Wakuu mmesikia huko alichokisema Dkt. Mpango kuhusu Mashangazi?
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philiph Mpango, amesema zinahitajika tafiti za kina pamoja na mikakati katika kufanya mapinduzi ya kitamaduni kubadili tabia na mazoea yasiyofaa yanayojitokeza katika Jamii hivi sasa ambayo ni kikwazo kwa maendeleo.
Dkt Mpango amesema hayo wakati akifungua mkutano wa kusherehekea miaka 30 ya Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) uliyofanyika Jijini Dar es salaam ambapo ametaja baadhi ya mazoea na tabia hizo ni pamoja na kutojali muda, kutokuwa na uaminifu mahali pa kazi pamoja na kutumia njia zisizofaa katika kupata kipato.
Makamu wa Rais ameitaka ESRF pamoja na Watalaam wa Fikra Tunduizi (Think Tank) kuangazia pia tabia za hivi karibuni za Vijana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wanawake waliyowazidi umri (Mashangazi) kama njia rahisi ya kujikimu, kutumia muda mwingi bila kufanya kazi kwa kushinda Vijiweni, uchezaji kamari, utupaji taka ovyo, uchomaji moto ovyo wa nyasi na misitu pamoja na ubinafsi.
Pia Makamu wa Rais amesema ni muhimu kuangazia tabia nyingine kama vile matumizi makubwa ya fedha katika anasa kuliko kuweka akiba ikiwemo uchangiaji zaidi katika matukio ya sherehe na tafrija kuliko kusaidia gharama za elimu na matibabu kwa familia za kipato cha chini.
Soma: Kuhusu utafiti wa tatizo la ajira, Dkt. Mpango usihadae Watanzania
Swali kwa makamu rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt Mpango, serikali ya CCM imejipangaje kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja, (National economy and social development strategies of an existing government)
Kwasasa mtanzania anapambana kwa juhudi zake mwenyewe siyo kwa msaada wa mifumo ambayo kiuhalisia imelala, (unworking government machineries), mfano afisa biashara hufunga biashara bila hata kusikiliza ama kumsadia mjasiriamali azitatue changamoto za kibiashara.
Afisa biashara alitegemewa awe muelimishaji na kuzitatua changamoto ama kuzichukua na kuziwasilisha Sehemu husika kumbe hawa maafisa biashara kazi yao ni kukusanya tozo tu, (regulating and rate settings)
CCM wanatumia mfumo wa unyumbu wa kisiasa, ambao imetufikisha hapa tulipo
Unyumbu wa kisiasa ni tabia ya waliopewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga kwa viongozi wao bila utii, (unafiki), a.k.a kujizima data, tuseme, kuahirisha kufikiri kizalendo.
Madhara ya huu mfumo wa unyumbu wa kisiasa ni makubwa ukiufuatilia kiundani, husababisha, jamii kushindwa kubuni mbinu za kukabiliana na changamoto zilizopo na zitakazo kuja, matokeo yake ni jamii ya kanyaga twende, yaani jamii ambayo haiwezi kuchakata mawazo chanya na hasi, wakijitokeza wenye fikra za kuwanyang'anya washika tonge, matonge, hushughulikiwa, (ostracism).
Vijana kutembea na mashangazi Kumbe kuna haja ya kuwauliza mashangazi na vijana kuliko kukemea tu, ili tupate kiini cha tatizo, (let us find root causes that will help future generation)
Ushauri
mkiunda tume nyuma ya mikamera majibu ya tume yasiwe nyuma ya pazia
Mkituundia tume majibu mnabaki nayo wenyewe Kumbe mnatuundia tume za vunga fala kwa jamu.
Tume zikiundwa nyuma ya mikamera, majibu msiabaki nayo wenyewe pamoja na kwamba hizo tume nizakwenu na kama ndivyo ilivyo kwanini mnazitangaza hadharani
Having said that, commission of inquiries are for the public interest