Dkt. Jakaya Kikwete amtunuku Rais Samia Shahada ya Udaktari wa Heshima UDSM. Sasa ni Dkt. Samia

Sasa inakuaje mwenye PhD ya kupewa naye anampa mwenzake.Wenye zao za halali wametulia tu
 
Rais Samia Suluhu amestahili stashada hii
 
Hakika Anastahili katika hili maana nimewahi kupendekeza kupitia jukwaa Hili kuwa Chuo kikuu Cha Dares Salaam kimpatie shahada ya udaktari wa Heshima kwa kazi kubwa aliyoifanya nchi yetu
Kwa hiyo ukipendekeza ndo jambo jema? Ni uchafu tu na hongo za teuzi. Anayetaka PhD, ajisajili aingie darasani! PhD ni kichwani siyo kupewa na ukaamini.

Hii siyo UDSM iliyosiofika miaka ya 70 na kuwa ni mfano wa watu wenye fikra. Enzi hizi hata VC ni mtu anayepigania wanawake mitaani tu!
 
Yes. Naye kapewa na chuo kimoha huko India. Waonaambiwa alimradi uwe na pesa.
😁
Dr Musukuma(PhD)
Watu wamesoma Kwa jasho na muda ila PhD hawana,anazawadiwa PhD std 7.
 
kwakweli ni mpambanaji bila kutoa order apewe sasa hivi angeishia kuisoma kwenye daftari,umejiwahi
 
Kumbe walikuwa wanamtamani sana Dk JPM?
Wangesubiri angalau hiki kipindi cha mpito kipite, wangempa kwenye ile 'mitano tena'πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ™Œ
 
PhD ya Utu na Ubinadamu wakati Wanasiasa wengi wako Jela, Wapinzani wanadhibitiwa, Watu wanakufa, Hali ya Maisha ni Mbaya, Police kutwa Wanabambika Kesi Raia na hapo hapo Chuo Kikuu kilichotoa hiyo Honourable Doctorate Wanafunzi wananyanyasika, Mikopo hawapati na Elimu waipatayo ni ya kuwafanya wawe Waoga wa Kujitambua na Wavivu Kifikra?

Halafu GENTAMYCINE nikiwa nawadharau na Kuwaambieni kuwa hamna Akili mnakataa na Kunichukia.

Haya nawaombenj sasa mjipange na mniandalie GENTAMYCINE Honourable Doctorate ( PhD ) yangu ya kuwa Mtanzania na mwana JamiiForums mwenye Maono, Akili, Mvuto, Uwasilishaji wa Kutukuka wa Masuala Mtambuka na Ushawishi mkubwa wa Kifikra na Kitaaluma na nitaomba Mgeni wa Kunitunuku awe ni 'Genius' Mwenzangu tu Rais wa Rwanda Paul Kagame sawa?

Mimi ndiyo GENTAMYCINE The Great!!!
 
Za kupewa bure huwa zina amsha fulani
Hadi akina Musukuma wanasema Bashiru ana PhD kama ya kwake[emoji1787]

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
Watu wanazipenda PhD ila hawataki kuzisotea.

Kama mtu anataka kuwa Dr. kwa nini asirudi shule aisotee badala ya kutumia cheo au kununua.

Msukuma kupata PhD darasani a ahitaji kukaa shule miaka miaka 13. Sasa leo kupewa bila kuzitolea jasho ni pathetic. Halafu inaonekana kabisa kuwa watu wamekubali kuwa Msukuma ni Dr..... Seriously!!
 
Dr. Ngongo ambaye ni Dr wa PhD ingawa ana Diploma ya kucheza ngoma kutoka chuo chetu pendwa cha Bwagamoyo anampongeza sana Rais Samia kwa kutunukiwa PhD.

Dr Ngongo anasisitiza na kuvitaka vyombo vyote vya habari ndani na nje kila watakapo mtaja Rais wetu mpendwa na mtukufu kuanza na neno Dr Samia Suluhu Hassan.
Chombo chochote kitakacho shindwa kuanza na neno Dr kitastahili kufungiwa na vile nje vitasusiwa mara moja.

Ngongo kwasasa viunga vya UDSM.
 
Kusoma tena wakati za bure zipo wee! Kuna mtu nilikuwa namuona anavyohangaika alipomaliza nilimpongeza sana.
 
PhD za Shuleni zimebaki kwa wanasayansi tu

Huku kwingine hakuna jipya kila Kitu marudio!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…