyume ila angetusaidia km nchi kuliko hivi alivyofanya...nadhani anashuhudia taifa letu likipitia mateso makali na kwa muda mrefuHalmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imemfutia uanachama wa Chama hicho leo Agosti 26, 2026 aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Emmannuel Nchimbi ambaye alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kustaafu siasa jana Agosti, 25, 2026.
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro leo Agosti 26, 2026 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba.
Dkt. Migiro ameeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa mara baada ya kukaliwa kwa vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya chama hicho ambavyo vilijadili suala la maadili ya Dkt. Nchimbi na vikaazimia kwa pamoja kumfuta uanachama mwanachama huyo.
Soma Pia: Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu
Huyu mzala alitukana matusi yote kwenye Tetesi kwa hiyo lazima amponde Emma..Unafikiri wewe unajua kuliko yeye? Kete zinasukumwa mzee
Na nikosa gani alifanya hadi aitwe kwenye kamati ya nidhamu?Kosa kubwa alilolifanya ni kukataa kuhudhuria kikao cha kamati ya nidhamu,kama angeenda,angeondolewa umakamu rais basi,sasa yeye kutoenda ndio kajikuta kwenye hali hii
Nyerere ndiye muasisi wa yote hayaNyerere alitabiri haya ,ccm sio mama yangu
Kapata wazimu wa papuchiNa nikosa gani alifanya hadi aitwe kwenye kamati ya nidhamu?
Chawa amkeni kumekuchaa,🤭
Alienda kinyume na katiba ya chama chaoNa nikosa gani alifanya hadi aitwe kwenye kamati ya nidhamu?
Dr. Nchimbi ni mkongwe ndani ya chama, anajua ni makosa gani ukiyatenda utafukuzwa. Dr. Nchimbi alikuwa anajua siku nyingi kuwa lazima atafukuzwa, na alijua kuwa akifukuzwa atakwenda kuunga juhudi vyama vya upinzani, hata hotuba yake ile yenye ukakasi ililenga hilo. Ndiyo maana aliwaambia wananchi wadai katiba mpya itumike kwenye chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2030. Kwavyovyote vile kauli yake ya kuitaka katiba mpya itumike kwenye chaguzi zijazo haina tofauti na kauli za wapinzani; maana yake CCM ianguke ikibidi kwa kutumia Tume Huru ya Uchaguzi kwenye chaguzi zijazo. Amekikosea chama kwelikweli kwa kumbembeleza mwana kwa wimbo mbaya, sawa na kuimba "OOOh, oyo oyo oyo CCM shindwa, CCM shindwa CCM shindwa kwakutumia katiba mpya chaguzi zijazo kwa Tume Huru na Katiba mpya". Maana na yeye kama Polepole anajua CCM inashindaje kwa kutumia katiba hii.Hata ile Barua waliandika wao hawa hawa waliomfukuza. Wakaisambaza usiku kwa usiku.
Ngoni anaamka anakuta mzigo umetapakaa ghafla Komba anasema ameipokea na ameikubali.
Kesho yake anaitisha kikao kisiri-siri ili ionekane kamati ya maadili ilikaa kumbe walikuja na majibu yao juu na mizugo ya kufuata katiba yao.
Barua wameandika wao.