Condoleeza Rice aliwahi kuwa mshauri wa mambo ya usalama wa Rais wa marekani (Kipindi cha kwanza cha Bush mdogo) ilhali hajawahi kuwa mtu wa ujasusi au mtu aliyepitia jeshii...
Kilichompa kiki sana ni uelewa wake mkubwa sana wa mambo ya soviet ambayo ndiyo aliyafanyia masomo yake ya shahada ya uzamivu. Huyu mwanama walimtumia sana katika kuelewa jinsi ya ku deal au kunegotiate na warusi mpaka ikafikia hatua ya kuumaliza ukomunisti USSR.
Usalama unahusu sera, mipango, mikakati, maamuzi, jiographia ya siasa za kikanda, na mambo mengine..Kwa hiyo tuache porojo porojoo tuangelee tunayoyayeelewa zaidi tusijifanye wajuaji kwenye yale tusiyoyaelewaa..
Chukua clip moja umuone mkurugenzi wa usalama wa kwa Zuma umsikie vitu anavyoongea ndo utafahamu bosi wa usalam kwenye karne ya ishirini na moja anapaswa awe vipi..
Anaongelea mambo ya kushauri kuhusu sera na mahusiano na nchi zingine na pia fursa za kiuchumi kwa nchi n.k. Wengi wakisikia usalama wanapata tu picha za james bond. Kumbe hayo mambo ni ya field tu wakati wa kukusanya taarifa.
Taarifa zikikusanywa zinapaswa kuchambuliwa na watu ambao wapo vizuri kichwani. Na katika uchambuzi IT inaweza kuwa na msaada mkubwa sana...