Dkt. Mollel: Ni ujinga Waziri kutoa Data za Walioathiriwa na Corona kila siku. Bei ya chanjo ni Tsh 400,000


Hakuna mpika data yoyote anayejaribu kuhadaa umma kuwa mambo ni mazuri, ambaye atakuwa tayari kutoa data za ukweli kila mara. Na isitoshe serikali hii ni ya vitu zaidi kuliko watu.
 
Abaki kwenye fani yake ya dentistry yawaachie md specialist wa internal medicine na nyinginezo watoe mchakato wa magonjwa.
Hakuna awezaye kujibu kisayansi hoja zake za kisayansi. Katumia data kuhusu matatizo ya upumuaji kuwa yapo hata kabla ya Corona na yalishika namba 2 duniani kwa kusababisha vifo.
 
Kwahio dunia nzima ni wajinga?

Ni ujinga na kukosa busara na hekima kuita wengine wajinga, kila mtu anafanya kila anachokiona ni sawa / kuita wengine wajinga sababu wanafanya tofauti na wewe ni ujinga. Kila mtu ana mbinu zake heshima kitu cha bure.
 
Kansa pia inaua na takwimu zinatolewa.

Mtu akasema kumbe ndo maana ilianza na taarifa ya mapapai kukutwa na korona kisha ziii. Vita ya uchumi ina mbinu nyingi kweli.
 
... Mbowe na genge lake ndio waliosaini mkataba wa WHO.

Your too political than a scientist
Can you re-define yourself.
Hivi ndo vichwa vinaleta matatizo kwa kuingiza siasa kwenye sayansi.
Jifanyie factory default labda utarudi kwenye normal thinking.
 
Misplaced argument!! Magonjwa yote uliyotaja ikiwemo na corona hutolewa data. Kinachotakiwa ni kutoa hizo data kwa vyombo husika, hata kama itakuwa mara moja kwa mwezi. Kama hujui hili basi wewe ni layman - data za kila siku zinaonesha upimaji na kwa kuwa upimaji unapaswa kufanyika kila siku wanakwepa hitaji hilo. Lakini kama Dr. Mollel anasema data huwasilishwa kwa mwezi - sio vibaya. Tatizo ni kutowasilishwa kabisa ili kuleta picha kuwa vifo vyote havina uhusiano na covid-19!!
 
Hakuna mpika data yoyote anayejaribu kuhadaa umma kuwa mambo ni mazuri, ambaye atakuwa tayari kutoa data za ukweli kila mara. Na isitoshe serikali hii ni ya vitu zaidi kuliko watu.
Serikali hii ni ya vitu zaidi kulilo watu! Hauna aibu?
 
Hivyo yeye Mh.Naibu Waziri ambaye ni Dr kitaaluma hafahamu kuwa kuhuisha taarifa/takwimu katika jamii inaweza kuwasaidia wengine kuchukua tahadhari zaidi,kutathmini ukubwa wa tatizo na kusaidiana kulitokomeza!Viongozi wote hata wanataaluma wasomi wanashindwa kujisimamia kuiwezesha jamii kupata uelewa mpana wanafanya siasa nyepesi nyepesi kwenye serious issues.
Sasa hivi hata watoa huduma za afya kama Madaktari,Manesi nk wanasita kuandika even provisional Diagnosis wanataja Symptoms&Signs of it?What a tragedy!
Dr.Mollel aje na takwimu,mikakati na raslimali zinazohitajika kukabili COVID 19 aache siasa.Anawalindaje watoa huduma kwa kuwapatia Uhuru wa kuelimisha jamii na kutoa Diagnosis bila kuzuiliwa ili waongeze ufanisi.
 
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Jinsia Wazee na Watoto amesema watu wengi wanasema Tanzania haitoi data, ambapo amesema data haina haja ya kutangazwa kila siku na Waziri, utakuwa ni ujinga mtupu.
Tutamfute mtu au kaburi la aliyetuloga tukamuombe AU tukaliombe msamaha!
Only ni Tz, huwezi kukuta lugha kama hii dunia nzima.
 
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Jinsia Wazee na Watoto amesema watu wengi wanasema Tanzania haitoi data, ambapo amesema data haina haja ya kutangazwa kila siku na Waziri, utakuwa ni ujinga mtupu....

Ugonjwa unapogeuzwa mtaji wa kisiasa mbona inakuwa shughuli?

Anatumia nguvu nyingi Mollel. Ni nini kinafichwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…