Dkt. Mollel: Ni ujinga Waziri kutoa Data za Walioathiriwa na Corona kila siku. Bei ya chanjo ni Tsh 400,000

Dkt. Mollel: Ni ujinga Waziri kutoa Data za Walioathiriwa na Corona kila siku. Bei ya chanjo ni Tsh 400,000

Na gharama ya sanda, Jeneza, kuchimba kaburi na kufanikisha mazishi ni shilingi ngapi?
 
Hakika kabisa mkuu,,

Jana nimepima corona amana hospital 230000 kipimo + 25000 gharama za amana hospital.


Ni noma tupu kwa sisi mabaharia.
Amaa watu mnajua kuchezea hela....[emoji848]
 
Hiyo chanjo ije.. wanaoweza wachanje, wasioweza waendelee kumuomba mungu!
 
Serikali haina hela ya chanjo, ila hapo baadae chanjo ni lazima hyo haikwepeki
 
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Jinsia Wazee na Watoto amesema watu wengi wanasema Tanzania haitoi data, ambapo amesema data haina haja ya kutangazwa kila siku na Waziri, utakuwa ni ujinga mtupu.

Amesema Data huwa inataka uchakataji ili kujua tatizo ya magonjwa yanayosababisha vifo na kujua namna ya kuyakabili.

Kwa kipindi cha karibuni kumekuwa na taharuki ambayo imesababisha kila anayefariki kupakaziwa amekufa kwa #CoronaVirus hivyo inahitajika uchakataji kujua waliopakaziwa

Amesema ili kutoua watu, mtu akienda hospitali huwa wanasema ana matatizo ya kupumua ili kwanza kujua kama anashindwa kupumua kwa tatizo la presha, nimonia, sukari au bakteria.

Msikilize:

View attachment 1709630
Yaani ni mwendo wa kucheza kwa kufuata midundo ya ile ngoma ya chattle!
 
Yani serikali imetangaza vita dhidi ya propaganda za corona sio corona yenyewe
 
Hakika kabisa mkuu,,

Jana nimepima corona amana hospital 230000 kipimo + 25000 gharama za amana hospital.


Ni noma tupu kwa sisi mabaharia.
Wanatumia kipimo gani?KILE cha zamani au hiki kipya.?
 
Tujiulize kama chanjo yao ni real sio feki kwa nini waliopata chanjo nchi zao wanawazuia wasisafiri kwenda nchi zenye Corona au zilizokataa chanjo?

mtu ukipata chanjo iwe a ndui au yellow fever ruksa kusafiri nchi yeyote hata iwe na huo ugonjwa.

wazungu wanaogopa nini si waruhusu watu wao waliochanjwa kwenda popote na ndege zao zianze kuruka kama kawaida kwenda popote duniani.

Hizo chanjo zao feki serikali ikomae hivyo hivyo hakuna kupokea chanjo hata wakiileta bure
 
Back
Top Bottom