Pre GE2025 Dkt. Mpango aomba apumzike kuwa Makamu Rais akimaliza muda wake, Rais Samia aridhia ombi hilo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Utekaji na mauaji ni haramu kwa padri.
 
Rais Samia, leo kwa maneno yake amesema Dr. Philip Mpango alimwambia anataka SASA kupumzika (yaani amechoka), hataki tena kuendelea na hiyo nafasi. Rais akakataa, lakini Dr. Mpango akamwandikia barua rasmi ya kuomba kutaka kuachana kabisa na hiyo nafasi SASA (kujiuzuru), Rais ameridhia ombi lake hilo kwa sharti kuwa itabidi amalizie miezi tisa ya utawala wake iliyobakia.

Kama hoja itajengwa kuwa, uamuzi wake huo wa kujiuzuru unahusika baada ya huu utawala kwisha Oktoba mwaka huu basi kimantiki tangazo la Rais halina mantiki na ombi hilo la Dr.Mpango halina mantiki kwa kuwa kikatiba wote (Rais na Makamu wake) mikataba yao ya kuongoza inakoma mwishoni mwa oktoba mwaka huu.

Wataalamu wa siasa, sheria, katiba hii imekaaje?
 
Sasa sheriq ya nini hapo?,wakati common sense hio barua anayoiptiisha ni rais na rais amekataa kuipitisha na kucomment inabidi amalizie miezi Tisa yake
 
Wameshindwana mitazamo au shida ni Nini?
 
Hakuna anachopoteza! Maana atakula mpaka anaenda kaburini! Mshahara ni 80% ya sitting VP gari la kifahari, nyumba nzuri atakabidhiwa, walinzi, wahudumu! Bora apumzike ale vya bure!
 
Mpango kaandika barua kwa Raisi kuomba ajiuzulu au kaandika kwa mwenyekiti kuomba kupumzika?
 
Kwa kipindi chote alichohudumu hiyo nafasi hajaisaidia Kigoma kwa chochote kile wakati wenzie wanajenga Kizimkazi.

Dr Mpango ni mzigo acha apumzike.
Mara ya mwisho kufika Kigoma ilikuwa lini?
 
Sasa sheriq ya nini hapo?,wakati common sense hio barua anayoiptiisha ni rais na rais amekataa kuipitisha na kucomment inabidi amalizie miezi Tisa yake
Yaani anajiuzuru leo kwa sababu kachoka na kazi halafu hapo hapo anaendelea kukaa ofisini kuifanya kazi ile ile mpaka mkataba wake unapokwisha. Common sense inatokeaje hapo?

Sote tunajua mtu akijiuzuru leo, basi kesho hayupo tena ofisini, na hapo hapo mtu mwingine anawekwa nafasi yake.
 
Kwa kipindi chote alichohudumu hiyo nafasi hajaisaidia Kigoma kwa chochote kile wakati wenzie wanajenga Kizimkazi.

Dr Mpango ni mzigo acha apumzike.
Mkuu
Upo Wapi
mwasenga, Buzebazeba, Kasulu, Buhigwe
Hajafanya Lolote Mimi Nasikia Buhigwe Miradi Tele
 
Mara ya mwisho kufika Kigoma ilikuwa lini?
Hata sasa niko Ujiji hapa.
Mpango acha apumzike tu,
Hana msaada wowote kwa mkoa wake wa Kigoma.

Wenzake wanapambana wabaki au wapate madaraka ili wasaidie mikoa yao na nchi kwa ujumla, yeye anakuwa msaliti anakimbia uongozi.
Acha akapumzike kwake Chanika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…