Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Msifanye makosa kuchagua kiongozi kwa kujaribu, mtapoteza miaka mitano bure!

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Msifanye makosa kuchagua kiongozi kwa kujaribu, mtapoteza miaka mitano bure!

Kinyume na hapo, tutaishi maisha ya tabu na shida nyingi. Hakika TUMEPATWA.
Atake asitake.....na Ndugai akabariki hii kauli. Itapendeza sana kama huyu ndugu atanyimwa uspeaker maana Ubunge ndo keshajinyakulia kwa kupita bila kupingwa
 
Rais Magufuli amewataka watanzania wachague mtu ambaye wana uhakika na uongozi wake badala ya kutaka kuchagua mtu kwa kujaribu

Dr Magufuli amesema majuto ya kuchagua kwa kumjaribu kiongozi yatawagharimu kwa miaka mitano hivyo fanyeni uamuzi sahihi wa kumchagua mtu aliyewaletea maendeleo yanayoonekana kwa kila mtu, msibahatishe.

Rais Magufuli amesema hayo mjini Magu akiwa njiani kuelekea Mwanza anakosubiriwa na maelfu ya wananchi.

Chanzo: Channel ten.

Nawatakia Dominica yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 
Huko Magu, Magufuli amesikia alitoa vitisho kwa wananchi baada ya kumkataa mgombea wa Ubunge na Udiwani

Magufuli amewaambia hebu wasimchague kisha waone kisha akaendelea kuongea Kisukuma

amesema kama hawatowachagua,wasimuulize kuhusu maendeleo kwakuwa hatotoa pesa ya shughuli yoyote ya maendeleo eneo hilo
 
EhODeVsXYAAlGu_.jpeg


Nachojua mimi huu ni muda wa kuuza sera na sio kutisha wapiga kura na kutumia mabavu. Ni muda wa kushawishi. Kama hali ni mbaya basi ashauriwe kupimzika kidogo ajitafakari na kutuliza mawazo
 
"Hatuchagui Mtu wala sura, hata sura yangu ni mbaya, tunachagua Vyama , huwezi kuchanganya mambo Rais awe CCM wengine Vyama vingine, Mimi sifichagi nawaeleza ukweli fanyeni makosa mtajuta, nileteeni Mbunge na Diwani wa CCM, mkiniletea mwingine itaniuzi"
Kwa hiyo yy ana uhakika kwamba lazima awe Rais?
 
amesema kama hawatowachagua,wasimuulize kuhusu maendeleo kwakuwa hatotoa pesa ya shughuli yoyote ya maendeleo eneo hilo


Ina maana eneo hilo halitawekwa kwenye bajeti itakayopitishwa na Bunge lenye Wabunge wa VYAMA tofauti(Vyama Vingi)?

Mgawanyo wa PESA UKO KWENYE BAJETI INAYOPITISHWA NA BUNGE.

WATANZANIA CHAGUENI WABUNGE WA UPINZANI HALAFU TUONE ATAKAVYOZUIA HIZO PESA,

"HAPATATOSHA"
 
Back
Top Bottom