Pre GE2025 Dkt. Mpango aomba apumzike kuwa Makamu Rais akimaliza muda wake, Rais Samia aridhia ombi hilo

Pre GE2025 Dkt. Mpango aomba apumzike kuwa Makamu Rais akimaliza muda wake, Rais Samia aridhia ombi hilo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amemwandikia barua ya kuomba apumzike Umakamu wa Rais ambapo amesema baada ya kutafakari ameridhia ombi hilo.

Lakini kwa sasa Dkt. Mpango ataendelea kuwa Makamu wa Rais hadi utakapofanyika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2025.

Soma:Breaking News: - Uchaguzi 2025 - CCM yamchagua Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza katika Uchaguzi wa Oktoba 2025

Akiongea leo January 19,2025 kwenye Mkutano Mkuu Maalum Jijini Dodoma, Rais Samia amesema

""Dkt. Philip Mpango ndiye Makamu wa Rais miezi ya karibuni hapa amekuja kuniona kuniomba apumzike, ana sababu kadhaa lakini sio za kazi, anasema yeye sasa ana miaka 68 na angependa kuishi zaidi kwahiyo naomba nipumzisheni.

Nikambishia bishia Wiki iliyopita hapa akanikabidhi barua yangu hii ( ya kujiuzulu?) na barua sikumjibu, nilipoenda kwenye Kamati Kuu nikawaeleza hiyo hali na kwa pamoja wote tukakubali tumpumzishe"
Utekaji na mauaji ni haramu kwa padri.
 
Rais Samia, leo kwa maneno yake amesema Dr. Philip Mpango alimwambia anataka SASA kupumzika (yaani amechoka), hataki tena kuendelea na hiyo nafasi. Rais akakataa, lakini Dr. Mpango akamwandikia barua rasmi ya kuomba kutaka kuachana kabisa na hiyo nafasi SASA (kujiuzuru), Rais ameridhia ombi lake hilo kwa sharti kuwa itabidi amalizie miezi tisa ya utawala wake iliyobakia.

Kama hoja itajengwa kuwa, uamuzi wake huo wa kujiuzuru unahusika baada ya huu utawala kwisha Oktoba mwaka huu basi kimantiki tangazo la Rais halina mantiki na ombi hilo la Dr.Mpango halina mantiki kwa kuwa kikatiba wote (Rais na Makamu wake) mikataba yao ya kuongoza inakoma mwishoni mwa oktoba mwaka huu.

Wataalamu wa siasa, sheria, katiba hii imekaaje?
 
Sasa sheriq ya nini hapo?,wakati common sense hio barua anayoiptiisha ni rais na rais amekataa kuipitisha na kucomment inabidi amalizie miezi Tisa yake
 
Wameshindwana mitazamo au shida ni Nini?
 
siyo bure kuna kitu hapo......aache ulaji na prestige yote hiyo...never

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mgombea urais, Samia Suluhu Hassan amempendekeza Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 2025.Dk Nchimbi ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Januari 15, 2024 katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho kilichofanyikia Unguja, visiwani Zanzibar.Dk Nchimbi alichukua nafasi iliyoachwa wazi na Daniel Chongolo aliyejiuzulu Novemba 29, 2023.Rais Samia amempendekeza Dk Nchimbi leo Jumapili, Januari 19, 2025 katika mkutano mkuu maalumu jijini Dodoma.
Hakuna anachopoteza! Maana atakula mpaka anaenda kaburini! Mshahara ni 80% ya sitting VP gari la kifahari, nyumba nzuri atakabidhiwa, walinzi, wahudumu! Bora apumzike ale vya bure!
 
Mpango kaandika barua kwa Raisi kuomba ajiuzulu au kaandika kwa mwenyekiti kuomba kupumzika?
 
Kwa kipindi chote alichohudumu hiyo nafasi hajaisaidia Kigoma kwa chochote kile wakati wenzie wanajenga Kizimkazi.

Dr Mpango ni mzigo acha apumzike.
Mara ya mwisho kufika Kigoma ilikuwa lini?
 
Sasa sheriq ya nini hapo?,wakati common sense hio barua anayoiptiisha ni rais na rais amekataa kuipitisha na kucomment inabidi amalizie miezi Tisa yake
Yaani anajiuzuru leo kwa sababu kachoka na kazi halafu hapo hapo anaendelea kukaa ofisini kuifanya kazi ile ile mpaka mkataba wake unapokwisha. Common sense inatokeaje hapo?

Sote tunajua mtu akijiuzuru leo, basi kesho hayupo tena ofisini, na hapo hapo mtu mwingine anawekwa nafasi yake.
 
Kwa kipindi chote alichohudumu hiyo nafasi hajaisaidia Kigoma kwa chochote kile wakati wenzie wanajenga Kizimkazi.

Dr Mpango ni mzigo acha apumzike.
Mkuu
Upo Wapi
mwasenga, Buzebazeba, Kasulu, Buhigwe
Hajafanya Lolote Mimi Nasikia Buhigwe Miradi Tele
 
Mara ya mwisho kufika Kigoma ilikuwa lini?
Hata sasa niko Ujiji hapa.
Mpango acha apumzike tu,
Hana msaada wowote kwa mkoa wake wa Kigoma.

Wenzake wanapambana wabaki au wapate madaraka ili wasaidie mikoa yao na nchi kwa ujumla, yeye anakuwa msaliti anakimbia uongozi.
Acha akapumzike kwake Chanika
 
Back
Top Bottom