Dkt. Mollel: CHADEMA walipanga njama za kumpiga risasi Lissu

Dkt. Mollel: CHADEMA walipanga njama za kumpiga risasi Lissu

Basi jamani utata umeisha,bwana mollel unaambiwa anao ushahid wooooteeeeee, ila atautoa tu pale chadema itakapoeleza matumizi ya ruzuku
Kwa hiyo tusubiri jeshi la polisi waongee na msajili wa vyama na CAG kuhusu ruzuku ili kumlainisha bwana mollel atoe ushahidi wake huo
**Halii hii inaonyesha wazi kwamba ukihama cdm kwenda ccm akili zako zinaongezeka sana, Dr Mollel katisha vibaya mno.


View attachment 1017124
Ukiwa CCM automatically unakuwa MPUMBAVU...!! CHADEMA waliposhindwa kumuua Lissu wakaingia kwa Naibu Spika kung'oa sisitivii kamera?
Wakaenda na kwa Kalemani kuondoa sisitivii kamera?
Mengine tutapata majibu yake mbinguni, ila CCM na genge lenu la wahuni hamtaepuka lawama za kumwagwa kwa damu ya jamaa maana mmeonesha dhahiri nia yenu OVU ya kutaka kuendelea kumtenda Lissu vitendo VIOVU ili kupoteza uhai wake.
Mara asipewe pesa ya matibabu, mara afutiwe ubunge, mara azuiliwe mshahara wake, hivi na hao wapelelezi hawawezi kuunganisha nukta kumtambua mhusika wa suala hili???
Niligoma kuunga mkono CCM japo nilikua najifunika na kupandisha bendera ya CCM nikiwa mdogo, I SAW WICKEDNESS IN MY OWN FAMILY WITH YOU CCM. SHAME!!!
 
Kama wasomi tunao wategemea kulisaidia Taifa letu, uwezo wao wa kujenga hoja na kuhoji ndio huu.... Basi tuna safari ndefu sana sana.
Wapinzani ni wauaji, walitaka kumuua Dkt Slaa, ZZK kaponea chupuchupu na tena juzi kati wametaka kumuua wakajifanya eti zito imebidi wamkamfiche hahahaha, genge hili lilishaumbuka
 
Hv hawa wanasiasa wanaabudu Mungu gani? Hv wana dini hawa wanasiasa? Wanaamn kua Mungu yupo? Maana wanausema uwongo hadharani ilihali wakijua ni uongo. Hawajui km kusema uongo ni dhambi? Wanajua kua kuna kufa??? Mungu awafungue na waone madudu yao. Hv kweli Chadema wangekua wamehusika na shambulio la Lisu na ushahidi upo,c wangeshaumbuliwa mchana kweupe? Muogopeni Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nini ushahidi wake asiwape polisi ili wawakamate wahusika,au kwa kuwa ni CHADEMA wenzake basi serikali haina haja ya kushughulika nao?
Akili za CCM bwana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana Lissu huwa hawakopeshi hawa watu kwa huu ushetani wao.

Eti hawa ndio wa kulaumu wanachafuliwa wakati hizi ndio kauli wanazotoa.

Naunga mkono lugha anazotumia Lissu kuwaelezea hawa watu kuanzia mwenyekiti wao mpaka hawa vibaraka wake.

Hawa watu hawastahili heshima yoyote kwa matendo yao ya aina hii.
 
Wapinzani ni wauaji, walitaka kumuua Dkt Slaa, ZZK kaponea chupuchupu na tena juzi kati wametaka kumuua wakajifanya eti zito imebidi wamkamfiche hahahaha, genge hili lilishaumbuka
Hii Inch ina vyombo vya ulinzi, unadhani wasio julikana wangekuwa hao unao wasema leo wangekuwepo? Serekali ingekubali kuchafuliwa kihasi hivi?
 
Kwani nani asie jue ni mpango wa cdm na ndio maana walikua washaandaa na hosp kabisa na usafiri na kila kitu
Husiolijua ni kama usiku wa giza. Kwani hufahamu moja ya walipchangia kumsafirisha Lisu kutoka Dodoma ni Mbunge wa CCM? Je naye alihusika katika maandalizi yake?
Unapotoa hoja jaribu kutumia sehemu ndogo sana ya ubongo kufikiri kabla ya kutoa. Kuna matukio mengi sana yalifuatana baada ya jaribio ya kuuwawa kwake kushindikana ambapo ukifikiri sana hupatimajibu yaliyokuwa wazi, mojawapo la tukio ambalo ni la mwishomwisho kabisa ni la Mheshimiwa Spika kutokujua kama bado TAL yupo matibabuni
 
"Ukiwa unalima shamba lako akatokea nyoka utakimbia kulima watoto wako wafe njaa au utaigonga kichwa ijifie huko ili uendelee kulima uponyeshe watoto wako!"
 
Alichosema yeye ni sample aliyo iba wakati akiwa mmoja wa madaktari waliofanya postmortem ya mauwaji yaliyotokea Arusha kwa mabomu akawambia akina Mbowe,Lema,Selasini kuwa wapeleke sample hiyo South Africa kwa mkemia mkuu kwa kuwa hawakuwa na imani na serikali lakini walikataa wazo hilo Dr Molelly na akaliambia Bunge wawaulize ni kwanini walikataa sample isipelekwe South Africa?
 
Basi jamani utata umeisha,bwana mollel unaambiwa anao ushahid wooooteeeeee, ila atautoa tu pale chadema itakapoeleza matumizi ya ruzuku
Kwa hiyo tusubiri jeshi la polisi waongee na msajili wa vyama na CAG kuhusu ruzuku ili kumlainisha bwana mollel atoe ushahidi wake huo
**Halii hii inaonyesha wazi kwamba ukihama cdm kwenda ccm akili zako zinaongezeka sana, Dr Mollel katisha vibaya mno.


View attachment 1017124
Crap like any other!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo mbunge hana Akili timamu. Wakati Spika wa bunge anasema hajui, Kangi Lugola anasema hajui chochote, Katibu wa CCM anasema hajui, Kamanda Sirro anasema, hajui, Majaliwa anasema hajui, Magufuli anasema hajui, huyu kada wa CCM wa kuchongwa anasema anajua na ushahidi wote anao. Sasa serikali inashindwa nini kuuchukua huo ushahidi ili kuwaumbua CHADEMA na Lissu? Serikali sasa mmeshapata jibu, nendeni sasa BBC, VOA, CNN, DW mkamjibu Lissu.

Nitachangaa sana kama hao wote niliowataja hatajitokeza hadharani kumuunga mkono huyo Mollel.
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Back
Top Bottom