Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Bunda walijichanganya wenyewe, Utawapelekeaje Barabara watu wanaokutukana?

Hahahahaha yeye akitukana Watanzania na kutoa VITISHO vya kutoa kichapo ni sawa ila akigeuziwa kibao ni KOSA 😂😂😂😂

“Bunda walijichanganya wenyewe, Ilani hii lengo kutengeneza Barabara kutoka kwa Lugola kule tukaunganishe na ukerewe kuja hadi Bunda baadaye tunaipasua hadi Serengeti lakini utawapelekeaje Watu wanaokutukana?, hata kama ni Malaika utagoma kidogo”

"Lakini utawapelekeaje watu wanaokutukana hata kama ni malaika utagoma kidogo. Mimi sio malaika nina roho na moyo na hata ukiwa na chakula kizuri huwezi ukampelekea mtoto wa jirani utampelekea mtoto wako wa kuzaa kama ana njaa" - Magufuli

View attachment 1559749
Huyu jamaa asipoangalia anaweza kosa kura hata za wajinga anaowategemea

Maana sasa watu wanaanza kuona rangi zake halisi kuwa ni mtu Mwenye roho mbaya, chuki na visasi visivyo vya kawaida
 
Magu usitufokee. Fedha si zako. Ni Kodi zetu. Kwanza tarehe 28 Oktoba 2020 sisi wananchi wa Tanzania tuna JAMBO LETU dhidi yako.
 
Tunaomba kura afu mpiga kura unamsengenya live live!!

Kazi ipo aisee!!
 
Mpeni mapumziko magufuli. Amechanganyikiwa vibaya
Ni heri yeye kuliko hao waliosema tutashtakiwa MIGA halafu hao hao wazungu wakaja kukubaliana na ubia wa kibiashara.

Ni heri yeye kuliko dalali wa wazungu mwenye kuwasilisha maslahi yao.
 
Dalali wa wazungu ni yule aliyetuahidi tutalipwa trilioni 490 na kila mtu atapata Noah alafu leo kawa kimya kama kamwagiwa maji!
 
Unataka upewe Noah ya bure bure bila aibu.

Kampuni iliyoanzishwa ya ubia ina thamani kubwa kuliko hicho ulichotaka upewe bure tu.

Dalali wa wazungu kagonga ukuta,rafiki yake Trippi.
 
Huyu si alitaka kuwa kiongozi wa malaika?

Si alisema maendeleo hayana vyama?

Si amewahi kusema kuwa hata kwa wapinzani anapeleka maendeleo habagui?

Sasa kulikoni anapiga U-turn
Huyu jamaa mwamini kitu kimoja tu kwa kila vitu kumi alivyozungumza/anavyoahidi. Anajua kubadilika badilika hata kinyonga anasubiri sana
 
Amesema ukweli mnageuza maneno huwezi kufanya jambo jema kwa mtu ambaye anakutukana.
lakini kodi kwake unachukua! Baniani baya kiatu chake dawa! Kama kweli kayasema hayo, tukubali kuwa labda aliteleza
 
Watu wanakuja kuona vyuma anavyosema anavyo mwili wake wote. Hata hivyo wingi wa watu katika mikutano ya Lissu huwezi kulinganisha na mikutano ya JPM. Ya JPM inakuwa na nyomi ya kutisha.
Nyomi ya kuja kuona wasanii na tamasha la muziki ndo nyomi la Ccm. Mbaya zaidi mnalazimisha hadi watumishi na wanafunzi wasifanye kazi na kusoma ili waende kwenye kampeni zenu. Kweli Ccm mmeishiwa.

Alafu kwenye kampeni mnalazimisha watu kuchagua watu wenu na kuwatisha hivi👇😂😂😂😂😂 Kweli CCM mmeishiwa

D91FBDD3-4EB6-4BEA-B2AD-5C18BEA16004.jpeg
 
Palipo na mbunge wa upinzani amekuwa akiwaambia wapiga kura sehemu husika walikosea kuchagua, kauli hii imekuwa ikinikera mpaka imebidi leo niseme. Kwa hakika ni yeye ndiye tuliokosea kuchagua maana kwa muda wa miaka mitano tu ameusambalatisha umoja wa kitaifa ambao waasisi wameupigania kwa miaka zaidi ya hamisini.

Ni katika utawala wake kumekuwepo na sehemu zinazoitwa kanda ya ziwa, eneo la kaskazini na sasa eneo la kusini kwa akina Membe, umoja wa kitaifa kwisha kazi. Kiongozi hupimwa kwa kauli na tabia zake ambazo kweli nyingi zina ukakasi. Mzee Mkapa nakumbuka hotuba zake za mwisho wa mwezi alikuwa anasoma, ina maana kitu kikiandikwa huhaririwa kwanza kabla hakijasomwa ili kuondoa kauli zinazoweza kuleta utata, mwenzetu huyu ni kanyaga twende tu bila kujali kauli ni kama risasi ikitoka hairudi.

Rais wakati wa kutawazwa hula viapo viwili kwa mpigo akiwa ameshika biblia au kitabu kingine kwa imani yake, kiapo cha kwanza ni kuilinda katiba, kiapo cha pili kuwatumikia wananchi wote sawa bila ubaguzi wa dini, itikadi, kabila au rangi, sasa kauli ya kusema mlikosea kuchagua inatoka wapi ukizingatia hiki kiapo cha pili?

Mtu huyu bwana mungu tu anasaidia.
 
Lakini kodi wote tunalipa yaani achuki huyu mzee.
 
Back
Top Bottom